Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Katiba ndio chombo pekee ambacho kinawapa wananchi mamlaka ya kujitawala. Katiba ni mali ya wananchi na sio mali ya watawala wanaowekwa na wanachi kwa njia ya kura.
Hakuna kificho kuwa tangu mwaka 1977 ilipotungwa katiba ya JMT taifa letu limepata mabadilijo makubwa. Na kadiri mabadadiliko yanapotokea ndio na hii sheria yetu mama pia inahitaji mabadiliko. Mfano ni miaka ya 1980's watanzania walihitaji haki za binadamu ziwekwe kwenye katiba yetu na zikawekwa.
Yapata miaka 44 tangu katiba ya sasa itungwe tena na kupitia kamati ya wanaCcm ishirini. Taifa letu limepata mabadiliko makubwa, hivyo hii katiba inahitaji mabadiliko makubwa sana.
Mfano kuna matukio mengi ya wananchi kupigwa, kupoteza maisha na kupata ulemavu wa kudumu wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Wananchi wanataka kuwa na haki ya kulinda uhai wao na wa ndugu zao. Wananchi wanataka wawe na na mamlaka ya kufungua kesi mahakamani ili kudai haki za ndugu zao wanaopotea bila maelezo wakiwa mikononi mwa vyombo vya dola. Maana matukio mengi yanalipotiwa lakini majibu inakuwa ni uchunguzi usio na mwisho.
Hivyo basi kama kwa sasa kikwazo ni pesa ya kuweka bunge la katiba kama lile la mwaka 2014 lililopoteza pesa za walipa kodi bila mafanikio, basi hii katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho ili ikidhi mahitaji ya wananchi na hali ya sasa ya kisiasa.