Kila mtu anapofariki hata kama ni kijana mdogo kabisa kauli utakazozisikia ni "mapenzi ya mungu", "mungu amempenda zaidi" na kauli nyingine za aina hiyo, sasa kwa nini mabilionea mungu hawapendi zaidi mapema na wengi huishi muda mrefu hadi kuzeeka tofauti na masikini?
Ni nadra sana kusikia billionea kafa akiwa na umri chini ya miaka 50.
Mimi kwa kipindi kirefu sana nimekuwa na jiuliza mambo kama haya pale nilipoanza kusikia heti vifo vya watoto vimepungua kutokana na jitihada na huduma ya bure ya mama na mtoto akili yangu ikaanza kufunguka na kuanza uchuguzi
Niligundua kuna aina tatu za kifo
1:Kifo cha kujitakia
2:kifo cha kusababishiwa
3: kifo cha uzee hasa hiki ndio original
Vingine vyote vina epukika kasolo hicho
Kwa mtu asiye tukia akili vizuri akisikia kuna vifo vinavyoepukika ana shangaa
Iko hivi Mungu aliweka kanuni mbalimbali
Kanuni kuu ni kila mwenye mwili ataonja mauti lini na wakati kani hilo sio jukumu lake
Binadamu alipewa nguvu kubwa sana ya kuamua hatima yake
Hosea 4:6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako. My people are destroyed for lack of knowledge:
“
Kumbukumbu la Torati 30:15 Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, na mauti na mabaya; “
Kumbukumbu la Torati 30:19 Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana
; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; I
Sasa hapa kuna mambo mengi unatakiwa utulize akili kuelewa
1: kifo kinatokea ikiwa kanunu zimevunjwa au kanuni inachukua mkondo wake
Mwanzo 3:3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
Hapa tunaona Mungu ameweka kanuni ya kwanza kwamba ikiwa utakula matunda hayo utakufa kwa msingi huu kwamba ikiwa utavunja kanuni hii kifo kitatokea
Sasa twende pamoja
* kanuni zipo nyingi
*kanuni si lazima uvunje wewe anaweza
kuvunja mwingine wewe ukakutano na kifo
Kwa uchache kanuni mbalimbali
Hapa nachahua chache
1: kanuni ya afya unakula nini unakunywa nini
Ikiwa utavunja kanuni bora za ulaji kifo kitatokea na sababu umevunja kanuni bora ya ulaji na unywaji
Hii ni pamoja na kanuni za mapumziko,mda wa kulala nk mengi hufundiswa na watahalamu wetu
Wewe ni shahidi mnavyo pingana na docta wa mhimbili kuusu ulaji
2: kanunui ya usalama hii inajumuisha mwienendo yote ya kutenda mazingira ya kazi uangalifu sehemu mbalimbali
Kama kuvunja kanuni za upepo,moto ,maji,
Usalama sehemu za mwitu nk iwe wewe au mwingine kifo kinaweza kuyokea
Mfano yankawaida
Deleva asiyefata kanuni za usalama barabarani anaweza kusababishia wengine na yeye kifo ,
Dakitari asiye na ujuzi au kafanya makosa anaweza kusababisha kifo
Mtu usika asiye zingatia kanuni mbalimbali za kuvuka barabara anaweza kusababisha kifo
Kumbe ni mhimu katika maisha yetu kuzingatia kanuni ili kuwa ma maisha marefu
3:kanuni ya kuishi na watu wengine
Mungu vile vile anazo kanuni za namna ya kuishi na watu wengine, ukivunja kanuni hiyo unaweza kusababisha kifo kutokana na magonvi na kuamisiana ,vita na mambo mabalimbali
4:kifo kutokana na uzee mwili umechoka viungo life time ya viungo vya mwili seli nk zimefika mwisho
Nayo hii kanuni uwezi kuivuka
5: mwisho kwa leo kuvunja kaninu za kiroho kunaweza kusababisha kifo
Kumbukumbu la Torati 28:15-50