Uzi wako na mada yako umeuliza swali la maana kabisa. Majibu yanaweza kuwa mawili:
1. Mabilionea wengi kupata utajiri huo katika umri mkubwa, hapa tunaongelea 35-50 kwahiyo wengi huwa wanajikuta wapo na muda mrefu wa kuishi mpaka miaka 70-90
2. Matajiri wanapata huduma bora za afya, hali bora za maisha, lishe bora, viwango vidogo vya msongo wa mawazo, muda wa mazoezi na afya, wanafanya kazi zisizochosha mwili, wana bima za afya na rasilimali za kifedha za kutosha.
Sasa ukimlinganisha mtu huyu na kapuku lazima kapuku aage ulingo wa mapambano mapema: elimu juu ya afya hana, masaa 12 yupo kazini, hapati muda wa kupumzika vya kutosha na kufanya mazoezi, afya duni, mawazo kuhusu maisha yake na familia. Kukosa fedha kunaongeza zaidi njia za mtu kufa mapema: kukosa bima za afya, mtindo mbovu wa maisha, kulazimika kutumia miundombinu mibovu inayohatarisha maisha: ndiyo maana waganga njaa wengi wanaondoka kwa ajali za mabasi, mafuriko n.k.