- Mchango wa Sheikh Hassan bin Amir: Mohamed Said anaeleza kuwa Sheikh Hassan bin Amir, aliyekuwa Mufti wa Tanganyika miaka ya 1950 na 1960, alikuwa na mchango mkubwa kwa kuuza kadi za TANU ndani ya msikiti na kuhamasisha Waislamu kumuunga mkono Mwalimu Nyerere ili kuikomboa nchi kutoka kwa Waingereza.
- Hiana katika Uandishi wa Historia: Anadai kuwa waandishi wa historia walifanya "hiana" kwa sababu historia ya kudai uhuru ilitawaliwa sana na Waislamu, lakini jambo hilo halikuandikwa ipasavyo.
- Asili ya TANU na Nyerere: Said anafafanua kuwa Mwalimu Nyerere hakuunda TANU peke yake; aliikuta TANU nyumbani kwa Abdul Sykes (mwenye kadi namba 3). Pia, anabainisha kuwa chama cha African Association kilianzishwa mwaka 1929 na Waislamu sita, akiwemo babake Abdul Sykes,.
- Al Jamiat Islamiyya Tanganyika: Anaeleza kuwa hafla ya kumuaga Mwalimu Nyerere kuelekea Umoja wa Mataifa mwaka 1955 ilifanyika kwenye jengo la Al Jamiat Islamiyya Tanganyika. Umoja huu ulianzishwa mwaka 1933 na wale Waislamu sita walioanzisha African Association ili kusimamia mambo ya Kiislamu kando na siasa.
- Uislamu wa Chifu Mkwawa: Mohamed Said anawajibu wanaomkosoa kwa kusema kuwa Chifu Mkwawa alikuwa Mwislamu aliyeitwa Abdallah baada ya kusilimu mikononi mwa Abushiri ibn Salim, na alikuwa akijua kuandika kwa herufi za Kiarabu.
- Mashujaa Waliosahaulika: Anawataja watu kama Ali Migeyo wa Bukoba na Hamza Mwapachu kama watu ambao walistahili kuwa miongoni mwa waasisi 17 wa TANU kutokana na harakati zao, lakini majina yao hayakupewa kipaumbele katika historia ya chuo kikuu
View: https://youtu.be/SH9_SyP_w-I?si=MKGFNm5TqJ8XWOmu
Kama mapinduzi ya zanzibarEinstein,
Ndiyo historia yenyewe ilivyokuwa.
Ikiwa Mtafiti atawakwepa Waislamu atakosa uhalisia wa ukweli.
NImeomba nijibu kwa maandishi siyo videoKinyungu,
Video hiyo ukiitazama itakueleza yote katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Majibu ya maswali yako yote yako humo.
Blender,Okay.
Je wapigania uhuru walikuwa na malengo Gani ya kudai uhuru ?
Kinyungu,NImeomba nijibu kwa maandishi siyo video
Jamaa na wengineo aina yake, hutowasikia wakimtaja okello hata siku 1.Kama mapinduzi ya zanzibar
Huwezi sikia jina la John okello likitajwa
Ova
Blender,Kumbe we Mzee Mohamed Said upo kwenye payroll
Huwezi kupinga namna hiyo.Wewe Mzee ni shida sana!Maskin unaangaika sana!Waislam na uhuru,Waislam na uhuru!Kwa hakika una shida kichwani ila nadhani ni Geriatrics diseases zinakusumbua!Pumzika achana na hayo mambo!Kuwa karibu na muumba wako achana na haya mambo Mzee!
Hapo nicheke kidogoBlender,
Swali hili nawaachia wengine wajibu.
Blender,Hapo nicheke kidogo
Unataka kuongeza viewers? Mbona maswali yangu ni rahisi sana kwa mtafiti kama wewe kama unavyojiita. Naomba unijibu kwa maandishi. Kama haiwezekani pia niambie🙏🏾Kinyungu,
Video hiyo ukiitazama itakueleza yote katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Majibu ya maswali yako yote yako humo.
Sasa hapa unataka kutangaza tununue tu kitabu hakuna kitu kingine.Kinyungu,
Ikiwa unataka majibu kwa maandishi soma kitabu cha Abdulwahid Sykes.
Allen,Nadhani Kinyungu na wenzako mnatafuta sindano katikati ya lundo kubwa la uchafu jalalani.
Mzee Mohamed Said kachangua kuidadavua historia ya Uhuru wa Tanganyika kwa kuegemea ushiriki wa waislamu kwenye kupigania uhuru.
Bahati mbaya kwa mnaompinga, taaluma inaruhusu uchambazi wa aina hiyo. Maana wengine wanaweza kuja na uchambuzi wa makuli, wauza vitumbua, wanawake, wamanyema na kadhalika jinsi walivyoshiriki kupigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini kasoro ya maandiko ya Mzee Mohamed ni pale anapoweka Dhana kuonesha kwamba ni kama waislamu wamedhulumiwa kutokuwekwa kwenye historia ya Uhuru wa Tanganyika.
Bahati mbaya sana, anaiweka hiyo dhana kiuchochezi kama vile kulikuwa na mpango mahsusi wa kuifuta historia ya waislamu kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika.
Na yeye ni miongoni mwa waanzilishi na mfuasi mtiifu wa dhana ya "mfumo kristu" dhana dhaifu isiyo na mashiko lakini inayoshadadiwa na baadhi ya watu.
Mhusika Mkuu (Main character) kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika ni Mwalimu Julius Nyerere. Na ipo hivyo Dunia nzima.
Hivi watu wanapowasifu Christiano Ronaldo au Lionel Messi huwa wanakuwa wanapuuza michango ya wachezaji wengine waliowafanya Messi na Ronaldo kuwa maarufu?
Kinyungu,Sasa hapa unataka kutangaza tununue tu kitabu hakuna kitu kingine.
Dzigbone,Ukiachana na ulevi wa POMBE kuna huu ulevi wa UDINI.