Kama ICC itamfungulia mashtaka Samia, tujiandae kufunga na kuzira kula kwa ajili yake hata ikibidi kufa

Kama ICC itamfungulia mashtaka Samia, tujiandae kufunga na kuzira kula kwa ajili yake hata ikibidi kufa

The Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
11,099
Reaction score
13,709
Nimesikia maadui wa taifa mashambenga, na wambea wengi wakitangaza na kusherehekea uwezekano wa mama kufungliwa mashtaka kwenye Mahakama ya Kimataifa kuhusiana na vurugu, siyo mauaji, maana waliokufa hawakufa, ndiyo maana hawakuzikwa.

Wangezikwaje wakati hakuna miili ya kuzika? Halafu, ajabu 'maadui wa taifa letu' waliohongwa na mabeberu wanadai watanzania wengi waliuawa!

Sisi siyo washenzi wala wanyama kuua ndugu zetu wakati tunapendana mbali ya kuwa kisiwa cha amani.

Hivyo, ijulikane. Kama mama atafunguliwa mashtaka jambo ambalo liko wazi, tujue anaonewa. Na akionewa, wote tumeonewa. Akishtakiwa, wote tumeshitakiwa. Akituhumiwa kuua, wote tumeua.

Naamini kwa 'anavyopendwa' siyo kupondwa, watanzania watakuwa tayari kufunga hata kususia chakula hata kufa kwa ajili yake sawa na wale waliokufa kwenye vurugu sorry maandamnao.
 
Umesahau kuwa kuna mifupa ya mijusi iliyogundulika tanzania na duniani ilikuwa ya miaka milioni zilizopita.

sasa October 29 na dunia ya leo hii internet na teknolojia unajua inatokea kizimkazi au
 
Hivi huwa hamna aibu kupoteza muda mreefu kuandika Pumba na Mashudu?

Eti Bibie
Ni kwelli. Kwa mzwazwa hata almasi ni mashudu tokana na ombwe vichwani ukiachia mbali ugonjwa na changamoto ya afya ya akili.
 
Back
Top Bottom