Kama kijana nawezaje kuishi kwenye misingi ya dini(mlokole)

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Kuna wakati unafika unatamani kuishi katika misingi ya imani lakini ujana ni kama unakwamisha.

Changomoto kubwa ni vishawishi vya uzinzi na ulevi nawazaga sana vijana waliokoka wanawezaje kushindana na dhambi ya uzinzi na ulevi tena katika mji ambao wanawake wanavaa vimini na suruali za kubana mji ambao kuna baa kila kona katika dunia ambayo TV na Social network zimejaa content za ngono.

It's not easy.
 
Hakika...Uzinzi ni maamuzi siyo Sawa na kula chakula kwamba utavunga lakini lazima baadae utakula.Inawezekana japo yahitaji jitihada
Ukimwamini Yesu, ukahudhuria mafundisho bila kukosa, ukafanya maombi na sara mara kwa mara, kiu ya kufanya mabaya inapungua na unaweza kuuamlisha mwili wako ulimi, na fikira zako hata kama kuna vishawishi.
 

Dogo usisikilize maneno ya mtaani ya watu walioshindwa.inawezekana kabisa ukaacha uzinzi ukiamua kwa dhati ya kumtegemea Mungu.Ni hiv, mpe Bwana Yesu maisha yako, badili style ya maisha yako kuanzia aina ya friends tafuta rafiki ambao ni wacha Mungu,acha kuwa idle,idle huwa ni sumu sana, jichanganye na mambo ya kanisani ukiwa idle.kama kwaya etc.Hudhuria ibada mara nyingi soma neno la Mungu mara kwa mara.

KUMBUKA: Kinachookoka ni roho,mwili utabaki na tamaa zile zile za kimwili, ila Mungu atakupa nguvu ya kuzishinda hizo tamaa za kimwili
 
baba morgan mkuu Kama umeamua kweli, una hitaji kuacha hizo dhambi, basi TAFUTA WATU WANAITWA UWATA .
mkuu
 
Mungu akubariki kwa kuleta uzi huu. kuna watu wameokoka toka wakiwa na miaka 10 na wengine 12 na wameishi bila kuzini wala kulewa. unaweza kuwahukumu kwa makosa mengine ya kibinadamu kwasababu wanadamu wote ni wadhaifu ila Mungu amewasaidia kuishi katika utakatifu na kujitakasa pale wanapokosea.

cha kufanya, Wewe mpe Yesu maisha yako, yeye atakupa uwezo wa kushinda dhambi, kwasababu kwa nguvu zako hata ungekariri Biblia yote, vifungu vikae kichwani kama ndugu zangu wasabato, hauwezi kushinda dhambi, inahitaji roho yako iokolewe kutoka kwenye utumwa wa dhambi na utakuwa huru, hautasumbuliwa na uzinzi wala ulevi wala ugomvi.

Ukiokola, Mungu huwa anakupatia Roho Mtakatifu ambaye Yesu alisema bila yeye hamuwezi kufanya chochote na atatuongoza na kututia kwenye kweli yote. huyu ndiye Roho ambaye ukiwa naye, mtu anaweza kuja kukutukana matusi yote ya nguoni mbele za watu, na wewe moyo wako usighadhibike wala usimjibu vibaya, ukamsamehe na maisha yakaendelea. huyu ndiye Roho ambaye ukikutana na incident ya uzinzi unahisi umekutana na kinyesi cha mbwa kabisa, ulevi wala dhambi yeyote unahisi kabisa moyoni kwamba hilo ni chukizo na unajisikia vibaya hata kuiwaza. utatenda dhambi pale tu utakapoiruhusu wewe mwenyewe ila Roho Mtakatifu anakuwa ameshakuelekeza hapo fanya hapo usifanye rohoni mwako kwasababu yeye ndiye anaihukumi mioyo yetu nini ufanye na nini usifanye.
 
Haina maana ukiokoka unafanyika kuwa Malaika, hivyo hata hao unaowaona na kudhani wameokoka bado wanaishi kawaida tu.... ukijitesa sana hutoboi.
 
Asante kwa huu ujumbe.
 
Huu ni ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…