Rockefeller
JF-Expert Member
- Nov 21, 2016
- 1,209
- 2,243
Kuwe na uamsho wa raia kuwa na passport, alafu masharti yasiyo ya lazima au sio ya kiusalma yapunguzweHilo nalo ni tatizo. Tufanyeje mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuwe na uamsho wa raia kuwa na passport, alafu masharti yasiyo ya lazima au sio ya kiusalma yapunguzweHilo nalo ni tatizo. Tufanyeje mkuu?
Hilo limeshapigiwa kelele sana na wenye akili lakini watawala ni kama vile wameziba masikio.Kuwe na uamsho wa raia kuwa na passport, alafu masharti yasiyo ya lazima au sio ya kiusalma yapunguzwe
Nailinganisha Tanzania na Kenya!
Kwa mwaka 2021, Tanzania yenye ukubwa wa kilomita za mraba 945,087 ilikadiriwa kuwa na watu wapatao milioni 63, wakati jirani yake, Kenya, yenye ukubwa wa kilomita za mraba 582,646 ilikuwa na idadi ya watu wapatao milioni 53.
Pamoja na Tanzania kuizidi Kenya kiukubwa mara 1.6 na kiidadi ya watu mara 1.2, bado Kenya iliipita mbali sana kwa upande wa "maokoto" yaliyotumwa na raia wake waishio ng'ambo. Kenya iliizidi Tanzania mara 6.5.
Ndiyo kusema, ingawa Tanzania imeizidi Kenya kieneo na kiidadi ya watu, Kenya inaizidi sana Tanzania kwa "maokoto" kutoka kwa raia wake walio ughaibuni.
Hiyo inamaanisha nini?
✓ Wakenya wengi wapo smart zaidi upstairs kuwazidi Watanganyika na Wazanzibar?
✓ Wakenya wanajua kung'amua fursa ambazo Watanzania hawazioni?
✓ Wakenya ni wazalendo zaidi kwa nchi yao kuwazidi Watanzania?
✓ Wakenya ina idadi kubwa zaidi ya raia wake ughaibuni kuizidi Tanzania?
Dual citizen ina faida kwa nchi kubwa zenye uchumi imara kwa nchi masikini ni janga kubwa
Wewe unaonekana ni empty handed. Saudi Arabia ina diaspora wengi sana nje lakini ni nchi tajiri sana na raia wao wanaishi maisha mazuri kuliko hata baadhi ya raia wa nchi za ulaya.1. Diaspora kubwa ni dalili ya umaskini Kwa nchi wanazotoka. Eg. Tafuta diaspora ya Botswana ulinganishe na Uchumi wao.
2. Sio sifa watu wako kuhemea nje ya mipaka wanaojielewq hutengeneza mifumo rafiki na kuvutia wawekezaji na raia nchini mwao. Wewe unashabikia Wakenya kwenda kuolewa [emoji304] ughaibuni aibu sana
NB: Ficha aibu ndogo ndogo
Kwa lugha nyingine, nchi kuwa na diaspora wengi ni ishara kuwa nchi hiyo ina raia wengi ambao vichwa vyao vimechangamka.Wewe unaonekana ni empty handed. Saudi Arabia ina diaspora wengi sana nje lakini ni nchi tajiri sana na raia wao wanaishi maisha mazuri kuliko hata baadhi ya raia wa nchi za ulaya.
Nchi kuwa na diaspora wengi haimaanishi kuwa ni masikini bali watu wanachangamkia fursa ili warudishe matunda kwenye nchi zao za asili.
Mkuu hizi mentality z a kuwa maisha bora au ili upate dola nyingi ni lazima uwe na watu wengi nje ni upumbavu inabidi tuzalishe zaidi ili tuuze nje zaidi uchumi haukuwi sababu ya kuwa omba omba ya msaada wa ndugu walio njeKenya wanaonekana wapo vizuri sana upstairs! Wakati jirani zao wakibweteka kwa kuwa na ardhi kubwa na idadi kubwa ya watu, wao na viongozi wao wanachangamkia fursa zilizopo ng'ambo.
Kwa jicho la haraka haraka, inaonekana Kenya, Rwanda na Uganda zimeipita mbali sana Tanzania kwa raia wake kufaidi vya ughaibuni!
Ni nani aliyewaloga watawala wa Tanganyika wasijue umuhimu wa kwenda "nje?"
Angalia takwimu ya mwaka 2021. Hizi ndizo dola za Kimarekani zilizoingia nchi husika kutoka kwa raia wao wanaoishi ughaibuni:
1. Kenya, dola 3,718,000,000
2. Uganda, dola 599,300,000
3. Tanzania, dola 569,500,000
4. Rwanda, dola 246,000,000
Usije ukajisifia kuwa tumeipita Rwanda! Ukilinganisha ukubwa wa Rwanda na idadi ya raia wake, hicho kiasi ni kikubwa sana. Ingawa sijaangalia, lakini inawezekana na sisi tumeipita Burundi.
Kwa takwimu hiyo, unafikiri Dual citizenship ina faida au haina?
Nitarejea baada ya muda mfupi.