Kama JWTZ halitowaomba Radhi Raia wasio na Hatia WALIOTESWA KINYAMA na MP wa Lugalo Juzi, nawashauri walishtaki Jeshi

Kama JWTZ halitowaomba Radhi Raia wasio na Hatia WALIOTESWA KINYAMA na MP wa Lugalo Juzi, nawashauri walishtaki Jeshi

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
GENTAMYCINE sijapendezwa na Kitendo cha Raia Kato kujichukulia Sheria mkononi na Kumchoma Kisu Afande Lt. Col. Muna na ninalikemea sana.

Ila GENTAMYCINE sijapendezwa na Foolish Approach ya Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ya kuamua Kuvamia hovyo Nyumba za Watu, Kuvunja Milango yao, Kupiga hovyo Watu na hasa hasa Kuwajeruhi vibaya sana Wamama ( tena Watu wazima ) ambao wengi Wao hadi Usiku huu GENTAMYCINE naandika huu Uzi Wanauguza Majeraha yao huku Mmoja wapo alikamatwa na MP hao akiwa Dukani Kwake na kuamrishwa Kuingia Garini huku akiliacha Duka likiwa wazi ambapo Wahuni waliingia na Kuiba Pesa zote za Hesabu na Simu zilizokuweko ndani.

Nijuavyo GENTAMYCINE ni kwamba JWTZ wana Kitengo chao cha Mawasiliano, Mahusiano na Elimu kwa Umma ( Kurugenzi ya Habari na Mawasiliano ) hivyo Kiungwana tu wangejitokeza na Kukiri Mateso haya kufanyika kwa Raia wasio na Hatia na kuomba Radhi ila wamechagua Kunyamaza na pengine hata Kufurahia kilichofanyika

Kuna Taarifa ambazo si nzuri nimezipata Jioni hii ( japo naendelea Kuzithibitisha ) kuwa kuna Wanawake Wawili waliokamatwa Baa ya Igole au ya Bombardier nao Kujumuishwa katika Kundi la Watu 74 Waliokamatwa na kupelekwa Kambini Mwenge kupewa Adhabu Kali za Kijeshi zilizojumuisha Kuchapwa na Virungu na Fimbo Ngumu Migongoni, wakirukishwa Vichurachura, wakibebeshwa Mawe na Kubiringitwa Udongoni Wamekufa ( Wamefariki ) leo.

Na kwa leo Mchana, Alasiri na hata Jioni hii GENTAMYCINE nimeshuhudia Raia kadhaa ( tena Wababa na Wamama ) Watu wazima bila kuwasahau Mabinti wakiwa Wamevimba Miguu, Macho, Ugoko na Pua zao na Wakilalamika sana na Kuhoji Kosa lao hasa hadi Kuteswa na Kupigwa kote kule Juzi Usiku kulikuwa ni nini?

GENTAMYCINE niliamua kwenda mbali zaidi kufanya Mahojiano na baadhi ya Wanasheria ( Mawakili ) juu ya Kilichofanyika na kudai kuwa kilikuwa ni Kinyume na Utaratibu wa Sheria za nchi na kwamba Wahusika wakiungana na kwenda Kushtaki hali itakuwa mbaya Kwao ( JWTZ ) hata kama wale MP wa Lugalo WALIOWATESA KINYAMA RAIA kwa kujua kuwa walichokuwa wanakifanya kilikuwa ni kibaya walivalia Kininja ili kuficha Nyuso zao Wasijulikane.

JWTZ nawapenda ila hapa mmebugi.
 
GENTAMYCINE sijapendezwa na Kitendo cha Raia Kato kujichukulia Sheria mkononi na Kumchoma Kisu Afande Lt. Col. Muna na ninalikemea sana.

Ila GENTAMYCINE sijapendezwa na Foolish Approach ya Wanajeshi ( hasa MP wa Lugalo ) ya kuamua Kuvamia hovyo
Sio kwamba hawaoni

Sio kwamba hawajui kwamba wamefanya makosa

Sio kwamba wahusika hawajaguswa na hili

Sio kwamba hawawezi kusema

La

Ila kwakuwa washajiona wao miungu watu basi watapotezea

Ukitaka walisemee itokee hivi

Jamii Forums wachapishe taarifa hii katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram na twitter juu ya unyanyasaji wao

Trust me lazima watasema Tu

Vinginevyo tuendelee kupaza sauti pengine Mungu atawaadhibu kama anavyo muadhibu kanali huko sakafuni

Tanzania kuna uoga ila Amani tunadanganywa

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Watu wanaogopa hata kuja mazoezini uwanjani !! kama jana na leo viwanja vilikua na watu kidogo sana !!!
Wajeda acheni kujitutumua mtakua mnaumia kwa sababu hamtaki kuamini kama mnaishi na raia maana mmepanga nyumba hizi hizi za uswahilini huenda wasikuue kwa kisu , ila ukarogwa au mwanao akafanyiwa vibaya au ukawekewa sumu maana hatuwezi jua huko kwenye kubeba beba raia huenda walikunotice wakukuwekea visasi !

Mkipanda magari ya umma lipeni nauli ndo maana unapewa
mshahara fanya transaction ili tupate mzunguko wa pesa kodi zilipwe hizo hizo ndo zinakurudia kwa njia ya mshahara na hilo gari halitumii maji !! Pang'ang'a

Ukiomba kitu ukanyimwa au ukakataliwa / kuzuiliwa kupewa huduma fulani usikimbilie kujinasibu kwamba wewe mjeda ! fuata utaratibu uelezwe kwanini hujasaidiwa ! kama umeonewa unajua sehemu ya kulalamika nenda !! na Bank muwe mnapanga msitari kama watu wengine eti likija kulipa ada za watoto linapitiliza hadi mbele na hizo laki mbili huenda mlipewa hiyo priority kwa kutambua umuhimu wenu lakini sasa hamjitambui !! wanaume wako Gaza huko Ukraine sauti ya risasi ndo muziki mtamu maskioni kwao!! Wewe uko MayFair Bar unapiga wanaokukatalia maombi yako badala ufe vitani tukupe nishani unafia Bar !! Hii ni kuonesha hamna kazi za kufanya zaidi ya kwenda lindo nako mnaenda na vigodoro vya kulalia.

Hawa watu kadri wanavyoumia au kuwapoteza wenzao watawekana kitchen party wenyewe kwa wenyewe wafundane huko huko ! Nidhamu ya kupokea order wanayo !! ila sasa ushamba wa vazi dadeki !! yaan huko uswahilini wakipishana zamu za usafi chooni anaanza kujiongelesha mambo ya jeshi !! umeme wakipandisha bei au zamu yake ikafika hayuko vizuri anaanza kuvimba 🤣🤣

Kaeni kwenye hizo nyumba za kambi na chakula na vinjwaji kunyweni huko officer's mess !! mpaka mjifunze kubehave kama binadamu wa Karne ya 21 .

Mkuu GENTAMYCINE nasikia hapa kawe waliwahi kumuua kijana mdogo tu kwa ajili ya haya haya mambo ya kutoa adhabu !! ikaleta vurugu mtaani !!!
 
Watu wanaogopa hata kuja mazoezini uwanjani !! kama jana na leo viwanja vilikua na watu kidogo sana !!!
Wajeda acheni kujitutumua mtakua mnaumia kwa sababu hamtaki kuamini kama mnaishi na raia maana mmepanga nyumba hizi hizi za uswahilini huenda wasikuue kwa kisu , ila ukarogwa au mwanao akafanyiwa vibaya au ukawekewa sumu maana hatuwezi jua huko kwenye kubeba beba raia huenda walikunotice wakukuwekea visasi ! mkipanda magari ya umma lipeni nauli ndo maana unapewa
mshahara fanya transaction ili tupate mzunguko wa pesa kodi zilipwe hizo hizo ndo zinakurudia kwa njia ya mshahara na hilo gari halitumii maji !! Pang'ang'a
Ukiomba kitu ukanyimwa au ukakataliwa / kuzuiliwa kupewa huduma fulani usikimbilie kujinasibu kwamba wewe mjeda ! fuata utaratibu uelezwe kwanini hujasaidiwa ! kama umeonewa unajua sehemu ya kulalamika nenda !! na Bank muwe mnapanga msitari kama watu wengine eti likija kulipa ada za watoto linapitiliza hadi mbele na hizo laki mbili huenda mlipewa hiyo priority kwa kutambua umuhimu wenu lakini sasa hamjitambui !! wanaume wako Gaza huko Ukraine sauti ya risasi ndo muziki mtamu maskioni kwao!! Wewe uko MayFair Bar unapiga wanaokukatalia maombi yako badala ufe vitani tukupe nishani unafia Bar !! Hii ni kuonesha hamna kazi za kufanya zaidi ya kwenda lindo nako mnaenda na vigodoro vya kulalia.

Hawa watu kadri wanavyoumia au kuwapoteza wenzao watawekana kitchen party wenyewe kwa wenyewe wafundane huko huko ! Nidhamu ya kupokea order wanayo !! ila sasa ushamba wa vazi dadeki !! yaan huko uswahilini wakipishana zamu za usafi chooni anaanza kujiongelesha mambo ya jeshi !! umeme wakipandisha bei au zamu yake ikafika hayuko vizuri anaanza kuvimba [emoji1787][emoji1787]

Kaeni kwenye hizo nyumba za kambi na chakula na vinjwaji kunyweni huko officer's mess !! mpaka mjifunze kubehave kama binadamu wa Karne ya 21 .

Mkuu GENTAMYCINE nasikia hapa kawe waliwahi kumuua kijana mdogo tu kwa ajili ya haya haya mambo ya kutoa adhabu !! ikaleta vurugu mtaani !!!
Uandishi uliotukuka
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
 
Wakati mwingine hao wajeshi waishi pekee yao. Mwalimu Nyerere alipowawekea baa zao na maduka yao alijua.

Hao wakikosa vita wanapagawa wanaweza kupiga hata ukuta.

Hao wahanga kama wapo watani zangu waende mahakamani nawajua watauza hata nyumba ili walipwe fidia ya kupigwa.

Na wewe paparazi ole wako wakushtukie utatembezwa bila nguo kambini hata mtaani kwako.
 
Binafsi sijafurahishwa na vitendo vinavyofanywa na wanajeshi hasa kwa raia.

Jeshi la polisi liliwekwa kwa ajili ya kuingiliana na raia na wao ndio wanaohusika na raia direct.
Kitendo cha jwtz kwenda kuingilia uhuru wa raia ni uvunjifu wa sheria hasa kukiuka haki za binadamu.

Jwtz(MPs) msijikute nyinyi ni waungu watu na huo upolisi wenu ni wa huko makambini kwenu na sio uraiani.

Hakuna vita mbaya sana kati ya raia na wanajeshi.

Na siku ikitokea kwa hapa Tanzania basi naamini wanajeshi watakufa wengi sana.

Mnaleta ukontawa kwa raia wakati mkiwa makambini mnakuwa wasafisha vyoo na vijakazi wa jeshini.

Acheni ufala.

Ubabe sio dili.
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Daktari na mwalimu nao wakifanya uhuni sababu ya mazingira magumu ya kazi itakuwaje?
Kazi ya jeshi waliomba na wanalipwa hawajitolei.
 
Kibano kitaendelea hadi jasho liwatoke hakuna atakayewatetea awe wa ndani au nje ili siku nyingine mjifunze.Hata watoto au familia zao hamuwezi kuwafanya lolote.Jifunzeni kuheshimu majeshi yetu, mnanyonyana korodani sababu ya wao kujitoa mhanga usiku na mchana laiti mngejua mazingira wanayofanyia kazi na hawana pahala pa kulalamikia.Next time mjifunze na kuwa na adabu, hiyo ni trailer msiombe picha ianze
Mikwara mwitu hii Mzee.
 
Back
Top Bottom