Kama huna kiwanda ndani, umeme wa jua ni rahisi na wa uhakika?

Kama huna kiwanda ndani, umeme wa jua ni rahisi na wa uhakika?

Mkuu umeme kuwa AC haimaanishi kuwa ndio una nguvu zaidi. Kubadilisha umeme wa solar ambao ni DC kuufanya AC ni rahisi tu. Ndio kazi ya Inverter hiyo.

With enough panels and batteries, hakuna ambacho huwezi kuendesha kwa kutumia solar

Tesla ameshafunga power back up yenye uwezo wa 100MW kwa kutumia battery. Huo umeme unatumika kuwasha South Australia na vitu vyote watu wanavyotumia.

Fatilia zaidi utaona teknolojia ya battery iko mbali sana.

View attachment 1867857
Jamaangu mimi nafahamu umeme. Na fani yangu ina uhusiano na umeme japokua sio uhandisi wa umeme.

Nimesoma na kufanya practicals za umeme toka Tachnical School mpaka uni.

So ninajua habari ya AC, DC inverter nk

Mimi nilichouliza katika ngazi ya commercial(ina maana feasible kiuchumi) kwamba una uhakika kuna betri kama hizo zinapatikana?

Achana na ngazi ya utafiti (Elon Musk unayemsema) kwasababu yule yuko kwenye R&D bado
Kama una taarifa za mtu yeyote au sehemu yeyote ambapo raia anafanya hayo na anaokoa gharama kuliko umeme wa Tanesco naomba unijulishe. Nitafurahi sana kujifunza mkuu
Bado sijawahi kukutana nayo katika soma soma yangu na kujifunza
 
Mkuu Culminate, in theory solar inaweza endesha kila kitu, problem hapa ni cost. project uliyo-sight hapo ina faidika na economy of scale. watu wengi wamesema humu Tanesco ni cheap, ni cheap kwa sabau ya economy of scale. ingekuwa kila mtu anazalisha kwenye kijumba chake ingekuwa ghali pia. Hivyo kwa mfano Tanesco wakiamua (najua wanampango huo tayari) kuzalisha umeme wa solar kwa kiwango kama hicho pia utakuwa rahisi. Battery kwa sasa ndiyo kikwazo kwa solar. mimi nimefanya feasibility study ili nitumie solar nyumbani kwangu nikalinganisha actual cost ya solar (upfront cost + maintenance) kulinganisha na Tanesco (upfront cost + monthly tariffs) nimeamua solar uwe backup only
Yes nakazia hapa. Ndomaana nadhani hatukuelewana na Jamaangu huyo

EDIT:
Najazilizia kwa mfano umeme was tanesco wangekua wanazalisha halafu wanauhifadhi ndo tunanunua ingekua kichefuchefu pia. Tanesco wanaweza kuufanya tuweze kumudu kwakua unazalishwa unasambazwa unatumika.

Kitu kinachoicost solar ni pale kuhifadhi utumike usiku na rainy days. Ndo nilichokua nasema teknolojia ya betri bado hapo

Ukiachana na mambo mengine kama eneo kuhitajika kubwa kwa ajili ya hizo panels nk nk

Japokua teknolojia imekua sana katika uzalishaji. Ukiangalia panels za miaka ya 2000 mwanzoni zinazozalisha watt 50 labdanum na za sasa kuna improvements ila umeme was solar kuwa commercially viable(Comparing na vyanzo vingine ) Nadhani bado sana kwa sasa (Kwa maoni yangu)
 
Solar ni pasua kichwa, hasa ukitumia hizi za 'kichina'

Ukitaka ufanisi wa hizi system chukua panel za 'mono' badala ya 'poly-crystalline'

Panel za 'mono' hata kukiwa na mawingu mawimgu, inavuna jua la kutosha, bei za mono ni parefu mno

Controller chukua za 'mppt', achana ujinga ujinga wa izi za 'pwm', jiandae na bei pia, 'mppt' inakosti mara 6 nzima ya 'pwm' kwa kiwango kile kile cha current, ila hutajutia

Achana na 'inverter', chukua vifaa vinavyotumia DC mf: tv ya DC, friji la DC, nk

Ukifata huo mwongozo, unadunda nayo vizuri sana
 
Mkuu Culminate, in theory solar inaweza endesha kila kitu, problem hapa ni cost. project uliyo-sight hapo ina faidika na economy of scale. watu wengi wamesema humu Tanesco ni cheap, ni cheap kwa sabau ya economy of scale. ingekuwa kila mtu anazalisha kwenye kijumba chake ingekuwa ghali pia. Hivyo kwa mfano Tanesco wakiamua (najua wanampango huo tayari) kuzalisha umeme wa solar kwa kiwango kama hicho pia utakuwa rahisi. Battery kwa sasa ndiyo kikwazo kwa solar. mimi nimefanya feasibility study ili nitumie solar nyumbani kwangu nikalinganisha actual cost ya solar (upfront cost + maintenance) kulinganisha na Tanesco (upfront cost + monthly tariffs) nimeamua solar uwe backup only

Mkuu hapo juu alikuwa na wasiwasi na battery. Ndio maana nikawa naeleza kwamba teknolojia ya betri imefika mbali na inaendelea kuimarika, hivyo si kikwazo sana kwa solar.

Sasa kama ni ishu ya economics of scale. At indidual level, ni kweli solar ina gharama. Panel, charge controller na battery zenye ubora ni bei yake ipo juu.

Lakini bado zipo faida nyingi za kutumia umeme wa solar

(i) Huu ni umeme wako mwenyewe. Unazalisha mwenyewe, unatumia mwenyewe. Ukiwa na solar huna haja ya kuhofia umeme kukatika. Hivyo, una uhakika na umeme wako.

(ii) Hupati hofu ya kupanda kwa gharama za umeme wala kuongezewa kodi usizozitarajia.

(iii) Unaunga mkono juhudi za kutunza mazingira. Kila mtu akiwa na solar hatutakuwa na haja ya kuwa na nguzo wala transformers zenye umeme mkubwa huku mitaani.

Watu wengi wanaweka kwa sababu hizi.
 
Jamaangu mimi nafahamu umeme. Na fani yangu ina uhusiano na umeme japokua sio uhandisi wa umeme.

Nimesoma na kufanya practicals za umeme toka Tachnical School mpaka uni.

So ninajua habari ya AC, DC inverter nk

Mimi nilichouliza katika ngazi ya comercial(ina maana feasible kiuchumi) kwamba una uhakika kuna betri kama hizo zinapatikana?

Achana na ngazi ya utafiti (Elon Musk unayemsema) kwasababu yule yuko kwenye R&D bado
Kama una taarifa za mtu yeyote au sehemu yeyote ambapo raia anafanya hayo na anaokoa gharama kuliko umeme was tanesco naomba unijulishe. Nitafurahi sana kujifunza mkuu
Bado sijawahi kukutana nayo katika soma soma yangu na kujifunza

Mkuu, i was simply emphasising a point kuwa solar inaweza kutumika kwenye kila kifaa kinachotumia umeme wa kawaida.

Gharama ni kweli ziko juu lakini zinakuja na faida nyingine ambazo huwezi kuzipata kwenye umeme wa Tanesco.

Kama ukiwa na vyanzo vyote viwili ni nzuri zaidi lakini kwa ambaye hana chaguo solar itamfaa. Na akifungiwa mfumo mzuri anaweza asione tofauti yoyote na umeme wa Tanesco.
 
Okey nimekusoma mkuu

Ngoja niendelee kusoma na wachangiaji wengine. Actually it's very interesting kupata maarifa mapya unaweza kujikuta unapata mkombozi wa luku
 
solar ni pasua kichwa, hasa ukitumia izi za 'kichina'

ukitaka ufanisi wa hizi system chukua panel za 'mono' badala ya 'poly-crystalline'

panel za 'mono' hata kukiwa na mawingu mawimgu, inavuna jua la kutosha, bei za mono ni parefu mno

controller chukua za 'mppt', achana ujinga ujinga wa izi za 'pwm', jiandae na bei pia, 'mppt' inakosti mara 6 nzima ya 'pwm' kwa kiwango kile kile cha current, ila hutajutia

achana na 'inverter', chukua vifaa vinavyotumia DC mf: tv ya DC, friji la DC, nk

ukifata huo mwongozo, unadunda nayo vizuri sana

Nashukuru Mkuu kwa kulisema hili, watu wengi wakitaka umeme wa solar wanafika pale gerezani wakiwa hawajui chochote.

Mtu amekariri tu kuwa vifaa vizuri vya solar ni vya Germany. Pale ukifika unakuta vitu vya kichina vyote vimeandikwa made in Germany. Mtu anaingia mkenge ananunua baadae anakuja kulalamika kuwa solar inazingua.

Huwez nunua charge controller ya pwn ya 30k ikawa sawa na mppt ya victron au morningstar ya 700k. Haiwezekani. Hizi controller nyingi hazina hata absorption stage unadhani battery yako itakaa kweli miaka mitano mbele.

Mtu anaambiwa solar system ya watts 200 ikiwa complete ni milioni moja na kweli anakubali kununua.

Umeme wa solar ni mzuri lakini ni gharama. Yani ni gharama kweli.
 
Nawaonaga baadhi hutumia betri za minara ya simu zilizoisha kwenye solar kwa vile tu kupata nafuu lakini kwa uzoefu wangu ninaona matajiri Wanatumia kama back up power au akiwa anasubiria ahadi za tanesco itimie lakini kwa TZ kufanywa kama ni main steam bado.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]sio zola?
 
Nawaonaga baadhi hutumia betri za minara ya simu zilizoisha kwenye solar kwa vile tu kupata nafuu lakini kwa uzoefu wangu ninaona matajiri Wanatumia kama back up power au akiwa anasubiria ahadi za tanesco itimie lakini kwa TZ kufanywa kama ni main steam bado.
Solar ya uhakika ni ghali
 
Zinakufa sekunde tu hzo unaanza kutafuta lak8 ya kufnga mpya bora uvte umeme ujipimie matmiz yako ulipe tratbu
Sio kweli,mimi huu ni mwaka wa nne 4 haujasumbua hata kidogo.Bulb mwanga hata zaidi ya Tanesco.Fanyiwa installation vizuri na mtaalamu wa solar.
 
So long unasema wewe sio fundi, naelewa kuwa you have no clue kwenye solar systems.

Yani system ya milioni 2 iwashe friji nyingi na water pump? Ingekua hivyo tusingehangaika na Tanesco

Umeme wa jua ni bure kimatumizi lakini unafaa kwa matumizi madogo tu ya kuwasha taa na TV, kwa matumizi makubwa kama hayo uliyotaja investment cost ni kubwa sana up to 10 million na bado maintenance costs ipo kwa sababu ukiwa na matumizi makubwa battery life span inashuka kiasi cha kuhitaji replacement hata kila mwaka

Mimi ni fundi na pia nina kiwanda kidogo nyumbani chenye matumizi ya 1.5Kwatts tu lakini batteries 10 za 100Watts zikiwa full charged (mpya) haziwezi run hiyo load kwa zaidi ya 8 hours

Fikiria ukitaka kuendesha such load for 24hrs utahitaji betri ngapi na panels ngapi?

Wewe unaongelea water pump na friji nyingi
Sawa bwana fundi, nahitaji muongozo kidogo nataka nifunge solar sehemu.
 
Mr. System ya milioni 2 inaweza kuwasha friji mpaka tatu. Au ukawasha moja huku unavuta maji ardhini kwa matumizi ya nyumbani.
Nimefunga hiyo ya m.2 ninapata maji na friji inanguruma ndani.
Chief unefunga ya watt ngapi, kampuni gani? Betri je? N.k
 
Back
Top Bottom