Kama Hujui Waulize Wanaojua: Historia ya Kupigania Uhuru wa Tanganyika

Okay.
Je wapigania uhuru walikuwa na malengo Gani ya kudai uhuru ?
 
Wewe ni mtumwa wa dini—nothing else!

Neither religious identity nor ethnic identity was a factor in the fight for independence. The movement was totally blind to anyone’s religious faith or ethnicity.

Wewe hii emphasis ya Uislamu wa mtu ndani ya harakati za ukombozi wa Tanganyika unaipata wapi?

Give us a break please!
 
Wewe Mzee ni shida sana!Maskin unaangaika sana!Waislam na uhuru,Waislam na uhuru!Kwa hakika una shida kichwani ila nadhani ni Geriatrics diseases zinakusumbua!Pumzika achana na hayo mambo!Kuwa karibu na muumba wako achana na haya mambo Mzee!
Huwezi kupinga namna hiyo.
 
Nadhani Kinyungu na wenzako mnatafuta sindano katikati ya lundo kubwa la uchafu jalalani.

Mzee Mohamed Said kachangua kuidadavua historia ya Uhuru wa Tanganyika kwa kuegemea ushiriki wa waislamu kwenye kupigania uhuru.

Bahati mbaya kwa mnaompinga, taaluma inaruhusu uchambazi wa aina hiyo. Maana wengine wanaweza kuja na uchambuzi wa makuli, wauza vitumbua, wanawake, wamanyema na kadhalika jinsi walivyoshiriki kupigania uhuru wa Tanganyika.

Lakini kasoro ya maandiko ya Mzee Mohamed ni pale anapoweka Dhana kuonesha kwamba ni kama waislamu wamedhulumiwa kutokuwekwa kwenye historia ya Uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya sana, anaiweka hiyo dhana kiuchochezi kama vile kulikuwa na mpango mahsusi wa kuifuta historia ya waislamu kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika.

Na yeye ni miongoni mwa waanzilishi na mfuasi mtiifu wa dhana ya "mfumo kristu" dhana dhaifu isiyo na mashiko lakini inayoshadadiwa na baadhi ya watu.

Mhusika Mkuu (Main character) kwenye kupigania uhuru wa Tanganyika ni Mwalimu Julius Nyerere. Na ipo hivyo Dunia nzima.

Hivi watu wanapowasifu Christiano Ronaldo au Lionel Messi huwa wanakuwa wanapuuza michango ya wachezaji wengine waliowafanya Messi na Ronaldo kuwa maarufu?
 
Hapo nicheke kidogo
Blender,
Kucheka kidogo ni kitu kizuri katika maisha.

Mimi hucheka kidogo pia.

Kinachonichekesha ni hizi ghadhabu ninazoziona hapa namna ninavyoshambuliwa kwa maneno ya dharau, "We Mzee."

Huku ni kujaribu kunidhalilisha.

Lakini kwa makuzi niliyokulia mimi mzee anaheshimiwa kwa umri wake haiwezekani kijana akamkejeli mtu mzima au mzee kwa umri wake.

Mimi sioni vibaya kuitwa mzee kwani hiyo ndiyo nafasi yangu katika jamii.
Hutazama nyuma nikacheka kidogo peke yangu:



Blender,
Ndoto yangu ilikuwa siku moja nitavaa jezi ya Sunderland kisha jezi ya timu ya taifa.
Haya hayakuwa.

Basi hujichekea.
Allah alikuwa kanipangia mambo mengine bora kuliko mpira.


London

Paris

Bwana Blender,
Nimezunguka sana dunia na nikiangalia nyuma nacheka kidogo.

Zaidi hucheka hapa ninapoona natukanwa kwa uzee wangu.
Huwa najiuliza huyu anaenikejeli ana umri gani?

Je katika huo ujana wake analo ambalo akiwa mzee ataangalia
nyuma na kucheka angalau kidogo?
 
Kinyungu,
Video hiyo ukiitazama itakueleza yote katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Majibu ya maswali yako yote yako humo.
Unataka kuongeza viewers? Mbona maswali yangu ni rahisi sana kwa mtafiti kama wewe kama unavyojiita. Naomba unijibu kwa maandishi. Kama haiwezekani pia niambie🙏🏾
 
Allen,
Unaweza kunifahamisha kwa nini historia ya uhuru ilipinduliwa ikaandkwa vinginevyo?
 
Sasa hapa unataka kutangaza tununue tu kitabu hakuna kitu kingine.
Kinyungu,
Sina sababu ya kufanya hivyo kitabu hiki kina miaka 28 na kimechapwa
mara nne tunakwenda toleo la tano.

Kitabu kimependwa mno.
 
Ukiachana na ulevi wa POMBE kuna huu ulevi wa UDINI.
Dzigbone,
Nimeweka hapa mfano wa udini na nitarejea tena:




Nadhani mabango ya maandamano ya Waislamu dhidi ya NECTA
yanaeleza nini udini.

Mimi nimeandika historia ya mchango wa Waislamu katika kupigania uhuru.

Kuandika na kusahihisha historia iliyojwa si sawa si udini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…