Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
View: https://www.youtube.com/watch?v=VSeLKOuuolI&t=729s
Ukimsikiliza vizuri na kwa utuo imla wa Rwanda, Paul Kagame anavyoongea kwa kujiamini huku akipiga vijembe kuwa wanaomtisha ni maputo yanayoweza kutobolewa kwa sindano, unashangaa anapata wapi jeuri au ni usahaulifu wa binadamu.
Madaraka kupita kiasi hulevya kupita kiasi walisema wahenga. Wanaompenda Kagame wamuonye asichokoze simba waliolala. Ukiangalia anaowapia vijembe yaani Tanzania na Afrika ya Kusini, unashangaa nini kimempata.
Je ni mwanzo wa mwisho wa Kagame? Je Kagame aliyeishi kwa upanga anakaribia kufa kwa upanga? Ni mpumbavu gani anaweza kuilinganisha Tanzania kivita hata kama inaongozwa na mama? Je mwanzo wa mwisho wa Kagame umefika au ni mwisho wa mwanzo wa Kagame?