RockCarnegie
JF-Expert Member
- Jan 17, 2019
- 963
- 1,927
Kuanzia Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli, mwenezi Polepole na makada wengine ni kama vile wamepigwa ganzi!
Maendeleo waliyohubiri kuyafanya kwa miaka mitano yameyeyuka mithili ya theluji kwenye joto la jua!
Stigler's, flyover, ndege na SGR zimewekwa kwenye mizani ya uhalisia wa maendeleo ya watu na nguli wa siasa nchini Tanzania ndugu Tundu Lissu, zimeonekana kupungua kwa kiwango cha kutisha! Kwa sasa jahazi hili lilikuwa turufu ya kuivusha CCM ya Magufuli limepigwa na tsunami, linayumba na karibia linazama!
Mwenyekiti na wanachama wa CCM wanalia, 'mabeberu' 'mabeberu', 'wasaliti' 'wasaliti' 'wametumwa 'wametumwa'! Hawana hoja tena ya kutetea waliyojimwambafai nayo kwa miaka mitano mfululizo!
Juma moja la Tundu Lissu jukwaani tayari wamesharusha mawe huko jimbo la Hai, huku matukio ya Arusha na Ruangwa yakithibitisha kwa CCM ya Magufuli inataka kuwaaga Watanzania kwa kuvuruga amani wanayoihubiri kila uchwao!
Je wasanii 200 na nyimbo 500 za kusifu na kuabudu ni safina mpya ya wanaCCM itakayowaokoa na siku 60 ya kimbunga cha kampeni kutoka vijana wa CHADEMA wakiongozwa kamanda Tundu Lissu?
Heri mimi sijasema, tusubiri tuone!