Kama kuna Wizara ya Mipango na Uwekezaji mbona hakuna idara inayohusika na Uwekezaji kwenye Halmashauri zetu za Wilaya, Manispaa na majiji?

Kama kuna Wizara ya Mipango na Uwekezaji mbona hakuna idara inayohusika na Uwekezaji kwenye Halmashauri zetu za Wilaya, Manispaa na majiji?

M.Rutabo

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
1,031
Reaction score
2,647
Nimekuwa nashindwa kuielewa serikali yangu kama kuna field ambayo ni muhimu kuitilia mkazo basi ni field ya uwekezaji.

Kwa kulitambua ilo ndo maana waliamua kuitenga wizara ya fedha na mipango na kutengeneza wizara mpya ya mipango na uwekezaji. Ila hajabu ukienda halmashauri, Manispaa na majiji hakuna idara yoyote inayo usiana na uwekezaji. Sasa uwa najiuliza uwekezaji unaanzia uko juu tu uku chini hakuna umuhimu wowote.

Na watu waliosoma finance and investment planning hawaajiriki halmashauri na ngazi zote za serikali za mitaa?
 
Nimekuwa nashindwa kuielewa serikali yangu kama kuna field ambayo ni muhimu kuitilia mkazo basi ni field ya uwekezaji. Kwa kulitambua ilo ndo maana waliamua kuitenga wizara ya fedha na mipango na kutengeneza wizara mpya ya mipango na uwekezaji. Ila hajabu ukienda halmashauri, Manispaa na majiji hakuna idara yoyote inayo usiana na uwekezaji. Sasa uwa najiuliza uwekezaji unaanzia uko juu tu uku chini hakuna umuhimu wowote. Na watu waliosoma finance and investment planning hawaajiriki halmashauri na ngazi zote za serikali za mitaa?
Ni swala muhimu,Ile Idara ya biashara ipewe jukumu hili pia au wale watu wa mipango
 
mbona iko idara ya mipango kwenye hizi halmashauri ambako kumejaa maafisa mipango na wachumi wengi tu!
 
Nimekuwa nashindwa kuielewa serikali yangu kama kuna field ambayo ni muhimu kuitilia mkazo basi ni field ya uwekezaji. Kwa kulitambua ilo ndo maana waliamua kuitenga wizara ya fedha na mipango na kutengeneza wizara mpya ya mipango na uwekezaji. Ila hajabu ukienda halmashauri, Manispaa na majiji hakuna idara yoyote inayo usiana na uwekezaji. Sasa uwa najiuliza uwekezaji unaanzia uko juu tu uku chini hakuna umuhimu wowote. Na watu waliosoma finance and investment planning hawaajiriki halmashauri na ngazi zote za serikali za mitaa?
Inaonekana kuna taarifa hujapata. Tangu mwaka 2022 Serikali ilianzisha Kitengo cha Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kikiwa na sehemu mbili (i) Maendeleo ya Viwanda na Uwekezaji na (ii) Biashara na Masoko.

Mpaka sasa hiki kitengo kwenye maeneo mengi hakina watumishi waliokusudiwa kwa maana wanaoratibu shughuli zote bado ni wale tu Maafisa Biashara waliokuwepo ambao walikuwa kwenye Idara ya Fedha na Biashara
Screenshot_2024-08-04-12-44-09-63_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
Screenshot_2024-08-04-12-29-45-06_f541918c7893c52dbd1ee5d319333948.jpg
 
mbona iko idara ya mipango kwenye hizi halmashauri ambako kumejaa maafisa mipango na wachumi wengi tu!
Kwasasa kuna Idara ya Mipango na Uratibu (zamani ikiitwa idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji) yenye watu wake lakini pia kuna Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji ambapo tegemeo ni itakuwa na watu wote wa uchumi, biashara, uwekezaji, mipango, n.k
 
Back
Top Bottom