Kama kiongozi mkristo akiwa mtekaji, muuaji, mtesaji, fisadi, akitubu dhambi zake anasamehewa basi tuna safari ndefu sana

Wewe unajuaje anakua amesamehewa dhambi zake mkuu? Anaye samehe dhambi ni MUNGU tu. Kwa hiyo msamaha wa dhambi unabaki kuwa siri kati ya mwenye dhambi na MUNGU wake. Isipokuwa sisi tunamwongoza sara ya toba mbele za Mungu ili aweze kumsamehe. MUNGU ni mwenye REHEMA anaweza kumsamehe mtu yeyote aliye amua kugeuka na kumfuata hata kama alifanya dhambi kubwa MUNGU anamsamehe. Huyo ndio MUNGU mwenye REHEMA.
 
Mkuu,

Umeuliza swali zuri sana, nafikiri utapata majibu mazuri pia.

Falsafa ya Ukristo kwenye suala la dhambi inaeleza kuwa ni kosa unalolifanya kwa mujibu wa Mungu, yaani ni jambo ulilolofanya kinyume na amri za Mungu, na hapo uliyemkosea ni Mungu (baadhi ya hizo dhambi zinahusisha kuwakosea wanadamu pia, lakini huitwa dhambi kama imeenda kinyume na Mungu)

Unapotubu, kwa kumaanisha kabisa unakuwa umepatana na Mungu. Katika Ukristo hizo dhambi zote zinasamehewa kabisa, wala Mungu hakuhesabii hata dai moja ukitubu kweli.

Lakini, hiyo ni umepatana na Mungu, kinachofuata ni kupatana na mwanadamu mwenzio ( kama dhambi ilihusisha kumkosea mwanadamu mwenzio). Kwa hapo, Bado unawajibika kuomba msamaha kwa wanadamu, ama kulipia makosa yako kama inavyotakiwa kwa Sheria za wanadamu.

Mungu anakuwa amekusamehe, lakini unaweza kuhukumiwa kunyongwa, kifungo cha maisha ama kulipia faini kwa Sheria za jamii uliyopo. Kwa hiyo, jambazi ama fisadi akienda kanisani na kutubu, Padre ama Mchungaji atamtangazia msamaha wa Mungu kama maandiko yanavyofundisha, halafu polisi watamchukua na kumfikisha mahakamani kama Wana ushahidi, na kesi itaendelea kama kawaida.
 
Hata yule anayezalisha wanawake na kuwakimbia watoto huku akiacha wanateseka bila msaada akiomba msamaha kwa Mungu amsamehe wa, ila usichokijua ni hiki kila dhambi ina adhabu yake hapa hapa duniani hata kabla ya huo moto, kwahiyo atasamehewa ila adhabu atakumbana nayo

Daudi alifanya uzinzi na mke wa mtu, ili kuficha akatengeneza mazingira ya kifo cha mume wa yule aliyezini naye, Daudi alimsamehewa hiyo dhambi baada ya kutubu lakini msamaha haukuondo madhara yaliyosababishwa na ile dhambi, Mungu alimwambia mauti hautaondoka nyumbani mwako
 
Ni ngumu kumeza ko maana yake ukauze then urudi kwenye ufukara maana kwamba ukiwa tajiri hawez kukupokea na mbona makanisan matajiri ndo wanaopendelewa na kupewa vyeo
Makanisa ya Sasa ni biashara lakini ukweli wa yesu ndo huo hata aliyeambiwa na yesu mwenyewe hakutegemea alisononeka sana.

Soma hapa

Luka 18:21-23 (KJV) Akasema, Hayo yote nimeyashika tangu utoto wangu.
Yesu aliposikia hayo alimwambia, Umepungukiwa na neno moja bado; viuze ulivyo navyo vyote, ukawagawanyie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha, njoo unifuate.
Lakini aliposikia hayo alihuzunika sana, maana alikuwa na mali nyingi.
 
Soma tena unavyojikanyaga! Nadhani kazana na masuala ya uchimbaji mafuta mengine waachie aki na Mwakasege na Tonny wa mitungi ya gesi
 
Soma tena unavyojikanyaga! Nadhani kazana na masuala ya uchimbaji mafuta mengine waachie aki na Mwakasege na Tonny wa mitungi ya gesi
Mambo ya MUNGU niya kila mtu. Mungu alikuja kumwokoa kila mtu. Hata wewe utahubiri habari za MUNGU.
 
Mambo ya MUNGU niya kila mtu. Mungu alikuja kumwokoa kila mtu. Hata wewe utahubiri habari za MUNGU.
Kazi ya kuhubiri nawaachiamapadre, ila ninachojua ni kuwa ukiungama kwa Padre akakusamrhr, utakuwa umasamehewa dhambi zako. Mengine tuchimbe gesi
 
ACHA KUMTETA MAREHEMU!
 
Kazi ya kuhubiri nawaachiamapadre, ila ninachojua ni kuwa ukiungama kwa Padre akakusamrhr, utakuwa umasamehewa dhambi zako. Mengine tuchimbe gesi

Mathayo 28:19–20

“Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Waefeso 4:11–12 👇
“Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine manabii, na wengine wainjilisti, na wengine wachungaji na walimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…