Kwangu Mimi kujikita upande mmoja siyo tatizo, kitu pekee nisichokubaliana nacho ni kuonesha kwamba hao ndugu zake wa Kariakoo kutokutajwa kwao ulikuwa ni mpango maalum wa kuipoteza historia ya mchango wao.
Jambo la pili ukisoma na kusikiliza hoja zake ni kama anajaribu kudogosha mchango wa Mwalimu Nyerere kwenye kupigania Uhuru wa Tanganyika.
Na kawapata wafuasi wa kutosha wanaoanza kuamini mchango wa hao anaowapigia chapuo ni mkubwa sana kuliko wa Mwalimu Nyerere.
Na amefanikiwa kujenga dhana kuwa Mwalimu Nyerere alipokuja Dar es salaam alikuwa "mshamba" na alioneshwa mji na wazee wa Kariakoo.
Mtu aliyetoka Edinburgh kusoma anakuwa hajui mambo mengi kuliko hao wazee wake anaosema walimtoa ushamba Mwalimu Nyerere.