Kama kilichoripotiwa na CAG ni Kweli, basi Magufuli alikuwa sahihi mara 3...

Ni kweli mashirika ya umma jukumu kubwa kwao ni kutoa kwa maana hayakuundwa kwa ajili ya biashara Sasa ikitokea wakavaa sura ya kibiashara mpaka kutangaza faida na kutoa gawio hapo ndipo mkanganyiko unapoanzia ukiambiwa kwa muda wote walipotangaza faida ilikuwa uongo. Mbona hatusikii JWTZ wametoa gawio!!
 
Yaani ni watu kukuza mambo, kwa waliosima uhasibu hakuna wizi wowote kwenye report ya CAG, kilichowasilishhwa ni hoja na mapungufu yanayotakiwa kufanyiwa kazi.
 
Namba gani??? Na kwa ushenzi wenu mliotuonyesha kwa miaka 6 tu sahauni kutoa Raisi Tanzania hadi ipite miaka 1000
We kajamaa utakuwa unafunuliwa Malinda hata hivyo ulisema mme wako Lissu akishindwa Urais utakuwa tayari kufunuliwa Malinda.
 

Sasa unafikiri Mwendazake kafa akiwa masikini? Jamaa alikuwa tajiri mzuri tu hata kabla hajawa Rais, kwenye ujenzi kapiga vizuri tu!
 
Lakini muelewe kuwa popote duniani serikali haijawahi kufanikiwa kufanya biashara. Hata China walianza kupata mafanikio makubwa baada ya kuruhusu sekta binafsi. Serikali ibaki kuunda mifumo imara ya kuisimamia sekta binafsi kwa umakini na kukusanya kodi stahili pamoja na kuilea sekta binafsi ili iweze kushamiri na kuleta mapato serikalini. Anachosema Ndugai kuwa treni ya mwendokasi iruhusu mabehewa ya watu binafsi yuko sahihi kwani wafanyibiashara kama Mo na Bakhresa wanaweza kuleta abehewa yao au hata vichwa vya train wakiweza na shirka la reli likaachukua ushuru kwtoka kwa hao wafanya biashara. Suala ni serikali kujipanga na kusimamaia na kuhakikisha mambo yanasimamiwa kwa ukaribu na umakini. Miaka mitano ya mwendazake imeua kabisa sekta binafsi hasa kwenye sekta ya ujenzi, hasa wazawa. Mazingira ya udanganyifu yalitokana na serikali zenyewe kuwa corrupt na hivy na wakandarasi wakawa wanadanganya ili wapate pesa za kuwahonga watu wa serikali.
Ni kweli kwamba sehemu kubwa ya walioko serikalini ni wafanyabiashara na wakati huu watakuwa wanatoa ushauri kwa Rais wakivutia upande wwenye maslahi kwao na mama anapaswa kuwa makini sana. Inashangaza leo hata Muhongo anaponda Hydropower na kushadidia gesi ambayo waliingia mikataba ya kuhuni. Tufike mahali Watanzania tusiangalie maslahi ya mmoja mmoja bali tuangalie maslahi ya nchi yetu kwa ujumla kwani maoni mengi sasa kwenye mitandao ni kila mmoja kumtaka Rais afanye analoona linamfaa yeye binafsi au na kundi lake.
 
Chadema sin mna imani kubwa na mama Samia na mnasema mtamlinda kwa wivu mkubuwa, ??? Kama kweli report ya CAG kweli imebainisha wizi basi wahusika wachukuliwe hatua vinginevyo ni kelele zenu .
 
Huko mbeleni tutakua na serikali zinazoongozwa na robots. Bora kuamini kwenye science kuliko siasa.

Lakini nilichopata kutoka kwako hapa M.M unataka tuanze upya? Je Kuna upya wowote ndani ya CCM? Huko nje ya CCM nani msafi?
 
Upinzani uko kwenye damu yangu; ila sasa hivi naona kama umepotea maana sijui ni nani amebakia upinzani kweli. Labda tuunde upya kabisa... maana upinzani umekubali jukumu lisilo lao...
Kwa nini kama hamridhiki na hali ulivyo msijiengue ccm mkaunda chama chenu?
Halafu unataja bwawa la nyerere hivi linatoa MW ngapi?
Je nani kashapanda treni ya SGR?
Unaongea vitu havipo mzee.
Kubalini tu Magu alikuwa na uungu mtu ambao uliwafanya mumuone Mungu asiye kosea ndio maana hamuamini kama alivurunda.
 
Umesema kweli! Kama ufisadi tunaoambiwa ni kweli, Basi serikali yote ilikuwa corrupt! Watajitengaje kwa mfano!! Hivi wanafikiri tutawasifu wao kuwa Safi wakati Kuna uwajibikaji wa jumla?
Lakini tuende mbele turudi nyuma Magufuli Ni mchapa kazi hakuna mfano! Aliyoyafanya tumeyaona wenyewe hatuhitaji kusimuliwa na mtu! Yeyote akitaka ku-discredit au kubeza na kudharau kazi yake atajidharaulisha tu mwenyewe! Hakuna mzalendo wa kweli atakayemwelewa! Hata dhamiri yake mwenyewe hawezi kuishawishi!
Ilikuwa Ni ngonjera tu habari ya kuhamia Dodoma Kama makao makuu ya nchi. Hakuna aliyekuwa anaamini kuwa inawezekana kuhamia dodoma! Lakini huyu tunayeambiwa sasa kuwa alikuwa "fisadi" yeye kwa "ufisadi" wake amefanikiwa kuhamisha makao makuu kwenda Dodoma! Kwangu Mimi huyo "fisadi" alitufaa Sana kwa kuwa alifanikisha ndoto ya kuhamia makao makuu!
Lakini pia hili la mradi wa Stigler's George wa kujenga bwawa la kufua umeme lilishakuwa Ni ndoto isiyotekelezeka! Hivi tunavyozungumza takribani mradi uko tayari kwa asilimia 50! Lakini ghafla tunaambiwa Hilo pia ni changa la macho! Tunaambiwa upembuzi yakinifu unaotumika Ni wa miaka ya 70!! Umepitwa na wakati!! Wasichokijua Ni kuwa si lazima upembuzi yakinifu wa miaka ya 70 uwe umepitwa na wakati! Wakati wanafanya upembuzi yakinifu wa mradi mkubwa Kama ule ni lazima walifanya projection ya muda mrefu, at least miaka 100 mbele! Kwa akili ya kawaida huwezi kufanya upembuzi yakinifu kwa mradi mkubwa vile halafu ukakadiria uhai wa mradi kuwa miaka 10 au 20! Kwa hiyo uncertainties nyingi zilikuwa taken into conciderations! Ninaamini huu mradi bado unaweza kuongozwa bila matatizo na upembuzi yakinifu wa miaka ya 70. Ila mafisadi walitaka wapige pesa kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu mwingine kwa miaka Kama miwili hivi! Environmental impact assessment (EIA) pia ilifanyika huko nyuma na hakuna matatizo. Wote mnakumbuka mabeberu walivyopiga Vita huu mradi! Hivi unafikiri Kama tungetoa tenda ya kufanya EIA nyingine, mabeberu wangefanya kila wawezalo kupenyeza ushawishi wao huko na huu mradi wangeunyongea baharini.
 
Maswali magumu😂😂😂 .Mzee yupo yupo tu hajui ashike wapi, umemuuliza maswali ya msingi sana kwenye post yabkwanza, hakuna alilojibu
 
But kumbuka Lake Zone tuna numbers

..unajidanganya.

..unadhani mnaweza kufua dafu ikiwa CCM wataamua kutangaza matokeo wanayoyataka wao?

..lake zone ilishakuwa na chama kinaitwa UDP kilianzishwa na John Cheyo lakini hakikufua dafu mbele ya CCM / chama dola.
 
MMM, sikuwahi kukupa LIKE tangu JPM alipoingia madarakani, lkn leo nimekupa LIKE baada ya miaka mingi.

Vv
 
Nimezipenda hoja zako si kwasababu ni nzito sana , bali ni kwasababu zina maswali magumu unayoyapatia majibu rahisi sana. Mwl Nyerere aliwahi kusema kwamba watanzania ni watu wa ajabu sana kwasababu wana majibu rahisi kwa maswali magumu sana. Nami nasema usemi huo ni wako muandika thread hii.

Kwa mfano unashangaa watu waliokuwa wakimuunga mkono sana Magu leo wamemgeuka na hata miradi yote iliyokuwa inatajwa ni kama haipo/haikufanywa. Umeenda mbali zaidi na kumtaja Ndugai kwa kushangaa kwanin bandari ya Baga-yo haikujengwa. Na na na............

Swali langu kwako ni moja tu, sijui mwenzetu ulikuwa wapi kati ya 2015-2020? Kwa sababu katika kipindi hicho sauti ilikuwa moja tu na kila aliyejaribu kufungua kinywa cha alikipata cha mtemakuni. Hivyo ulitaka Ndugai wakati ule aseme nini? Na hapo ndio utafahamu umuhimu wa kuwapa watu wako uhuru wa kuzungumza na kutoa mawazo yao amaye pengine ni tafauti nawe.

Hayati Magu, nilimpenda lakini doa kubwa lililoniudhi ni kuwabana wanataaluma kuzungumza wanayoyaju. Kilichompata Prof Assad si kikla mmoja anaujasiri namna hiyo, na wataalam wengine wengi tu waliosahau taaluma zao, kisa eti kuna simba mmoja tu anayojua kila kitu.

Swali langu ninalojiuliza mwenyewe ni moja tu; Hivi Hayati ukali wote ule juu ya wanataaluma (Kuzuia takwimu n.k), alikuwa anaogopa nini? Au alikuwa anaficha nini? Kama kulikuwa alichokificha, pengine ndicho kinachoanikwa hapa hadharani leo. Endelea na uchambuzi wako bila kusahau maswali hayo makuu na utupe jibu. Alamsik!
 
Mijitu mijizi, mizushi inayofikiria karibu including Mosoga
imeshangalia sana kifo cha Jemedari Shupavu JPM... Ni kushangalia ujinga na uzushi.... Utadhani macho yao yapo makalioni....mpaka kushindwa kuona aliyoyasimamia JPM while is tangible na yatakuwepo kwa miaka mia+.

Msoga huwa anajilaumu sana kwa madudu aliyofanya hili linajidhihirisha utetezi anaofanya kila platform.. ni kum-outshine mwendazake na kujifanya aliyosimamia yote zilikuwa plan zake.. Serikali ilikuwa masikini wa kutupwa ilitegemea kufadhiliwa almost kwa kila kitu... Ninahakika JPM angepewa maisha marefu tungeishuhudia nchi yetu ikimeremeta kwa infrastructure za maana zenye viwango maridhawa kama tulivyo shuhudia..

Mama yetu Samia hakuwa amejiandaa kuongoza nchi.. viatu ni vikubwa mno anaongea vijineno vya wambea na watu wasio thabiti kwenye wanacho simamia... Its to early to conclude the analysis but sioni mtu imira kama tuliye muhitaji... JPM popote alipo JPM is will remain the best president JMT ever had.
 
Hata kama walizuiliwa kuongea wanapopata nafasi sasa sio kuongea ujinga... Nampongeza sana JPM kuwaziba midomo kama ndio ujinga huu wanaoungea sasa.
 
Msiwagawe watanzania kwa sera zenu za ukabila.

Mimi niko kanda ya ziwa,mbona sijasikia hayo unayojaribu kudanganya mchana kweupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…