Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Kwa miaka michache niliyopata kuishi Duniani niliweza kugundua kuwa hii dunia ina vigezo na masharti vinavyozingatiwa, ukiwa huna Vigezo hivyo na Kama hutofuata masharti jua utaendelea kubaki kulialia na kuwa msindikizaji.
Dunia inatisha Ila nilikuambia usiogope.
Tangu nikiwa mdogo nilisikia watu wakilalamika, mpaka napata Akili na kujiita Taikon bado watu walewale wanalalamika kilichobadilika ni ongezeko Lao kwani wasindikizaji huzaa na kuzaliana,
1. Mtu unalialia hakuna Ajira alafu hujasoma hii inafurahisha Sana, hata Ajira zikitoka wataajiriwa waliosoma, Mimi na Wewe madarasa madogo tutaendelea kuwa wasindikizaji.
Hili suluhusho lake ni kusoma, Taikon anawaambia watu kutoka jamii masikini, somesheni watoto wenu kivyovyote, iwe kihalali au kuiba mitihani, kivyovyote mtoto wako asome, maisha huko mbeleni hayataangalia ulikuwa mtenda haki au vipi.
Nina ushahidi wa kutosha juu ya hili, wale walioambiwa wameiba majina miaka Ile ili watoto wao wafaulu leo hii watoto haohao ndio maafisa, linapokuja suala la maisha usiogope, usiwe mzembe mzembe,
Usijejidanganya elimu haina msaada, utakuwa mjinga wa mwisho kabisa, Elimu ni elimu tuu, mpe mtoto wako Elimu ikiwa wewe ulizembea, dunia hii ni ya waliosoma na wenye vipaji.
2. Kuna watu walikuwa wakilia ukame, hakuna mvua lakini mvua zikinyesha hawana hata mashamba, wanaopata chakula ni walewale hasa wenye mashamba ndio wanakula maisha
Hilo Taikon alishalitambua angali yupo shule ya Msingi, nilisoma Biblia vyakutosha ningali sijabalehe, vita karibu zote za Biblia ilikuwa kugombea Ardhi, nilipokua kidogo nikiwa sekondari nikasoma mambo ya Ukoloni kisha vita karibu vyote vya kihistoria sababu kuu ni kugombea Ardhi, Ardhi ni kitu cha thamani,
Kijana hakikisha unapata Ardhi kadiri uwezavyo, iwe mjini au kijijini, iwe visiwani au barani, kufa kupona upate Ardhi,
Ardhi ndio Urithi wapekee Kwa watoto na wajukuu, mnyime mtoto yote lakini usimnyime Ardhi,
Ukilima huwezi kukosa chakula abadani, Babu yangu, Mzee Clifford Tenga aliyekuwa diwani Kisiwani, Same aliwahi kuniambia; Ukishakuwa na Shamba maisha hayawezi kukusumbua, Hakikisha hata Kama unakazi gani usiache Kulima"
Mungu ailaze Roho yake mahali panapomstahili, nilikuja kumuelewa baadaye nilipomaliza chuo.
Nami bila uchoyo nasema, ukiwa na Shamba maisha hayawezi kukushinda abadani.
3. Wengi wanalialia kusumbuliwa na wenza wao, wanawake wanasema wanaume siku hizi wamebweteka, hawana sifa za kuitwa wanaume.
Huku wanaume nasi tukisema, wanawake WA siku hizi hawana sifa za kuwa mke.
Lakini katika Hilo usipokuwa na vigezo na masharti kwenye ndoa pia utakuwa msindikizaji na hutoacha kulialia.
Mwanamke lazima ujitambue, ujue ukoje na unastahili mwanaume wa Aina gani, halikadhalika na kwetu wanaume.
VIGEZO ni muhimu kuliko Jambo lolote kwenye maisha,
Sio utake mwanamke asiye WA kiwango chako atakusumbua, au sio uchukue mwanaume asiye WA kiwango chako atakusumbua.
Ndio Yale mtu anaona aibu kumtambulisha Mke au mume wake mbele ya watu, kisa vigezo havijadhingatiwa, dunia huwaga inatabia ya kuweka kila kitu sehemu yake, mahali panapostahili, ukijifanya kujiseti usipotakiwa Dunia itakuweka sehemu yako Kwa maumivu makali Sana.
Ngoja nipumzike kwanza,
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam