MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 1,970
- 4,037
Tumeshuhudia timu kubwa barani Afrika kama Al ahly, Wydad AC nk. zikiwatoza faini wachezaji wake na wengine kunyimwa mishahara pindi wanapofanya vibaya hususan katika michezo ambayo ilikuwa ndani ya uwezo wao. Mfano baada ya CR Belouizdad kupoteza kwa mabao 4 - 0 dhidi ya Yanga, wachezaji wote na benchi la ufundi waliadhibiwa kwa kunyimwa mishahara ya mwezi mmoja, huku wakiendelea kuchunguzwa.
Hii itaongeza ari na uwajibikaji katika timu hususan ya Taifa ambapo wachezaji wamekuwa wakicheza bila morale wala motisha kulinganisha na wanapokuwa katika vilabu vyao.