Chiwa
JF-Expert Member
- Apr 17, 2008
- 4,116
- 4,979
huhitaji wakati mwingine wala haya makanisa ya Kilokole ili kuacha tabia mbovu.Kuna wakati unafika unatamani kuishi katika misingi ya imani lakini ujana ni kama unakwamisha.
Changomoto kubwa ni vishawishi vya uzinzi na ulevi nawazaga sana vijana waliokoka wanawezaje kushindana na dhambi ya uzinzi na ulevi tena katika mji ambao wanawake wanavaa vimini na suruali za kubana mji ambao kuna baa kila kona katika dunia ambayo TV na Social network zimejaa content za ngono.
It's not easy.
wako vijana wameokoka lakini wanakila tabia mbovu hukohuko ulokoleni wanawashughulikia mabinti kupita kiasi na pia ni walevi.
wako pia vijana hawajaokoka lakini ni waaminifu mno kwa MWENYEZI MUNGU wanamweshimu MUNGU kupita hata wanavyomtaja wengi tu.
kwangu ningekushauri cha kwanza jua unataka nini kwa muda gani na kwa kiasi gani na utapataje unachotaka na kama hakipatikani njia gani zitumike ili uwe na maisha halali lakini yenye furaha na sio raha na kwakufanya hivyo fikra zako asubuhi ukiamka utawaza jinsi ya kupambana na malengo yako.
sintashangaa ukakaa siku mbili ukasahau kama Mzigo umesimama au haukusimama kwakuwa si hitaji lako la awali.