Kama kawaida ya madaktari, huwa hawapendi kuguswa

Wanasema eti hizo consultation fees zinahusika kuendesha hospitali haziingii mifukoni mwao
 
Duh nes anapata nying.yan tgs d hiz sio poa
 
Niliisha wahi pigwa sh 30000 pale hindu mwanza na kwenda kumuona Dr akasema hawana huduma hiyo ninayo itafuta...nikatoka nimekuwa wa baridi nawazia pesa yangu enzi ya magufuri pesa ilikuwa chunguuuu
 
Naona kunguni zinasagwa hapa, ngoja tuwasikilize madakatari wao wanasemaje...
Hoja alitoleta ni ya msingi, kama wanalipwa mshahara why wachukue tena consultation fee? Je wafanyakazi wengine nao wadai hiyo fee?
 
Sahihi kabisa, mimi niliwahi kuwa na mgonjwa pale MOI aise hiyo fee ni balaaaa, bora juzi Mhe Waziri amewamulika na kuwalipua live..
 
Ukihamishwa kutoka bima kwenda cash unakuwa considered kama "Private" hivyo gharama zinakuwa juu zaidi.​
Sasa huo ni mfumo wa hovyo sana... Hivi watanzania milion 60 ni wangapi hasa wenye hizo Bima? Sijui tunaelekea wapi aisee, awamu ya kwanza na pili matibabu was free.. Haya mambo ya malipo yalianza na awamu ya tatu kama sijakosea,na wengi tukadhani gharama zingekuwa affordable na huduma zingekuwa bora sana lakini very unfortunately yanayoendelea ni shidaaa..
 
Huo ndio mtindo wa kula kwa urefu wa kamba,Polisi wao walikuwa wanacheza upatu na buku mbili mbili wanazokwapua kwenye daradara,upatu unafika mpaka 100K kwa siku,Hii ikapigiwa kelele na ccm,ikapoa kidogo!!,sasa hata kada zingine ni hivyo hivyo ni kutafuta namna ya kukwapua pesa za wananchi,hari ni Tete sana kitaa,kila mtu anatafuta namna ya kuongeza mapato,na muhanga mkubwa ni mwananchi wa kawaida.
 
Kwani unataka wapate sawa wote, wakati hata wakiwa wanasoma ada zao tofauti wote, ya Dakitari ipo juu, na yeye ndo atamsikiliza patient na kumanage
Basi daktari aaachiwe hospitali yeye mwenyewe au unaonaje?
 
Na ukionekana unapiga kelele basi umeisha, unaonekana wewe mlalamishi, mjuaji sana. Wakati kumbe lengo lako zuri tuu.
Ndiyo kama humu kina vichwa vinadai daktari ndiyo kila kitu, imefikia hatua kwenye baadhi ya procedures zinazolipiwa na bima wao wanachukua 80%, hospitali inachukua 20%, wengine wanaondoka na 0%.
 
Daktari anasoma miaka 6
Muuguzi anasoma miaka 5

Mmoja unampa 10,000/=
Mwingine unampa 3,000/=

Halafu utegemee waperform sawa? Hell Noo.​
Muuguzi miaka 5.. sasa alitumwa kufeli form four au six??

ukiweka miaka ya form 5 na 6 kwa daktari unapata miaka 8.. Acha masihara kabisa
 
Usawa wa Dr aliyesoma miaka 6 na muuguzi aliyesoma wki nne Zoom college magomeni?
Umeongea point kubwa. Hawa manesi wa kiume wana wivu wa kike sana..

Ukiwa nao round hawez hata changia hoja yoyote.. Anasubiri apewe maagizo na Daktari. Bado anataka alipwe sawa.
 
Muuguzi miaka 5.. sasa alitumwa kufeli form four au six??

ukiweka miaka ya form 5 na 6 kwa daktari unapata miaka 8.. Acha masihara kabisa
Kuna mambo mengine uliza usaidiwe, nyakati zinabadilika acha kukariri.

Tofauti ya miaka ipo kwa madaktari, wauguzi, wafamasia na maabara ipo katika level ya degree na kuendelea.

Level ya diploma wote wanasoma miaka sawa (3), hawa wa diploma levelnya mshahara iko almost the same.

Level ya degree, MD wanatumia miaka 6 na waliobaki wanatumia 5, tofauti ya mwaka 1. Hawa mishahara yao imetofautiana lakini at a reasonable rate kwa sababu mbalimbali ikiwemo miaka ya kusoma.

Hapa hatukuwa tunazungumzia mishahara, tunazungumzia mambo ya posho ikiwamo hiyo consultation fee ambayo sasa inaenda kutolewa.

Na kinacholeta shida hapa ni hiyo migawanyo ambayo haiakisi uhalisia maana anayekwapua kikubwa ni mmoja huku wengine mkibaki na kiduchu...

Na kingine cha mwisho dogo, miaka ya sasa vigezo vya kusoma kozi zote za afya zinafanana. Huwezi kusoma Udaktari, Uuguzi,Ufamasia,Maabara kama hujasoma PCM,PCB,CBN. Na cut-off point zinafanana kwa kozi zote, kama zinatofautiana basi ni kwa alama 1 tuu.

Hivyo upunguze ujuaji, kubali kueleweshwa, na kaa ukijua nyakati zimeshabadilika sana.
 
Hakuna mahali nimesema wapate sawa, ila angalau kuwe na mpishano mdogo...
Angalau hospitali ichukue 50%, daktari 20%, muuguzi 15% na inayobaki wengine nao wapate.​
Kuna namna kama chuki flani hivi umeijenga kwa madaktari. Why usiombe kada nyingine(yako) waongezewe bila kuwa shutumu sana madaktari.
 
Dogo babu yako..
 
Mkuu na wenzenu wamesoma miaka 4 plus mmoja wa intern.
Hiyo difference iloyopo hapo siyo fair, ndiyo maana wanashangilia kuondolewa consultation fee huku nyie mkinuna.​
Mimi sio daktari ila kushangilia mwenzako anapokosa ulaji ni dalili za uchawi na umaskini.
 
Umeongea point kubwa. Hawa manesi wa kiume wana wivu wa kike sana..

Ukiwa nao round hawez hata changia hoja yoyote.. Anasubiri apewe maagizo na Daktari. Bado anataka alipwe sawa.
Wewe dogo nimekufundisha clinical skills nyingi sana ukiwa intern. Leo uko hapa unaipondea kada yetu😄.

Wewe ni bright gentleman, tumia akili usibebwe na upepo.

Hizo round mnazopita mnakuwa na nurses wenye certificates au diploma, nurses wenye degree hapa bongo ni wa kuhesabu sana. Hao EN kwanza scope of practice yao iko very limited.

Ni sawa sawa na round inayofanywa let say na specialists 3 then akawepo na CO mmoja, do you think ataweka inputs sawa sawa na endapo angekuwa na CO's wenzake? HAPANA.

Hivyo unavyofanya comparison, unatakiwa ufanye fair comparison..
 
Kama inakuuma na wewe ungesoma uwe daktari.. kwani shida iko wapi..

Tokea lini kazi ya consultation ikatolewa na nesi??

Muuguzi kazi yake ni ya kwenye vitendo zaidi na inafanyika kwa uzoefu daktari mpaka kutoa consultation inatakiwa mara kwa mara usome vitabu.. sijui unanielewa man na muuguzi utendaji wake wa kazi unategemea daktari amesema nin
 
Kuna namna kama chuki flani hivi umeijenga kwa madaktari. Why usiombe kada nyingine(yako) waongezewe bila kuwa shutumu sana madaktari.
Hamna mahali mtu kashutumiwa, ni ukweli mtupu.

Fanya uchunguzi wako utapata majibu
.​
 
Ni wapi au muongozo gani umeandikwa kwamba utendaji kazi wa muuguzi au mfamasia au maabara unamtegemea daktari?😄

Wewe uko pale kutimiza wajibu wako, na wengine wako pale kutekeleza wajibu wao. NO ONE HAS AUTHORITY TO COMMAND OTHERS.

Na unachofanya wewe everyone ana knowledge nacho, ni protocols tuu zimewekwa kwamba huyu afanye hiki na hiki, na yule afanye kile na kile, basi.

Na ndio maana wewe ukiandika wrong dose, kisha muuguzi akai-execute jinsi ilivyo, basi anakuwa yuko responsible yeye na sio wewe kwa sababu nyote mmesoma kile kitu na mmoja akikosea basi mwenzako anatakiwa akurekebishe.

So, usidanganye umma kwamba nyie ndio ma generali na wengine ma kuruta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…