Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Wanaume nimeita kikao cha dharura usiku huu Kwa sababu kuna udharura wa kufanya hivyo.
Leo mchana wakati napitia baadhi ya nyuzi humu JF, kuna mwamba mmoja yamemkuta na hivi ninavyoongea huenda akaacha makazi yake kwenda mbali na mji wake, na hii baada ya kufuma message ya mkewe akipanga mipango ya kunyanduana na class mate wake.
Sasa kwa mujibu wa mtoa taarifa ni kwamba mume alimtaka mkewe aondoke lakini mke kasema nipige lakini hapa kuondoka siondoki, kwa maana haendi kwao kama mume alivyotaka. So badala yake mume anataka kuondoka yeye na kwenda mbali na makazi yake.
Nikaona hapana haya mambo hayawezi kupita hivi hivi bila kuitisha kikao cha dharura na kupeana mawili matatu ili mambo kama haya yasimtomkee mwanaume mwingine.
Sasa machief ni hivi kama unahisi au unajua kabisa unampenda your baby mama na huwezi kumwacha au unajua kabisa ukijua mambo yake ya siri utaumia na kukosa amani mpaka kuamua kuacha mji wako na kusepa, basi nashauri hivi usimchunguze tafadhali kwa maana usifuatilie mawasiliano yake kujua anawasiliana na nani na mambo kama hayo.
Sijui kama wajumbe mmenielewa? Narudia tena usimchunguze kabisa, hii itakusaidia kuwa na amani na kufurahia ndoa yako, haya mambo ya kucheki message na kukagua kagua simu sio mazuri kwa afya yako kama mwanaume.
Ndio matokeo yake utoe kichapo na kumdhuru mtu na mwishowe uende ukaishi kwenye majumba ya serikali bila kutarajia, ndio namaanisha selo au gerezani.
Kwahiyo tuachane na haya mambo ya kuchunguza chunguza kama kweli tunataka kuishi kwa amani, au chunguza wakati unajua kabisa una moyo mgumu kwa maana umekuta mambo ya ovyo basi uwe jasiri kusepa kwa amani bila kudhuru mtu na kufungua kurasa mpya katika maisha yako.
Haya yanawezekana kabisa maana msiseme Mwenyekiti wa kikao anasema tu kwa mdomo lakini vitendo hamna, haya mimi niliyaishi katika ndoa yangu kabla sijasitisha mkataba, niliyaiishi kwa miaka saba na sikushighulishwa na simu ya mke wangu hata kidogo, na nilikuwa na amani tu.
Na hata nikiingia mkataba mwingine wa ndoa sera yangu ndio hio hio kwani nimeona ina faida zaidi kimwili na kiakili pia.
Na kuna watu wanayaishi haya maisha mpaka Leo na tabasamu linatawala ndani ingawa huenda kuna makando kando huko nje lakini hawajatafuta sababu za kuleta mitafuruku ndani ya ndoa.
Ndio maana wazee wetu huko nyuma walikuwa na utaratibu mmoja,si unajua zamani kulikuwa hakuna simu, basi akirudi katika mji wake, atamtuma mtoto apeleke koti nyumbani ili kusafisha njia hata kama bi mkubwa alikuwa anafanya rafu basi ajiweke sawa na Mzee akirudi asikute baya lolote ili furaha itawale ndani ya nyumba, na walikuwa wanarudi safari mchana sababu waliogopa usiku wasije kushtukiza na kukutana na mambo ambayo yangewaumiza.
Siku hizi sisi tuna simu basi ukiwa unarudi mtaarifu kabisa mamsapu kuwa kesho natia timu nyumbani ili hata kama kulikuwa na mtu anakusaidia kulinda nyumba yako basi wakati unarudi asiwepo ili uwe na amani.
Unajua kwanini walifanya yote haya ni kwasababu walijua kabisa kwa wao kutojua jambo hakuna madhara lakini wakijua lazima kuwe na madhara ya kimwili na kiakili pia, sijui mmenielewa wanaume wenzangu?
Anyways ni kikao cha dharura hivyo hakina mambo mengi, kazi kwenu kukubaliana na mimi muwe salama au mpinge mpate presha na kukimbia mji wenu.
Ni hayo tu!