Kama huna huruma, utu na imani tembelea hospitalini

Kama huna huruma, utu na imani tembelea hospitalini

Niongezee pia

Kama unataka uthibitisho wa Mungu hayupo ni hospitali pia.
 
Kuna siku kaka yangu alikua anaumwa akalazwa.Mm napeleka chakula jirani na kitanda cha bro kuna jamaa kalala pale namuuliza bro mbona jamaa km hana msosi hapo hata maji akaniambia huyo nilimbakizia msosi asubuhi sema maumivu tu makali yananisumbua nikasahau kukuambia mletee nae msosi..nilitoka fasta nikaenda kumnunulia msosi plus maji na matunda nikampelekea mshikaji alishukuru mpaka nikaona km kanioma mm malaika.Sio siri kuna watu jamani wanapitia shida acheni tu.
 
Sikuwahi kwenda Hospital kuangalia wagonjwa,,mwaka 2018 jamaa yetu mama yake alikua anaumwa nikaenda kumuona,nilio ona hospital nilisikitika Sana,nilikua mpole Mwezi mzima, ukienda hospital Kila Mwezi lazima ubadilike,

Kuna Mzee Kitaa alikua Swala Tano(RIP) Kila siku Mke wake anapika Uji Sufuria Kubwa Sana,, asubuhi Mzee anapeleka uji Hospital kwa wagonjwa wasio na uwezo Wala ndugu,hiyo ratiba ilikua DAILY Hadi anakufa...
 
Back
Top Bottom