Kama kweli Mo Dewji kamuuza Chama katukwaza wana Simba

Kama kweli Mo Dewji kamuuza Chama katukwaza wana Simba

Hamna kitu nmeumia kama kuona taarifa Instagram za wachambuzi wa soka bongo kuwa chama tayari kashapigwa bei na picha ikimwonesha yupo na Tuisila Kisinda kwenye uzi wa waarabu. Mo sijui umetutendea haki, nmetoa chozi langu kumshtaki Mo kwa mwenyezi Mungu kama hili jambo likiwa kweli. Moo ulituahidi kuwa bado unajenga timu ya ushindani ndani na nje ya Africa kumbe upo kimasilahi. Sikuamini tena Moo Dewji, mbona hujatuuliza wana Simba ili tukupe mawazo, wewe umejichukulia uwamuzi. Asante kwa haya maumivu ulotupa wana simba aisee
Kazi yako kwenye simba ni kupanua mdomo na kupiga kelele, hujui wachezaji wananunuliwa, kutunzwa na kuuzwa kivipi. Kuna watu wamewekeza mabilioni kwenye Simba, wewe umewekeza kupiga kelele. Football is both entertainment and business
 
Wakati anamnunua wewe ulitoa mawazo au mchango gani? Acheni mihemko. Wachezaji wananunuliwa na kuuzwa pia. Simba mngemuacha angekuja kuondoka free. Ingekuwa hasara kwenu.

Hamna kitu nmeumia kama kuona taarifa Instagram za wachambuzi wa soka bongo kuwa chama tayari kashapigwa bei na picha ikimwonesha yupo na Tuisila Kisinda kwenye uzi wa waarabu. Mo sijui umetutendea haki, nmetoa chozi langu kumshtaki Mo kwa mwenyezi Mungu kama hili jambo likiwa kweli. Moo ulituahidi kuwa bado unajenga timu ya ushindani ndani na nje ya Africa kumbe upo kimasilahi. Sikuamini tena Moo Dewji, mbona hujatuuliza wana Simba ili tukupe mawazo, wewe umejichukulia uwamuzi. Asante kwa haya maumivu ulotupa wana simba aisee
 
Kwa taarifa yako Clatous Chama yuko Morocco na wenzake wanajifua tayari kwa msimu ujao. We endelea kuchafukwa nyongo kwa unazi wa kijinga wa Utopolo.

Mwaka jana tulioneshwa picha kavaa jezi ya vyura...
Na Kuna picha zingine yupo kwenye mazoezi na Berkane
Screenshot_20210813-090521.jpg
 
Hamna kitu nmeumia kama kuona taarifa Instagram za wachambuzi wa soka bongo kuwa chama tayari kashapigwa bei na picha ikimwonesha yupo na Tuisila Kisinda kwenye uzi wa waarabu. Mo sijui umetutendea haki, nmetoa chozi langu kumshtaki Mo kwa mwenyezi Mungu kama hili jambo likiwa kweli. Moo ulituahidi kuwa bado unajenga timu ya ushindani ndani na nje ya Africa kumbe upo kimasilahi. Sikuamini tena Moo Dewji, mbona hujatuuliza wana Simba ili tukupe mawazo, wewe umejichukulia uwamuzi. Asante kwa haya maumivu ulotupa wana simba aisee
Ulimleta wewe..? Alimleta Mo na atatuletea wengine tulia mpira biashara kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nacheka kama mazuri, ila SIMBA SC kuuza key players wawili kwa wakati mmoja bila kujua uwezo wa tuliowasajili, katika kuziba pengo ni ujinga mkubwa.

Ikitokea Hawa tuliowasajili kwasasa wameshindwa kudeliver kile tulichokuwa tunakipata kwa kina Chama na Miquisone,basi tujue kwamba tutakuwa wahanga uwanjani kwa muda usiojulikana mpka pale tutakaocheza kamari nyingine katika manunuzi.

Hebu tuifikirie ile Simba Sc uliyowahi kucheza mechi kadhaa huku chama na Miquisone wakiwa benchi, hakika ilikuwa ni kituko.Leo tunauza Chama na Miquisone alafu replacement ni kumuongeza Ajib mkataba seriously? Aiseeeh[emoji23]

Lakini pia tujue tu kwamba hii biashara imefanyika kwa siri sana na jaluna shabiki wa kawaida atakaekuja kujua hao wachezaji wameuzwa kwa bei gani, unajua ni kwanini? Sikuzote hatutakiwi kuona kwamba Simba inaingiza hela,tunatakiwa kujua tu kwamba hakuna faida inayoingia pale zaidi ya kupokea hisani tu.Hivyo hizo deals zitabaki kwa tetesi mpaka kiama,labda tuzisikie kutoka kwa hizo teams zilizowasajili.

Anyways tumeuza Triple C alafu tukamuomgezea mkataba AJIB , daah ngoja tuone.
Nadhani mauzo ya chama kuna kitu nyuma ya pazia, sidhani kama zilikua ni plan za simba kumuuza. Na ndio mana hata Ajib ameongezewa mkataba ghafla tu.
 
Kwanza sio kweli kuwa Chama kaondoka sababu ya mabishano na MO mitandaoni. Dili la Chama kuondoka lilianza muda kidogo kabla ya hata majibishano yao mtandaoni. Watu wengi hapa wanamlaumu Mo lakini hawajui nguvu ya mameneja/mawakala wa wachezaji. Timu yoyote ile hata Simba ikimuhitaji mchezaji kwanza huwa wanamtafuta meneja/wakala wa mchezaji husika wakishamuweka sawa basi biashara imeisha hiyo hata mchezaji awe na mkataba na timu yake. Jiulizeni beki mpya wa Simba kutoka Kongo ilikuwaje akasajiliwa Simba mwishoni wakati kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri Yanga na Aucho ilikuwaje akaenda Yanga wakati Simba walikuwa walikuwa wameweka mambo vizuri. Mameneja/mawakala wa wachezaji hawana tofauti na hawa madalali wanaopangisha vyumba mitaani wakati wao hawana nyumba. Sio ajabu dalali kukupeleka leo kwenye nyumba ukalipia mwaka mzima lakini baada ya miezi mitatu dalali huyo huyo akafanya figisu kwenye nyumba kuhakikisha wewe unahama kwa sababu tu kuna mtu anatafuta chumba kama alichokupangisha kwa pesa mara mbili.

Na kwenye suala la kuuzwa mchezaji timu nyingi zikipata ofa kwanza huwa wanamuita mchezaji na kujadiliana nae lakini wakati huo unakuta mchezaji tayari kashajulishwa na meneja/wakala wake. Msimu uliopita Miquison kwa mapenzi yake mwenyewe aliamua kubaki Simba japo alikuwa na ofa nyingi tu mezani. Na kikubwa zaidi mchezaji kama binadamu tena mtu mzima yoyote yule anapopata ofa kubwa huwezi kumzuia na iwapo ukijitia kumzuia ataanza vituko na kucheza chini ya kiwango. Sasa hapo hasara ni kwa mchezaji au timu husika? Mfano mdogo Morison wakati anataka kuondoka Yanga vituko alivyokuwa anafanya ilikuwa balaa kiasi hata watu wengi wa Yanga walikuwa hawataki aendelee kubaki Yanga bahati mbaya tu kwao alikuwa naenda Simba ndio maana sarakasi zikawa nyingi.

Kwangu mimi suala kubwa sio Chama au mchezaji yoyote yule kuondoka kwani wachezaji huja na kuondoka bali ni je Simba ilikuwa imejiandaaje kutafuta mbadala wake anayefikia walau hata asilimia 80% ya uwezo wa wake iwapo Chama ataaondoka ghafla?
 
Chama kaondoka aisee,pia dharau za Mo kwny Instagram Ile siku ukute imechangia pia Chama kuondoka.
Ni kweli kabisa, Fedheha ambayo Mo kampa CHAMA, bora ajiondokee tu. Huwezi kumuaibisha vile mtu hadharani. Pia sjawahi kuona Boss wa timu anafatilia wachezaji wake kwa kiasi cha kuwaaibisha hivyo. Hata kama deal la CHama lilikuepo tangia awali, Lakini kitendo cha MO ndio kimeleta chachu ya Chama kuondoka!
 
Na timu yoyote ile inayowazuia wachezaji kuondoka wanapopata dili kubwa isitegemee kupata wachezaji wazuri wenye malengo makubwa. Wachezaji wazuri wakishajua tu hawaji kusajili na hata wakija mikataba yao inakuwa na vifungu vingi vya kuibana timu husika. Jambo la msingi ni mchezaji na timu husika kuachana kwa uzuri ikiwezekana mchezaji siku nyingine anaweza akarudi tena kama ilivyotokea kwa Makambo na Yanga au Okwi na Simba.
 
Back
Top Bottom