Uko sawa lakini unapojadili kuhusu taasisi kama FBI na idara kama CID kuna tofauti kubwa sana kiutaalam na kiutendaji.
usiweke neno SANA,utofauti uko kwenye mipaka ya kazi zaidi na si kiutaalam ama uwezo,kwanza maofisa wengi wa FBI ni mapolisi hawa hawa waliokuwa humo CID,lengo ni kuifanya FBI kuwa na wataalam wenye uzoefu usio na mashaka.
so ni kama kusema FBI anaongezewa uwanja wa kazi zaidi.
FBI ni wachunguzi wa uhalifu wa kupangwa kitaalam kama ujasusi, uhalifu wa kalamu unovuka mipaka, mauaji yanovuka mipaka, uhalifu unotishia usalama wa nchi, madawa ya kulevya yanohusisha makundi makubwa, uuzaji silaha unohatarisha usalama wa nchi hayo ni "very serious crimes".
yah kama nilivyosema hapo,nia ilikuwa kuunda FBI yaani wapelelezi wa polisi yenye nafasi kubwa zaidi kufanya mambo hayo ya upelelezi,kule CID hata nje ya jimbo lake hatoki.
CID ndani ya polisi bado zipo (wenyewe Marekani ) waita LAPD ni uchunguzi wa uhalifu kama vile watu kuuana au mtu kuua, ubakaji (sexual offences), watu kupigana na kuumizana (assaults), wizi wa kuagiza (steal to order) na kesi hizo uchunguzi wake hushughulikiwa na askari kanzu (detectives).
hii LAPD ni moja wapo na majina ya polisi nyingi ndani ya marekani hii ni ya jimbo la los angeles ,haya matukio yote uliyotaja FBI wanakuwa na report zake hata kwao,lengo sana si kutoa ushahidi mahakamani,hapana.
Sasa hapo tofauti yao ni kwamba watu wa FBI ni majasusi na wenye utaalam wa hali ya juu katika kuchunguza, na kushughulikia uhalifu niloutaja hapo juu lakini wao hutumia SWAT kutekeleza kazi zao.
mkuu,swat na FBI tena🙄🙄🙄.
SWAT ni ni kitengo maalumu cha polisi kinasubiri tu ripoti kutoka eneo la tukio,zitolewe na traffic polisi,sherif ama polisi yoyote vikidhi uhitajika wao wanatimba.
CID wao ni polisi kitaaluma na mtu wa CID huweza kujiunga na FBI akiwa amejiongeza kielimu na kwa kwenda kozi katika chuo cha FBI.
FBI ni polisi kitaalam pia ndio maana wana badge na vest kabisa,ila ni polisi ambaye hajafungiwa eneo alipo tu.
Sasa sisi tuna CCP Moshi lakini hatuna chuo maalum kama cha FBI ambacho hutoa vyeti baada ya mafunzo ya hali ya juu na maofisa wake huitwa "special agents" na yuko juu ya "police detective".
huu ni uzembe tu wa serikali,haijawahi kuwa serious na jamb lolote,ktk mtaala wa polisi umeandikwa kabisa,CID ni taaluma ndani ya polisi,ina kozi yake,kitambulisho chake,malipo yake na uongozi wake pia,ila eh kazi tupu.