Kama kweli Mungu yupo inabidi aniombe msamaha

kama wewe una uwezo wa kuumba au kumiliki uzima wa mtu basi atakuomba msamaha lakini kama binadamu amekopeshwa uhai na haulitambui hilo basi uombe msamaha kwa kile ulichokiandika.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengine mnakufuru na kujitafutia laana kipumbavu kabisa.

MHUBIRI 4:13 SUV

"Heri kijana maskini mwenye hekima Kuliko mfalme mzee mpumbavu. ambaye hajui tena kupokea maonyo."
 
Jamaa kama unatafuta trophy points kwa uzi wa kijinga namna hii unahitaji kujitathmini. Unakufuru kabisa yaani eti wewe Muumba mbingu saba na vyote vilivyo na uhai na visivyo na uhai akuombe wewe msamaha kweli...Pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hapo ndipo utakuja kuona habari za mungu zina ukakasi sana

Adam na eva baada ya kuasi kutokana na kushawishiwa na shetani, tunamuona mungu anatoa adhabu pamoja na laana kubwa kwa viumbe vyake ambavyo yeye mwenyewe amekiri kua havijakamilika. Hii pia ni adhabu ya uonezi kabisa kuwahi kutolewa na huyu mungu. Adamu atakula kwa jasho, huku eva/hawa akijifungua kwa uchungu pamoja na kupunguziwa miaka ya kuishi duniani

Lakini hatujaona mungu huyu akitoa laana kwa shetani kua kutokana na dhambi ya kumshawishi eva/hawa basi utatafuta kwa jasho, au utazaa kwa uchungu na hautadumu milele utakufa. Zaidi tunamuona mungu huyu pamoja na shetani wanatembeleana wakipiga soga. Wakati sisi huku vitabu vyake vimesema hatuwezi kumuona kutokana na dhambi tulionayo, je sisi tunadhambi gani kumzidi shetani mbona yeye anapiga stori na shetani ambaye ndiyo msababishi wa dhambi mpaka sisi kumuasi yeye?

Sent using unknown device
 
😂 😂😂 sasa kiumbe ambae huna uhakika kama yupo au hayupo akuombe msamaha si utakimbia
 
Kama mungu anatoa mitihani ili kuwapima viumbe vyake, niwazi kabisa kua huyu mungu hajui mambo ya mbele kabla hayajatokea.

Huwezi ukajua future ya mbele kua hata ukimpa mtoto wa chekechea mtihani wa form six hatofauru lakini umempa afanye hivyo hivyo. Haya matokeo yamekuja amefeli kama ulivyo ona katika maono yako mwanzo halafu unaanza kumu adhibu wakati ulishajua kua hatoweza kufauru

Mungu huyu hana tofauti na mfano huo. Kwasababu kabla hajakupa mtihani alishajua kua huwezi kufaulu.

Mtihani ni kipimo cha kujua kama mtu ameelewa au lah. Mungu kutumia mtihani kujihakikishia viumbe vyake kama vimemuelewa au lah, hiyo inatupa jibu kua mungu huyu hawezi kujua mambo yajayo na ndio maana tunamuona akitumia mitihani ili kujua, Mungu huyu wala hana uwezo wa kumsoma akili ya kiumbe wake ili kujua ufahamu wake ukoje kuhusiana na uelewa wa mambo aliyofunzwa yeye mwenyewe



Sent using unknown device
 
Quran 2-132
Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.

kama kweli unatafuta dini ya kweli hiyo apo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ibrahim alikuwa na dini gani na wakati gani? Mtume alikuja lini na alijifunza kuandika lini? Ninavyojua wayahudi walianza kuandika mapema na maandiko yao yapo toka wakiwa Iraq ila ya muhamad yalikuja kuandikwa baadaye. Ibrahim alikuwa myahudi sasa wapi na wapi na mwarabu?
 
wenye ulemavu wa viungo wanaimba na kumsifu Mungu wao wewe umzima lakini unakufuru. ukiambiwa urejeshewe Mama yako na achukue macho na Miguu yote au mikono yote unge chagua nini. Hata mimi nimeondokewa na mzazi mmoja ambae alikua tegemeo langu mpaka sikuendelea na form five lakini kiugumu niliishi tena kwa kufanya kazi zilizo nizidi umri lakini nilipambana kwakujitegemea nilitafuta hela ya kujilisha , kulipa kodi na nikajisomesha mpaka chuo. kwakipindi chote sikuwahi kulaumu ila nilishukuru kwakile nilicho pata Maombi yangu yalikua ni uzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ulikua unashukuru kwa nani?
 
Fact
 
Yapo mengi sana ya kumshukuru, lakini mshukuru kwa kukupatia hayo macho ambayo kwayo umeweza kuona na kusoma na kuandika huo ujumbe wako wa malalamiko juu yake na pia kwa hayo macho aliyokupa umeweza kusoma huu ujumbe wangu.
hayo yote hajanisaidia yeye
 
Yapo mengi sana ya kumshukuru, lakini mshukuru kwa kukupatia hayo macho ambayo kwayo umeweza kuona na kusoma na kuandika huo ujumbe wako wa malalamiko juu yake na pia kwa hayo macho aliyokupa umeweza kusoma huu ujumbe wangu.
hayo yote hajanisaidia yeye
 
Tuliookolewa na Mungu hatuwezi kufikilia ujinga kama huu, maisha yako ni zaidi ya ugumu wa maisha,
labda kama unayemtaka akuombe msamaha mungu wa nyumbani kwenu.
 
Mkuu huyu Mungu muache tu nna kinyongo nae sana

Ila ipo siku tutakutana nae tu muache aendelee kujificha
Yani kama upo serious kwa hili, basi jua unakosea sana. Lakini kama upo kiutani, basi nakushauri utafute kitu kingine cha kufanya nacho utani. Mungu anaweza akakufanya ukawa kichaa watu washangae imekuaje kuaje ukawa kichaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JF kuna vichaa humu ndani. Haiwi kwa thread hii iwe imeandikwa na mtu mwenye akili timamu. Haya maendeleo ya sayansi na teknolojia yanapelekea mpaka vichaa wawe wanamiliki simu,laptops wanaingia mitandaoni wanadhihirisha uwendawazimu wao. Nashukuru kwa kumjua mwendawazimu wa kwanza humu jf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…