Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kuwa na Ofisi ni sehemu ya utambulisho wa mahali taasisi fulani inapatikana. Lakini kuwa na Ofisi hakuhusiani na uimara wa taasisi husika. Makampuni yanayofilisika au taasisi zinazoshindwa kujiendesha na hatimaye kufungwa, nazo pia huwa na Ofisi.
Wakati Serikali ilipoamua kuyaunganisha mashirika ya hifadhi ya jamii ili kuleta ufanisi, mashirika hayo yalikuwa na Ofisi lakini yalifikia kwenye hatua ya kufilisika. Kwa ivo mbali ya Ofisi kuwa utambulisho wa Taasisi na sehemu ya kuhifadhia nyaraka mbali mbali za Taasisi husika, Ofisi kama ofisi haina mchango wowote ule kwenye kuifanya Taasisi kuwa Imara.
CHADEMA kwa sasa, inafanya harakati za kujenga ofisi zake nchi nzima. Na ofisi hizo zinajengwa kama hitaji la CHADEMA kuwa na sehemu itakayotumika kwa utambulisho na uhifadhi wa nyaraka zake. CHADEMA haijengi Ofisi ili kujiimarisha, bali inajenga ofisi kama kituo cha kukutania kupanga mipango ya chama.
Nguvu iliyonayo CHADEMA kwa sasa inatokana na Falsafa, Itikadi, Mrengo na Sera zake. Utofauti kati ya CHADEMA na CCM, hauko kwenye kuwa ama kutokuwa na Ofisi, bali utofauti wao unajengwa na mitizamo tofauti linapokuja suala la kusimamia maslahi ya Taifa.
Wakati CCM wanataka madaraka ya nchi ili wajineemeshe, CHADEMA siku zote wanataka madaraka hayo ili kuineemesha Tanzania na kuwafanya watanzania waone ni baraka kuzaliwa na kuwa mtanzania. Utofauti huo ndiyo unaowafanya CCM kutumia nguvu kubwa sana kupambana kiharamu na CHADEMA na siyo utofauti wa kuwa ama kutokuwa na Ofisi.
Kama kuwa ama kutokuwa na Ofisi kingekuwa ni kigezo muhimu kwenye kutambua ubora wa Chama cha siasa, basi leo hii nchi yetu isingekuwa inayumbishwa hovyo hovyo na CCM. CCM inafanya mambo mengi yanayokera na kuharibu nchi yetu, lakini yenyewe ina Ofisi kwenye karibia asilimia tisini na tisa (99%) ya nchi yetu.
Wakati hela za Tegeta - Escrow zinaliwa, CCM walikuwa hawana ofisi? Wakati Kabudi anataja takwimu za uongo za fedha wanazodaiwa Barricks, CCM ilikuwa haina Ofisi? Wakati Professa Assad anafukuzwa kiharamu kwenye nafasi yake ya CAG, CCM ilikuwa haina Ofisi?
Ofisi ni Jambo la muhimu kwa chama cha siasa, lakini si takwa la kikatiba wala si kigezo cha ubora wa chama.