Matendo 20:34-35 BHND
Mnajua nyinyi wenyewe kwamba nimefanya kazi kwa mikono yangu mwenyewe, ili kujipatia mahitaji yangu na ya wenzangu.
1 Wathesalonike 2:9 BHN
Ndugu, nyinyi mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu.
Mtume Paulo alikuwa akitengeneza mahema na kuuza ili apate pesa ya kujikimu.Hivyo angeweza kusema hivi:
1 Timotheo 6:9,10
Lakini wale ambao wameazimia kuwa matajiri huanguka kwenye majaribu, na mtego, na tamaa nyingi za kijinga zenye kudhuru ambazo hutumbukiza watu kwenye maangamizi na uharibifu. 10 Kwa maana kupenda pesa ndicho chanzo cha mambo mabaya ya kila aina, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo, wengine wamepotoshwa kutoka kwenye imani na kujichoma kila mahali kwa maumivu mengi.