Kama kifo ni mapenzi ya Mungu kwa nini mabilionea wanaishi muda mrefu?

Kama kifo ni mapenzi ya Mungu kwa nini mabilionea wanaishi muda mrefu?

Sidhani kama hii issue imeshawahi kujadiliwa kiundani haswa kutokana na maandiko.

Mwisho wa siku tunabaki kuamini kuwa kuzaliwa na kifo ni ahadi kuwa lazma mtu utakufa lakini haijaanishwa kama mtu anaweza kuendelea kuishi endapo kama kuna vitu vinaweza kufanyika.

Mfano kuna maskini wengi sana wanafariki kwa kukosa pengine pesa ya dawa na hospital kiasi ambacho wanarudishwa nyumbani kusikiliziwa which is a soft way ya kusema. Tunasubiri afe lakini kwa issue hiyo hiyo kuna mtu anapelekwa india na anapona.

Kwa hiyo ukiangalia kwa ujuujuu unaona tu vifo vingi vinazuilika na kuepukika kama pande zote zikiwa responsible.

Japo mtihani ni kuwa viongozi wa dini wanatuambia tu kifo ni ahadi. Na hawatuambii zaidi ya hapo japo Zaburi ilitaja miaka 70-80 which is below life expectancy ya Tanzania ambayo ipo 60's Ila duniani huko hadi 100 inafika.
Naam hii inahitaji waliobobea in deep.
 
Yoda,
Kifo si mapenzi ya Mungu.
Ntakupa maandiko kama matatu hivi ambazo zinasema kifo si mapenzi ya Mungu


1- Ezekiel 33:11 Waambie, ‘“Kwa hakika kama ninavyoishi,” asema Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova, “Mimi sifurahishwi na kifo cha mwovu, bali kwamba mtu mwovu abadili njia yake na kuendelea kuishi. Geukeni, geukeni mziache njia zenu mbaya, kwa nini mfe, enyi watu wa nyumba ya Israeli?”




2- Ezekieli 18:23 Je, ninafurahia hata kidogo kifo chamtu mwovu?’ asema Bwana Mwenye EnziKuu Yehova. ‘Je, sipendelei kwambaaziache njia zake naye aendelee kuishi?’




3- 2petro 3:9 Yehova hakawii kuhusiana na ahadiyake, kama watu fulani wanavyodhani,bali ni mwenye subira kwenu kwa sababuhataki yeyote aangamizwe bali hutakawote wafikie toba.

Ntafurahi sana kuendelesha haya mazungmuzo ki privet

Asante
 
Back
Top Bottom