ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
My Take
Wanaiba sana bando Hawa
============
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeanza mwaka mpya wa fedha kwa neema kwa kuripoti faida baada ya kodi ya Sh47.3 bilioni katika robo mwaka iliyoishia Juni 2026, ikiwa ni zaidi ya mara tano ya kiwango kilichoripotiwa mwaka jana.
Faida hiyo ni kubwa ikilinganishwa na Sh8.5 bilioni iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2025 ikichochewa zaidi ukuaji wa mapato ya huduma za data na M-Pesa.
Kwa mujibu wa ripoti ya kifedha ya robo mwaka unaoishia June 30, 2026 mapato ya Vodacom Tanzania PLC yaliongezeka kwa asilimia 18.2 na kufikia Sh515.3 bilioni kutoka Sh435.9 bilioni yaliyorekodiwa katika robo iliyoishia Juni 2025.
Mapato hayo ya kampuni hiyo, yenye zaidi ya wateja milioni 28, yanaonyesha kuendelea kuimarika kwa kampuni hiyo kubwa ya mawasiliano iliyokuwa ikiripoti hasara miaka mitatu iliyopita.