Jibu ni NDIYO, INAWEZEKANA.
Kuzini au kutamani kuzini ni dhambi, lakini kuwa na dhambi sio kigezo cha kutokwenda mbinguni. Kwa maana hiyo wapo wenye dhambi ambao wapo au watakwenda mbinguni.
Tazama hapa: Yahane 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Kwa hiyo neno hilo linatuonyesha kwamba suala la kwenda mbinguni kwa Mungu lipo
Pia tazama hii hapa: Warumi 3:23-25
23 kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu;
24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu;
25 ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho
Neno hili linatuonyesha kuwa hakuna mwanadamu asiye mkosefu
Kwa hiyo tukilisoma kwa pamoja neno la Mungu, tutaona kuwa licha ya kuwa na dhambi, lakini wapo wateule wa Mungu watakaokwenda kukaa katika ufalme wake