GE2025 Kama kupiga kura tunahimizana hivi. Je, 2030 hali si itakua mbaya sana?

GE2025 Kama kupiga kura tunahimizana hivi. Je, 2030 hali si itakua mbaya sana?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

baz kaiza

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2015
Posts
14,971
Reaction score
18,641
Nini kimetufikisha hadi hatua ya kuhamasishana kupiga kura kwa nguvu kiasi hiki? Je, ni kwamba wananchi hawatambui wajibu wao, au wamepoteza imani na mchakato wa upigaji kura? Hili ni swali linalohitaji tafakari ya kina.

Tunahitaji kurudi nyuma na kuangalia tulipojikwaa ili tuweze kujisahihisha. Ukiangalia kwa jicho la mbali, mwaka 2030 unaweza kuwa na changamoto kubwa. Watu wengi huenda wasijitokeze kabisa kupiga kura. Hata hao wanaotarajiwa kujitokeza Oktoba 29, kuna uwezekano mkubwa idadi yao ikapungua zaidi miaka ijayo.

Ni wakati wa watawala kukaa mezani na kujitafakari kwa umakini. Dunia haiwezi kusimama ikikusubiri. Ukishindwa kwenda nayo sambamba, unabaki nyuma. Tuache propaganda za kizamani. Ni muhimu watawala kubadilika na kuwa wa kisasa zaidi. Uongo na mbinu za zamani haziwezi kufanya kazi katika karne hii yenye teknolojia na idadi kubwa ya watu.

Tukumbuke, katiba ya kipindi cha Nyerere iliandaliwa wakati Tanzania ilikuwa na watu takribani milioni 12. Leo hii, idadi ya watu imefika zaidi ya milioni 65. Haiwezekani kuendelea kutumia mbinu na fikra za wakati huo kwenye mazingira ya sasa.

Bado tuna nafasi ya kujenga. Ni bora tukakaa mezani kwa pamoja, tukalinda tulichonacho na kukiendeleza, kuliko kusubiri kupoteza hata kile kidogo kilichosalia. Taifa likubali kujenga kwa umoja. Hoja zisikandamizwe kwa rungu. Wananchi wakipoteza imani na sanduku la kura, hali itakuwa hatari.

Tuchukue hatua mapema. Muda bado upo.
 
Watawala wameona huenda mwaka huu kukawa na mwitikio mdogo sana tofauti na vipindi vya nyuma. Na ikitokea hivyo itakuwa ni fedhea kwao na hautakuwa uhalali. Ndiyo maana kuna kiongozi mmoja wa kiti cha Urais alisikika akisema tujitokeze kwa wingi kupiga kura tuwaaibishe na akaenda mbali akisisitiza hata wagonjwa waliopo hospitalini kutakuwa na utaratibu wa kuwachukuwa wakapige kura kisha kuwarudisha.​
 
Nini kimetokea mpaka kupiga kura tunaimizana hivi? Wananchi ni kwamba hawatambui uwajibu wao au wameona kupiga kura hakuna maana tena? Tunaitaji kurudi nyuma na kuangalia tumejikwaa wapi tuweze kujisahihisha,Kama una jicho la kuona mbali 2030 na ali inaweza kua mbaya sana watu wasijitokeze kabisa hata hawa watakao jitokeze October 29 kupiga kura inawezakana kabisa 2030 wasijitokeze kabisa au wapungue. Ni nini kifanyike ni mda wa Watawala kukaa mezani na kujitafakari Dunia haitagoma kutembea ukishidwa kutembea nayo tuache Propaganda za zamani tu jipange watawala tuwe wa kisasa zaidi Uongo wa zamani huwezi kuutumia karne hii Tenochogyia population hivi vitu lazima vitakuja kuangusha watawala ni kama wanajisahau kwamba katiba ya kipindi cha Nyerere Tanzania nzima ina population ya watu Milio 12 huwezi kutumia sasa kipindi ambacho population ina watu milion 65 plus Tenochogyia bado tuna nafasi ya Kujenga ni bora watawala tukae mezani tulinde tulicho nacho kabisa kuliko kuja kukipoteza hata kidogo tulicho nacho Taifa tukubali kulijenga kwa pamojau hoja isipigwe Rungu.
Kimsingi uchaguzi wa 2025, ni sawa sawa na wa 2030 kwa kuwa hii ni scramble for 2030.
Same people now same people then
 
Maajabu ya kwanza kutokea na ni Tanzania tu hadi polisi wanahamasisha watu wakapige kura.

Wakati huo huo tumeambiwa kuna tume "huru" ambayo imeweka sheria hakuna mahakama ya kuingilia mambo yake sasa polisi na video za waliolipwa mitaani na wao kuhamasisha watu wakapige kura zina tija gani.?

Jukumu la polisi ni kulinda watu na mali zao ambalo hadi sasa limewashinda , ripoti ya haki za binadamu imeonyesha watu 200 wamepotea na wengine kutekwa na ni mmoja tu alifanikiwa kurudi salama akataja watekaji wake ila hakuna hatua yoyote imechukuliwa.
 
Watawala wameona huenda mwaka huu kukawa na mwitikio mdogo sana tofauti na vipindi vya nyuma. Na ikitokea hivyo itakuwa ni fedhea kwao na hautakuwa uhalali. Ndiyo maana kuna kiongozi mmoja wa kiti cha Urais alisikika akisema tujitokeze kwa wingi kupiga kura tuwaaibishe na akaenda mbali akisisitiza hata wagonjwa waliopo hospitalini kutakuwa na utaratibu wa kuwachukuwa wakapige kura kisha kuwarudisha.​
Hana akili amuaibishe nani sasa anayechuana naye??
Mpinzani kiboko yake si kamuwekea kesi ya mchongo.
 
Upigaji kura umebaki mitandaoni tu. Wananchi hawana habari na uchaguzi wa mwaka huu
watawala wanaweza kumeza pini lakini Ogopa sana watu wakikosa Imani na box la kura hatari sana hii sijui wanachuliaje ili jambo sisi huwa tunasema kama wana CCM tunaoangalia taifa kwanza
 
Maelekezo Maalum kuhusu tarehe 29 Oktoba.

Siku hiyo kazi ni rahisi sana

Viongozi wa CCM tunaishi nao mitaani; Nyumba zao zipo mitaani kwetu, mali zao zipo mitaani kwetu.

Ofisi za CCM zipo mitaani kwetu. Ofisi za Umma nazo zipo mitaani kwetu

VItuo vya kupigia kura vipo mitaani kwetu

Mawaziri, Wabunge na Madiwani tunaishi nao mitaani kwetu, familia zao na ndugu zao tunaishi nao mitaani kwetu. Machawa na mali zao tunaishi nao mitaani kwetu.

Ndugu watanzania, mafuta ya taa, petroli na viberiti havijawahi kuwa adimu.

Tukafanye kazi iliyotukuka hiyo Oktoba 29 hadi hawa Mafisadi watuheshimu na wakome kutuchezea na kutuua.

Share na mwenzako
 
Sasa kwani huyo jiwe alikuwa rais? Tanzania haina rais tangu 2015.
Kwaiyo kikwete ndie alikuwa rais? Hivi tofauti ya kikwete na Samia ktk uongozi wao ni kipi tofauti na jinsia?

Magu hawakumpenda wezi na baadhi ya wapinzani waliopelekwa na upepo wa kufuata mkumbo.
 
Back
Top Bottom