Kama huna Vigezo, hii Dunia utakuwa msindikizaji na kulialia!

Sahihi kabisa.
 
Wewe Ukilialia wenzio wanatoboa kupitia kilio chako wanakuacha uendelee kulia tena watoboe tena,Mwisho unazeeka unalia.
 

Nakubaliana na wewe.
Ila zingatia kuwa sio kila Uovu utaadhibiwa nao, na wala sio kila wema utabarikiwa nao
 
Leo umeandika madini.

Ila tofauti kati ya R na L inasumbua wengi
 
Sahihi kabisa Kuna watu tulilalamika na kulialia kwamba Magufuli mbaya , lakini Kuna watu walitoboa na kuneemeka, kaingia mama wakati wengine wanalia lia Kuna wengine wanasema mama anaupiga mwingi na wananeemeka pia. Wakati wengine wanalia lia kuhusu vita ya Ukraine na Russia kuwa imepandisha gharama za maisha kitu ambacho ni kweli lakini Kuna wengine hizo gharama zilizopanda wamepanda nazo huko huko juu.

Nilichojifunza yatupasa kugangamala/ kukomaa regardless maisha yamebadilika kwa namna gani au Hali imekaaje.

Kuhusu ardhi ni kweli na ndio asili ya mafanikio ambayo Mungu ameachilia kwa mwanadamu tangu kuumbwa kwake, tutafute ardhi kwa ajili ya kuwarithisha watoto wetu, Kuna baadhi ya wazazi kwa uvivu ama kuto kujua wanawaambia watoto wao kuwa mwanangu nimekusomesha, elimu ndio urithi wako kitu ambacho sio kweli elimu haijawahi kuwa urithi popote bali ardhi na mali zingine zisizohamishika ndio urithi. Bibilia unasema Baba mwema huacha urithi kwa watoto wake.
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Na wengi wanaotenda uovu hufanikiwa angalia wazungu walituuwa na kututawala wala hawajapata laana ndyo kila siku wanafanikiwa matajiri wakubwa wanafanikiwa Kwa kuiba na kupora Kwa wengine dunia hii bila roho ngumu huwezi fanikiwa wala kutoboa wengi waliofanya maamuzi magumu ndyo hufanikiwa ukijifanya kunyenyekea watu na kuwanusa matako utabaki ivyoo ivyo sikuzote
 
Kwa hiyo hapa umekufa maana sijaelewa
 
Cha kusikitisha kizazi cha sasa hivi ingawa siyo wote ukiwaachia urithi ukifa wanauza.

Nimeliona hili sehemu nyingi sana na hakuna ambaye nimeona akiuza nyumba ya urithi zile pesa zikaja kuzaa mali nyingi zaidi, binafsi sijawahi kumuona aliyetobowa kwa kuuza urithi aliorithi.
 
Hilo ndio janga la wavivu wanafikiri katika kuuza Sio kuendeleza, ingefaa sana tungejikita kuendeleza vya urithi mahangaiko na tabu zisingekuwa kubwa, ushaambiwa jasho la Mtu haliliwi ndio Maana wanaouza hizo nyumba huwa hawafanikiwi
 
Tatizo unaweza kujiona unavigezo kumbe hivyo siyo kabisa.Sasa nani ahakikishe kuwa ulivyonavyo ndiyo sahihi,hayupo.
Maisha hayatabiriki!
Leo king msukuma ndo anaoneka kuwa na vigezo!!??
Uliyoyataja yaweza kusaidia kwa kiasi chake lakini si kusema kwamba ukiwa na hayo ndo ushayapatia maisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…