Naantombe Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,253
- 15,748
Mnisamehe sana wenye imani zenu labda naenda mbali sana kulihoji hili suala.
Ni baada ya hili jambo kukithiri kwenye hizi nyakati za sasa. Kila mtu akifariki, watu huanza kupost kwenye mitandao 'RIP au Rest in Peace'
Binafsi sikumbuki kama nilishawahi kulisema hili neno kwa marehemu aliyekufa, sitaki kuhisi nipo sahihi kiasi gani, wala sitaki pia kusema wanaowaambia marehemu hivo pia wanakosea au wapo sahihi kiasi gani.
Ni suala binafsi la mtazamo wangu kwenye maisha, nahisi kwamba kama kila mtu atakufa, haina haja ya kuanza kumwambia marehemu 'Rest in Peace', kwa sababu hatujui ni nini kinafuata baada ya kifo.
Sioni tija ya kusema hayo maneno kwangu mimi, nayachukulia kama maneno fulani hivi ambayo hayajabeba maana halisi kwenye maisha.
Kwa wataalamu wa Bibilia na Koran, mnaweza kutusaidia pia reference ya vitabu vya dini vinasemaje kuhusu hili suala.