Kama huyu mwalimu kaonekana katili basi walimu wa zamani wa Manyara ranch primary wangepelekwa the Hague kabisa

Kama huyu mwalimu kaonekana katili basi walimu wa zamani wa Manyara ranch primary wangepelekwa the Hague kabisa

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,234
Reaction score
3,192
Kwa wale tuliozaliwa na kukulia Arusha na Manyara lazima wengi wetu tunaijua au kuisikia shule ya msingi Manyara Ranch ilivyokuwa enzi hizo. Miaka ya 90 nikiwa mwanafunzi wa shule ya msingi hiyo shule ilikuwa kama vile shule maalum ya watoto watukutu... ikumbukwe shule ilikuwa porini makuyuni ndani ndani mbali kabisa na barabara kabla ya miaka ya karibuni kuhamishiwa karibu na barabara ya Makuyuni - Karatu. Kisago kilichokuwa kinatembezwa huko ilikuwa hatari tupu. Yaani mzazi akiona unamsumbua anakutishia kukuhamishia Manyara ranch. Rafiki yangu Fred alitolewa Naura primary iliyopo katikati ya jiji Arusha na kupelekwa Manyara akiwa darasa la 6 kwa sababu za utukutu.

Nilikuja kukutana na Fred pale Moshi technical akiwa mwanafunzi mwenye nidhamu na kipanga wa hatari. Moshi tech nako waalimu hawakuwa wakicheka na kima. Mwl Mpande akija kuwaamsha asubuhi saa 11 mchakamchaka hatumii mbinu za kidiplomasia kuwaamsha. Unashangaa kiboko kimetua mwilini na ghafla unajikuta nje ya bweni hujui hata umetokaje. Mbaya zaidi mwalimu Mpande alikuwa mtu wa mazoezi hivyo ukisema umzingue anakufua kiukweli na hakuna kitu utamfanya.

Binafsi naona huyu mwalimu kufukuzwa kazi kaonewa sana. Hakuna ukatili wowote aliofanya. Jambo limekuzwa tu. Kama ni hivi basi Mwl Mpande na wale waalimu wa Manyara ingebidi wapelekwe the Hague kabisa kwa ukatili dhidi ya binadamu maana visago vyao sio poa. Cha kushangaza Mwl Mpande ndo mwalimu ambaye hadi leo hatumsahau na kila tukikutana naye lazima tumwachie kakitu kwa kuweza kutulea vyema. Mungu mbariki Mwl Mpande.

 
Mwalimu wa kujitolea kachomwa na mwalimu mwenye ajira ili asipate hata hiyo laki ya mwisho wa mwezi, tena unakuta ni mwalimu wa kiume yupo kwenye IST yake anafanya haya.

Hapa ndo naungana na mpwayungu kua ualimu ni laana kwa Tanzania
 
Kila zama na kitabu chake,

Zamani adhabu za kunyanyua mawe kwa mikono au kushika masikio liliku ni jambo la kawaida tu,

Pia hawa watoto wa siku hizi afya zao zimekua nyoro nyoro sana,ndio maana utasikia kesi,Mwalimu kamuua mwanafunzi,
Dunia ilisha badilika na sheria pia zinabadilika.
 
Ndiyo maana mmekuwa wajinga wajinga, waoga, msiowajibika na mafisadi
 
Zama hizi za Teko nolojia, unapaswa kuwa makini unaweza kutolewa kafara kuponya mengine
 
Kama ulivyosema, zamani. Mambo yanabadilika, maisha yanabadilika. Au upon tayari kurudi kijijini, kuvaa mabanzi na kuwinda swala porini?
 
Back
Top Bottom