Kama huna kiwanda ndani, umeme wa jua ni rahisi na wa uhakika?

Ushauri wangu kulingana na uzoefu katika matumizi ya hizi system za umeme wa solar au tanesco.

1. Kama eneo ulilopo kuna upatikanaji wa umeme wa tanesco basi acha kufikiria solar hata kama matumizi yako ni madogo we unga tu umeme wa tanesco.

2. Kama eneo ulipo hakuna umeme wa tanesco basi nenda kwenye solar tu.

Ila kulinganisha umeme wa tanesco na solar kwa upande wa gharama, ubora na nguvu basi tanesco uko vizuri.

Tumia umeme wa solar kama alternative na sio substitute way.
 
Vipi una uzoefu wa zile taa za solar za nguzo ambazo huwekwa barabarani au kwenye fence za nyumba.?
 
With proper calculations and investment, solar ni umeme reliable sana. Lakini hapa kwenye mahesabu umechanganya mambo.
 
Bila shaka inategemea na aina ya brand na materials zilizotumika.

Au elon musk asingewekeza Billions kwenye mradi wake wa solar city.
 
Ni batteries ndio zinazochoka na sio panels.
 
Mkuu sidhani kama umeshawahi kutumia solar system iliyopangiliwa vizuri. Solar ni reliable sana. Shida ni kuwa nyingi za humu mitaani watu wanaokota tu vifaa ambavyo havina ubora. Inapoanza kusumbua mtu anakata tamaa na umeme wa solar.
 
Mkuu sidhani kama umeshawahi kutumia solar system iliyopangiliwa vizuri. Solar ni reliable sana. Shida ni kuwa nyingi za humu mitaani watu wanaokota tu vifaa ambavyo havina ubora. Inapoanza kusumbua mtu anakata tamaa na umeme wa solar.
Ishu sio vifaa kwa ujumla. Ishu tatizo la dunia nzima ni BETRI

nimeandika kwa herufi kubwa muelewe. Umeme hata uzalishe kiasi gani kwa hizo panels ukija kwenye BETRI ya kuhifadhi ili utumie ndo kuna shida. Ukiwa na matumizi makubwa BETRI zinachoka na ni gharama kubadilisha kila mud

Magari ya Umeme duniani wanahangaika na BETRI

Umeme wa solar unashindwa kuwa mainstream kwasababu ya BETRI

Simu zenyewe bado tunahangaika na BETRI

Ni swala la kiteknolojia bado sayansi haijafikia huko ila tunable kea

So usije ukajidanganya eti Umeme wa solar utatumia vitu kama wa tanesco bado sana. Solar ni alternative tu kwa sasa
 
Mkuu!

Fundi yoyote wa umeme wa solar atakubali kuwa battery ni sehemu dhaifu katika mfumo wa solar. Lakini sio dhaifu kama unavyozani wewe. Teknolojia katika utengenezaji wa battery imefika mbali sana.

Sasa hivi zipo battery zenye ufanisi mkubwa. Kiasi kwamba mpaka utakapohitaji kubadilisha hizo battery zitakuwa zimeshajilipa tayari. Hivyo hupati hasara.

Nikupe tu mfano!

1. Tesla powerwall battery inaweza kukupa mizunguko (charge-discharge cycles) 5000 na ikabaki na ufanisi wa 90%.

Kumbuka kila mzunguko mmoja ni sawa na siku moja. Kwenye mizunguko 5000 unapata miaka 13 na zaidi. Tesla wenyewe wanatoa warranty ya miaka 10. Can you imagine? Warranty ni miaka 10.

Hapo bado kuna battery za victron, delta, LG na nyingine nyingi.

Narudia tena mkuu, kama unanunua battery cheap za hapo kariakoo, utalalama kila siku.

Hapa bongo zipo battery nzuri kiasi kama ritar, na leoch. Watu hawanunui kwa sababu zina bei. Lakini ufanisi wake ni mzuri kiasi. Uliza watu wanaozitumia.
 
Hizo betri nzuri kwa kutoa mizunguko 5000 (miaka 13) kwa matumizi yapi?

Sidhani na sina uhakika labda ndo unifahamishe wewe kwamba unaweza kutumia AC kwenye nyumba friji 2 na mashine ya kuvuta maji toka ardhini
 
Mtaalamu, 1.5kW ni kiwanda cha kufanya nini tena? Tuna pasi zenye mpaka 2.4kW, heater kwa matumizi madogo ya nyumbani ya mpaka 0.89kW.

Nikiwasha vyote vinavyotakiwa kwa usiku, bila pasi na radio hapa home, inasoma 1.39kW

1.5kW au 15.0kW?
Kiwanda sehemu ya kufanyia production au manufacturing, kiwanda hakipimwi kwa matumizi makubwa ya umeme ila aina ya matumizi. Mimi natumia 1.5kw kwa masaa 24 kwa siku 365 na kwa namna yoyote sihitaji power shortage kwa hata nusu saa

Wewe unaweza kutumia hiyo 2kw lakini ikitokea shortage ya hata kutwa nzima isikuathili kwa sababu ni matumizi ya nyumbani na pia labda load yenyewe unatumia kwa masaa 8 tu kwa siku
 
Bila shaka inategemea na aina ya brand na materials zilizotumika.

Au elon musk asingewekeza Billions kwenye mradi wake wa solar city.
Kwa kutumia original quality hiyo 2M aliyosema inanunua betri 2 tu 100watts na panel moja ya 200watts

Sasa imagine capacity hiyo ndio anasema inaendesha friji, taa na water pump, How? Water pump ndogo kabisa ni 750watts

Kila kitu kiko calculated, wala haihitaji kisingizio cha aina ya brand
 
Pasi ya 12v ipo lakini haina maana kuwa ndio inapunguza matumizi, heating element inahitaji wattage kubwa na high current, hata ukitumia pasi ya 12v huwezi kuitumia kwa zaidi ya dakika 30 kwenye betri ya 100watts
ndio ndio upo sawa mkuu
 
Hizo betri nzuri kwa kutoa mizunguko 5000 (miaka 13) kwa matumizi yapi?

Sidhani na sina uhakika labda ndo unifahamishe wewe kwamba unaweza kutumia AC kwenye nyumba friji 2 na mashine ya kuvuta maji toka ardhini

Mkuu umeme kuwa AC haimaanishi kuwa ndio una nguvu zaidi. Kubadilisha umeme wa solar ambao ni DC kuufanya AC ni rahisi tu. Ndio kazi ya Inverter hiyo.

With enough panels and batteries, hakuna ambacho huwezi kuendesha kwa kutumia solar

Tesla ameshafunga power back up yenye uwezo wa 100MW kwa kutumia battery. Huo umeme unatumika kuwasha South Australia na vitu vyote watu wanavyotumia.

Fatilia zaidi utaona teknolojia ya battery iko mbali sana.

 
Price per unit si zinatofautiana kulingana na matumizi na service line uliyoomba kwa Tanesco? Sasa kwa matumizi hayo, huoni kuwa hakuna haja ya kusema ni kiwanda? Mpaka matumizi ya 10kW kwa Tanesco ni matumizi ya kawaida nyumbani.

Kama ni mita ya Tanesco, wameifunga kwenye msitimu wao au nyumbani kwako?

Moja ya kipimo cha maendeleo ni matumizi ya nishati hiyo, hivyo chini ya 10kW haiwezi kuwa kiwanda aisee.
 
Mkuu Culminate, in theory solar inaweza endesha kila kitu, problem hapa ni cost. project uliyo-sight hapo ina faidika na economy of scale. watu wengi wamesema humu Tanesco ni cheap, ni cheap kwa sabau ya economy of scale. ingekuwa kila mtu anazalisha kwenye kijumba chake ingekuwa ghali pia. Hivyo kwa mfano Tanesco wakiamua (najua wanampango huo tayari) kuzalisha umeme wa solar kwa kiwango kama hicho pia utakuwa rahisi. Battery kwa sasa ndiyo kikwazo kwa solar. mimi nimefanya feasibility study ili nitumie solar nyumbani kwangu nikalinganisha actual cost ya solar (upfront cost + maintenance) kulinganisha na Tanesco (upfront cost + monthly tariffs) nimeamua solar uwe backup only
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…