Kama iliwahi kukukuta, nambie ulijinasua vipi kwenye hili balaa?!

Kama iliwahi kukukuta, nambie ulijinasua vipi kwenye hili balaa?!

rajiih

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2019
Posts
489
Reaction score
744
Wana JF mko poa tupeane pole juu ya hizi mvua zinazoendelea Nchini.

Kwa muda sasa hii hali imekua ikinitatiza huku nikibaki bila kujua hatma ya hii hali itanitoka lini na sijui hata ni nini kimenipata mpaka sasa.

Kama miezi saba {7} imepita nilikua katika PENZI strong sana, Ambalo lilidumu kwa miaka miwili na miezi hiyo niliyoitaja, Kwakua kila lenye mwanzo huwa lina mwisho basi Mahusiano yetu yalifikia tamati kwa sababu ambazo hata sijawahi kuzielewa mpaka sasa na kwa Maridhiano mzuri tulifikia kuwa kila mtu afanye mambo yake na Maisha yake kwa amani kabisa bila Ugomvi wowote ule.

Kwa upande wangu haikunipa shida sana nikiamini atakuja mwingine na maisha yatasonga kama kawaida, Lakini kwa wakati huu nilijipa break kidogo katika mahusiano na haikunipa shida sana kwa sababu akili yangu niliiandaa vyema katika maisha ya Ubachela.

Muda ukapita nikajiona sasa nmejipa muda wa kutosha yafaa nitafute Manzi tuanze MAHUSIANO mapya.

KISANGA KINAANZIA HAPA

Ajabu kila Manzi ninaetokea kumkubali ananipa jibu la moja sawa na niliyemkosa mwanzo huku sababu zikiwa zilezile.

'MHHM! YANII MTU KAMA WEWE UWE SINGLE UNATAKA KUNICHEZEA KISHA UNIACHE TU MTU KAMA WEWE HUWEZI KUKOSA MTU KABISA'

Najiuliza yani mtu kama mimi 'Mimi ni nani hasa na naonekana vipi mbele yao sipati jibu'

wakuu hili jibu limefanya mpka sasa naenda Mwezi wa saba huu bila Manzi na hata kama nikisema nikomae nae kuonyesha kweli kuwa niko single hapo ndo sina changu hakuna kitakachoenda kubadalika baada ya majibu hayo.
 
'MHHM! YANII MTU KAMA WEWE UWE SINGLE UNATAKA KUNICHEZEA KISHA UNIACHE TU MTU KAMA WEWE HUWEZI KUKOSA MTU KABISA.
Hawa wote waliokupa jibu la aina hii ukweli ni kuwa wamesha kuelewa in directly way ila kwa sababu wewe mwenyewe bado kuna clues ndogo ndogo haujazi master basi pambana.

Nyie ndo wale wa kuambiwa kusoma hujui na picha huoni..!!!! 🤒,

Ukiwa unaongea na mwanamke jaribu kuwa unaweka umakini kwenye macho yake,, kuna kitu Utakigundua na itakurahishia sana kuweza kugundua jibu atakalo litoa hata kabla hajaongea chochote.
 
As apo unataka jibu Gani tena mzee mbona unakua na kichwa kigumu jiongeze kijana ukiweza kujinasau kweny uo mtego wa hilo swali kazi inakua imeisha oya pombe sio sigara
 
Kuambiwa ukweli unalalama, kwa mafano apo tukakagua simu yako utakuwa na charting ya mtu mmoja tu ama na wale mloachana bado umewahifadhi kwa simuu ?
 
Back
Top Bottom