Kama hutumii mbinu hii katika biashara bado wewe sio mfanyabiashara bali mjaribu biashara

Kama hutumii mbinu hii katika biashara bado wewe sio mfanyabiashara bali mjaribu biashara

totob

New Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2
Reaction score
14
Habari wadau!

Kama hutumii mbinu hii katika biashara bado wewe sio mfanya biashara bali mjaribu biashara.katika biashara hakuna kitu muhimu kama” BRANDING”,unapoamua kufanya biashara jambo la kwanza muhimu ni kutengeneza brand yako,siku zote katika biashara bidhaa hutofautiana ubora kidogo sana lakini kinachotafautisha sana ni” BRAND”, Brand ni utambulisho na imani kwa mteja, hata uwe na bidhaa nzuri kiasi gani lakini kama hujui kutengeneza brand hutofika mbali kibiashara, na brand huanzia biashara za aina zote,hata iwe ndogo kiasi gani inahitaji brand ili iweze kukuwa na kuwa endelevu,ngoja nikupe kidogo mfano wa madhara ya kutokuwa na brand.

,”kuna bwana mmoja aitwae ATHUMANI alifungua duka lake la nafaka na kuweka mfanyakazi wake aitwaye JOHN,Duka lilipokelewa vizuri mtaani wateja wakawa wengi lakini kwa kuwa Duka halikuwa na jina wateja waliliita Duka la JOHN kwa sababu yeye ndiye walikuwa wakifahamu akiwahudumia na walidhani yeye ndio mwenye Duka,wateja walikuwa wakisambaza taarifa kwa watu wa mitaa mingine wakiwambia waende kwenye duka la JOHN watapata mahitaji ya bidhaa zao, lakini baada ya mwaka mmoja mmiliki wa duka bwana ATHUMANI aliamua kumfukuza kazi bwana JOHN baada ya kugundua kuwa alikuwa akimuibia katika duka lake, na bwana ATHUMANI akaamua kukaa mwenyewe dukani lakini bwana JOHN alipofukuzwa kazi akaamua kufungua na yeye Duka lake mtaani hapo hapo hivyo wateja wake waliamua kumfuata huko huko alikohamia kwa sababu jina lake lilishakuwa BRAND na upande wa pili Bwana ATHUMANI Duka lake lilidorola,kwa sababu wateja waliamini JOHN kashahama hapo na yeye ndiyo alikuwa mwenye duka”,Moja kati ya kosa wanalolifanya baadhi ya wafanya biashara ni kuruhusu biashara kumilikiwa na mtu badala ya kumilikiwa na BRAND.

BRAND ni kama pumzi katika biashara ukiziba pua itatokea mdomoni,kutotengeneza brand ya biashara yako vizuri itajitengeneza yenyewe vibaya na hivyo kusababisha biashara yako kudumaa na kujiendesha vibaya,kama nilivyosema awali “ni sawa na mtu kuziba pua na kupumulia mdomo”.mambo ni mengi sana yakuelimishana kwenye hili eneo kama unahitaji zaidi kusaidiwa au ushauri wa namna ya kukuza BRAND yako ya kibiashara kwa namna zote yani “TRADITIONAL BRANDINGI NA DIGITAL BRANDING”.
 
bado uja nyoosha maelekezo.. Em rudi tena u kaulize vizuri ulipo jifunza somo la BRAND.
 
Kanye west na 'yeezy'

Michael jordan na 'air jordan - nike'

Dr dre na 'beats' aliyoiuza
 
Jamaa kaandika jambo analolifahamu kuhusu branding na brand

Lakini wadau mnakuja ku comment bado hujui kuhusu branding na brand

Nadhani ulikuwa muda sahihi wa kuweka maelezo zaidi kuhusu swala hilo

Na si kukosoa tu
Sahihi mkuu, mtu kaeleza vile anaelewa, ilitakiwa mtu kukanusha kwa kukosoa na kumrekebisha kwa kutoa ufafanuzi ulionyooka.
 
Wa tz bhana mnasema hiyo si brand,lkn hamsemi brand ni nini!!, Hii nini maana yake, maana yake tumuamini aliyeleta uzi huu,sasa tufanyeje si tusiojua kabisaa!!,
Ni sawa na we kumshitaki mtu mahala,kwa kukuibia simu,lkn ukakosa ushahidi ili watu kama ni kweli kakuibia??,sasa kama huna ushahidi si ataachiwa huru?na utaonekana huna maana weye,ati unaishia tu kusema fulani kaniibia
 
Mi nampongeza mleta mada,maana ameleta kitu ambacho wajuaji wameshindwa kukileta ila mapingamizi yasio na maelezo yaliyonyioka,
Jamaa ameeleza vizuri sana ,nadhani alimaanisha biashara inatakiwa ijulikane kwa jina la biashara na si la muuzaji, hata kama muuzaji akiondoka biashara inabaki na utambulisho wake ule ule
 
Back
Top Bottom