Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Laana ni nini?
Laana ni zao la maneno ya haki yanayotamkwa katika hali ya uchungu. Yaani si kila jambo linalotamkwa kwa uchungu kwamba linaweza kuleta laana Bali ni uchungu wenye haki ndani yake.
Pia hata damu iliyomwagwa huweza kutamka maneno ya uchungu na kupelekea laana kwa mwagaji na kizazi chake.
Nini matokeo ya laana au nini dalili za laana?
Dalili za laana ni pamoja na;
(A) Ulemavu wa kudumu
(B) Magonjwa ya kudumu
(C) Kufa mapema
(D) Kuhangahika, mtu mwenye laana pia anaweza kuwa muhangahikaji sana. Hatulii
(E) Kutokufanikiwa (kufikia malengo)
(F) Kutokuzaa
(G) Kufanyiwa kitendo sawia na kile ulichokifanya kwa mtu aliyelia n.k.
Sisemi muache kazi, fanyeni hizi kazi lakini hakikisheni mnafanya kwa misingi ya Kimungu, msimwonee mtu.
Kama huwezi kufanya kwa haki ni vyema uache kabisa maana matokeo utakayopata ni makubwa kuliko ile dhuluma uliyoifanya.
1. Police, hii kazi katika kutekeleza majukumu ya kila siku lazima utasababisha machozi kwa watu wengine.
Hakuna chozi la mtu lisilotoa majibu. Tubu ili kizazi chako kisiishi katika laana.
Matokeo ya laana ni kuanzia kizazi cha 1 mpaka cha 4.
Matokeo yanaweza yakatoka naadaye huku wewe umeshakufa na kusahaulika.
2. Mkusanya mapato
Biashara za watu zimekufa, watu wengine wamefilisika kwasababu ya ukandamizi wa wakusanya mapato, wanalia vitandani mwao, watoto wanalia kwa njaa kwasababu yako wewe mkusanya mapato.
Tubu, chozi la mtu halitoki bila matokeo.
3. Askari magereza
Kuna watu hawana hatia, kuna watu wametumia mamlaka zao kuwasukumia watu magerezani. Wake zao wanalia, watoto wanalia, meza haina chakula. Haijalishi wewe unatimiza wajibu wako lakini kitendo cha wewe kumshikilia mtu asiye na hatia ni laana kwa kizazi chako.
4. Trafiki
Watu wengi wametoa machozi kwasababu yao. Kizazi chako kinalaaniwa.
5.Anayedhulumu haki ya mnyonge au mtu mwingine.
6. Mtu yeyote mwenye mamlaka anayetumia mamlaka yake kutoa machozi wengine.
Mtu huyo anapeleka laana kwa kizazi chake.