Kama huna mkono wa kufanya biashara za baa nakushauri usifanye

Kama huna mkono wa kufanya biashara za baa nakushauri usifanye

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Baa ni biashara nzuri sana kama ukipatia soko na upande fulani.

Ila biashara ya baa aina tofauti na kubeti sana. Tunaopitapita kwenye mabaa tumeona jinsi baa zilizokufa na kuibuka. Suala la baa lina changamoto nyingi kama mtu una roho ndogo au mtu wa dini bora kutulia na biashara nyingine.

Wateja wa baa ni watu wasio na shukrani yaani wakiichoka ndio basi tena. Wateja wa baa kuwapata unatumia nguvu kubwa sana ili wajae mfano kuwepo na wadada wazuri (wahudumu), watoa ofa wasioisha hapo kwako na wapambe .

Biashara za baa upande fulani zimejaa visasi kati ya wenye baa ambao wapo karibu na ushirikina sana kwa ajili ya wateja.

Kama haupo vizuri kwenye idara ya sangoma na wapambe utafunga mapema.
 
Baa ni biashara ya urafiki pia ni adui kwa mwenye mkono wa birika, pia haipendani na mwendeshaji masikini.
 
Usimamizi mzuri tu wala haihitaji kwenda kwa sangoma mkuu.
Usijidanganye maana biashara yenyewe ni ya shetani hakuna kitabu cha dini kinachobariki so usipopita vizur kujiweka vizur kwa sangoma utaishia kuifunga hyo biashara.

Hii biashara wanaiweza sana wachaga kusema ukweli jamaa biashara ya bar wameiweza sana kuiendesha kama vile wakinga na biashara ya nguo.
 
Acha kukalili, nani kasema bar ni biashara ya shetani??

Huko kwa sangoma unaenda kufanya nini? Hizi mentality za ajabu zinafanya waganga wawapige pesa kindezi kabisa.

Na unaongelea bar zilizo karibu yako au umetembea mikoa kadhaa na kuona jinsi zinaendeshwa??
Itakua upo dar wewe research yako ya dar unajumuisha Tz nzima!!.
 
Baa ni biashara ya urafiki pia ni adui kwa mwenye mkono wa birika, pia haipendani na mwendeshaji masikini.
Bar ni biashara ya kutupia mtaji kila wakati, ina demand ya hela kwenye maboresho na inarudisha hela kwa usimamizi thabiti.

Ni biashara ambayo inataka uwe na vyanzo vingine vya mapato.
 
Bar ni biashara ya kutupia mtaji kila wakati, ina demand ya hela kwenye maboresho na inarudisha hela kwa usimamizi thabiti.

Ni biashara ambayo inataka uwe na vyanzo vingine vya mapato.
Uko sahihi kwa 100 %. Just a leisure business!
 
muulizeni lava lava.alifanya Fujo pale mapinga akaondoka kimya kimya.
Alfungisha platinum bar.
Platinum akapangisha baa.
Basi ilipofunguliwa Tena watu wote wamekimbia kwa lava lava wameenda platinum.
Biashara ya baa wateja wao ni misukule
 
Kuna mpenda shangwe, mwingine mzinzi, mwingine Mla unga, mwingine ana ulevi wa smatifone, 24hrs anachati all this are.....!
 
Msitutukane wanywaji. Mambo gani kuitana misukule
Tunatumia pesa zetu na hatujawaomba. Kwani nyie huwa mnakunywa juice au soda duka moja!
Ukifungua bar tukaja kunywa kwako haimaanishi bar yako ni chama na sisi ni wanachama. Hapana, sisi ni wateja tu, na moody siku hiyo ikitaka kwenda kwingine usikasirike. Wewe weka huduma na mazingira vizuri
 
Back
Top Bottom