Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...


..kwa hapa Tz kila awamu mpya ya uongozi huzodoa watangulizi wake.

..Nyerere alikuwa haishi kuzodoa waingereza kwa hili na lile.

..awamu ya pili ya Mzee Mwinyi walikuwa wakizodoa utawala wa Mwalimu Nyerere.

..watu wa Mkapa walikuwa alikuwa wakizodoa utawala wa Mzee Mwinyi.

..hata awamu ya marehemu Magufuli nao walikuwa wakizodoa utawala wa Kikwete.

..hivyo basi msione ajabu kwa hiki kinachotokea ktk awamu ya Rais Samia. Jambo la msingi ni kutofautisha ukweli na uzushi/propaganda.
 
Nchi imepata hasara kubwa sana ndani ya miaka mitano ya dhalimu kuliko kipindi kingine chochote kile tangu tupate uhuru. Kaiacha kila sekta hoi bin taabani. Mwenyezi Mungu kainusuru nchi na maovu mengi sana ya kutisha.

Ndio maana walipitisha sheria za kujikinga ili wasishitakiwe yeye na pm,ndugai kwa kufanya mambo ya hovyo hvyo kama hayo.
 
Reactions: BAK
Hata miradi ikiisha itakuwa sio ya Magufuli.. itakuwa ya mama, maana yeye ndo ameimalizia. Tatizo umejaa chuki ya udini. Hapo ndo upumbafu wako unapodhihirika
Hakuna mradi wa mama samia, ndio maana anaiita miradi ya urithi.
 
uyo anamtetea Magufuli, na pia anasema turudi kwenye uchaguzi mkuu,SAMIA asigombee, asimamishwe msukuma yoyote kama Chenge, ili wasukuma washike tena hatamu, Tatizo ni uraisi wa Samia hapo,,, mwendazake alikuwa fisadi mkuu
upo kwenye mwezi?
 
Mkuu tena walikuwa hawamjui JPM kabisaaa!
Lile jengo pale la Kebby's litamsuta legacy yake, hakuwa msafi.
Alilijenga alipokuwa Waziri wa Ujenzi, pesa alipata wapi?
Na kwa biashara ipi, huyu mtetezi wa wanyonge!!
 
Sawa Baba Somoe binti Chiputa kutoka Chienjele tumekuelewa ila siku nyingine unda vifungu vidogo vidogo kwenye maandishi yako (aya)
 
Hata akivunja Katiba hakuna neno kwani nia yake ni nzuri!
Hata akiiba hakuna neno kwani nia yake ni nzuri!
Hata Watanzania wakitekwa, wakateswa na wakapotezwa hamna neno kwani nia yake ni nzuri!
Kwa unafiki na ujinga wa baadhi ya Watanzania, Magufuli, kwa vitendo hivyo ataenziwa kama malaika...!


Hii hakika ni kufuru...! Dunia nzima inatucheka!​

Kwa kiwango cha uovu wake mwendazake hata Adolph Hitler angeweza kumuonea wivu.
 
JPM mwizi tu! Hayo mema kayafanya kwa pesa ya kutoka mfukoni mwake? Hivi nyie watu mbona wajinga namna hii? Kaifanyia mema nchi wakati huo huo kaiingiza nchi kwenye mizgo ya kipumbavu kama ile ya kununua ndege zinazoendelea kulitia hasara taifa? Isitoshe asilimia kubwa ya miradi Jiwe kaikuta, halafu mnataka kudanganya watu kwamba eti inatokana na "wema wa Jiwe"
 
Kwenye sayansi ya Giza mwendabure yupo sahihi kwani alishawahi kusema hii inchi imechezewa sana na imeliwa sana napia wamecheleweshwa sana na wapinzani, lkn hajawahi kusema amekomesha kazia hiyo bali alikuwa anatupa tu habari tujue hivyo nayeye anafuata muendelezo huo ila kwa style nyingine, kimtindo mwingine na kwa namana nyingine na lawama ziwe mwiko.Ndivyo nilivyomwelewa.Natani anyway.
 
Mzee mwanakijiji utahangaika sana!

Kumtetea Magufuli kwa watu waelewa ni vigumu sana! Labda kwa watu wasiojitambua ambao walikuwa brainwashed.

Wewe mwenyewe unajua Magufuli alizuia kabisa ushuru wa vyombo vya habari. Kila aliyesema mapungudu yake alikiona cha mtema kuni! Kama alikuwa msafi na miradi yake haikuwa na kasoro,alikuwa anaficha nini?

Wacha watu waseme sasa upande mwingine wa utawala wake ambao yeye,alipokuwa hai, hakutaka ujulikane
 
Kweli mkuu, wawajibike watendaji wote.
 
Nimewasikia mahali watu kutoka kanda ya ziwa wakisema kwa kile baadhi ya watanzania na viongozi wanavyomdhalilisha hayati JPM ama hadharani, kwa uficho au kupitia mitandao ya kijamii wanawasubiria hao watu na viongozi wawafuate kutaka kupewa mtihani wa kufanya kwamba wenyewe ndio watausahihisha na kutoa maksi (itakuwa ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kwa mwanasiasa kupewa maksi zaidi ya saba (7%)

Yetu macho
 
Sawa Baba Somoe binti Chiputa kutoka Chienjele tumekuelewa ila siku nyingine unda vifungu vidogo vidogo kwenye maandishi yako (aya)

Kaandika utadhani anafoka [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Huyu sikutaka kumjibu, nimeona aandiko lake ni ujinga mtupu huyu alikuwa mpambape wa Dr slaa au huenda akawa mwenyewe, aliamuaga akili aweke tumboni na tumbo aliweke kichwani
 
Hata Magu amerithi miradi mingi tu na sasa inajulikana Ni yake wakati Ni ya JK. Mfano Ni daraja la Kigamboni na fly over
Fly over kuanzia tofali la kwanza mpaka gari zinapita ni kazi ya JPM usiwe maamuma. JPM ana rekodi ya kipekee Africa ndio maana Facebook na Instagram wanamlilia mnavyomwandama.
 
Akili huna usiniulize kwanini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…