Kama huna kiwanda ndani, umeme wa jua ni rahisi na wa uhakika?

Kama huna kiwanda ndani, umeme wa jua ni rahisi na wa uhakika?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Hello!

Umeme wa jua ni bora na ninatamani Watanzania wote wangekuwa nao.

Ukinunua system ya umeme wa jua kwa sh.laki nane unaweza kutumia kwa matumizi ya friji dogo la nyumbani, ukawasha TV, redio, ukanyoosha nguo and so.

Hakuna kulipa kila mwezi kama zamani au kukosa umeme kwakuwa luku imeisha.

Ukiweka system ya milioni 2 unaweza kuwasha ma friji mengi, ukavuta maji chini nyumba yako isikatike maji na hawa dawasa sijui dawasco na TANESCO ukaishia kuwasikia redioni tu.

Solar energy is simple and reliable source of power.

Mimi sio fundi wala siuzi vifaa vya solar. Sitangazi biashara bali nawahamasisha tu tutumie umeme wa jua, hauishi na ni salama
 
Naam mkuu upo sawa sawa maana kutokana na mazingira halisia umeme jua tunabidi tuutumie ipasavyo:

Changamoto ni kwenye gharama za vifaa japo ukijipanga unaanzaa mdogo mdogo:

1. Kuvuta paneli 3 za watt 150 (450)
2. Unaenda kwa charger controller (victron)
3. Unaenda kwenye betri 12v au 24v
4. Inveter kama unahitaji kutumia vifaa (tv,pasi,n.k)
5. Viambatanishi kama taa n.k

Maana kwa majengo yanayopatikana ukanda wa pwani yanahitaji nishati kubwa katika
1. Kupoza jengo 47%
2. Mwanga kwenye jengo 40%
3. Vifaa (pasi,tv,n.k)hutumia takriban 13%
 
Usiogope, inawezekana

Mimi nimefunga January mpaka leo iko vizuri, hakuna mabadiliko. Au ulifunga huu umeme wa zola wa mkopo?
Solar Kuna kipind huwa inachoka na kuwa kero mwanga unaanza kuwa hafifu hata frij itashndwa kfnya kaz ipasavyo na badae hata taa zinazimika kabla hakujakucha umeme sahiv kuvuta ni 27k tu kama huduma ipo karbu na ww unaweza kuvuta tu hzo solar zinasaidia huko vjijin sehem ambayo haina umeme
 
So long unasema wewe sio fundi, naelewa kuwa you have no clue kwenye solar systems.

Yani system ya milioni 2 iwashe friji nyingi na water pump? Ingekua hivyo tusingehangaika na Tanesco

Umeme wa jua ni bure kimatumizi lakini unafaa kwa matumizi madogo tu ya kuwasha taa na TV, kwa matumizi makubwa kama hayo uliyotaja investment cost ni kubwa sana up to 10 million na bado maintenance costs ipo kwa sababu ukiwa na matumizi makubwa battery life span inashuka kiasi cha kuhitaji replacement hata kila mwaka

Mimi ni fundi na pia nina kiwanda kidogo nyumbani chenye matumizi ya 1.5Kwatts tu lakini batteries 10 za 100Watts zikiwa full charged (mpya) haziwezi run hiyo load kwa zaidi ya 8 hours

Fikiria ukitaka kuendesha such load for 24hrs utahitaji betri ngapi na panels ngapi?

Wewe unaongelea water pump na friji nyingi
 
So long unasema wewe sio fundi, naelewa kuwa you have no clue kwenye solar systems.
Yani system ya milioni 2 iwashe friji nyingi na water pump? Ingekua hivyo tusingehangaika na Tanesco

Umeme wa jua ni bure kimatumizi lakini unafaa kwa matumizi madogo tu ya kuwasha taa na TV, kwa matumizi makubwa kama hayo uliyotaja investment cost ni kubwa sana up to 10 million na bado maintenance costs ipo kwa sababu ukiwa na matumizi makubwa battery life span inashuka kiasi cha kuhitaji replacement hata kila mwaka
Mr. System ya milioni 2 inaweza kuwasha friji mpaka tatu. Au ukawasha moja huku unavuta maji ardhini kwa matumizi ya nyumbani.
Nimefunga hiyo ya m.2 ninapata maji na friji inanguruma ndani.
 
Ni kweli isipokuwa initial costs are expensive. Ingawaje kuna matajiri wakubwa wengi ndio wanatumia
 
Mr. System ya milioni 2 inaweza kuwasha friji mpaka tatu. Au ukawasha moja huku unavuta maji ardhini kwa matumizi ya nyumbani.
Nimefunga hiyo ya m.2 ninapata maji na friji inanguruma ndani.
Ni porojo tu,

Weka facts hiyo system ina panel ya watts ngapi, na batteries ngapi za capacity gani. Kama mtaalam tutapiga hesabu hapa kujua output wattage halafu tulinganishe na wattage ya load kujua inaweza kuendesha hiyo load kwa muda gani

Tatizo kubwa kwenye mitandao watu mnaishi maisha ya kuigiza
 
hii kitu ya ghali sana na sumbufu sana kufikia kunyoosha nguo kwa pasi ya 220V au kuna pasi ya 12v mimi nimekaa nayo kwa miaka 4 tu imepiga mzinga
Pasi ya 12v ipo lakini haina maana kuwa ndio inapunguza matumizi, heating element inahitaji wattage kubwa na high current, hata ukitumia pasi ya 12v huwezi kuitumia kwa zaidi ya dakika 30 kwenye betri ya 100watts
 
Mimi ni fundi na pia nina kiwanda kidogo nyumbani chenye matumizi ya 1.5Kwatts tu lakini batteries 10 za 100Watts zikiwa full charged (mpya) haziwezi run hiyo load kwa zaidi ya 8
Mtaalamu, 1.5kW ni kiwanda cha kufanya nini tena? Tuna pasi zenye mpaka 2.4kW, heater kwa matumizi madogo ya nyumbani ya mpaka 0.89kW.

Nikiwasha vyote vinavyotakiwa kwa usiku, bila pasi na radio hapa home, inasoma 1.39kW

1.5kW au 15.0kW?
 
Back
Top Bottom