Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"

Kama wanzanzibar wakiniunga mkono twende serikali moja wakikataa basi bhana serikali 3 haziepukiki!

Mbona kila kukicha tunaanzisha mikoa mipya na wilaya mbona hatuhoji gharama? Na ccm inapeleka makada kuwa wakuu wa mikoa na wilaya mbona hatuhoji?
 
Kama wanzanzibar wakiniunga mkono twende serikali moja wakikataa basi bhana serikali 3 haziepukiki!

Mbona kila kukicha tunaanzisha mikoa mipya na wilaya mbona hatuhoji gharama? Na ccm inapeleka makada kuwa wakuu wa mikoa na wilaya mbona hatuhoji?

Kama nikweli hoja kuu tunayo fafanuliwa na CCM ni kuhusu gharama kama tutakubaliana muungano wa serikali 3. Basi nami naungana na Bw. Pasco katika hill la serikali moja. Kwani serikali moja inaleta picha nzuri ya muungano makubaliano katika kuungana kuliko kuwa na serikali mbili, moja ya muungano na upande mwingine unabaki na serikali yake ya awali. Otherwise kuwa na serikali ya muungano, na kama kubakiza serikali za awali basi iwe kwa pande zote.
 

Lyimo, ni sawa.kama utakubaliana na Warioba aliwahi kusema serikali 3 itakuwa ni gharama kidogo sana ukilinganisha na zile za serikali 2.maana wabunge wa baraza la wawakilishi hawatakuwepo kwenye bunge la Tanganyika maana hakuna wanae muwakilisha kaka.
 
Wanabodi, hii nimeikuta humu iliandikwa na Mkuu Mzee Mwanakijiji, miaka 2 ilyopita!. Kumbe wakati sisi tunazungumza haya leo, wenzetu walizungumza kitambo!.

Asante Mzee Mwanakijiji, nadhani now its high time tuunde pressure group ya serikali moja!. Kama rasimu inapendekeza serikali 3!, CCM imeamua kutupilia mbali maoni ya serikali mbili!, then kama nia ni kuulinda muungano, why not serikali moja?!.
Pasco
 

Count me in! Say NO to Serikali 3! Tangu lini Baba (Seikali ya Muungano), Mama (Serikali ya Tanganyika) na Mtoto (Serikali ya Zanzibar) wakawa na hadhi sawa na eti kukawa na amani na raha mstarehe? Hiyo ya Baba, Mama na Mtoto nimeweka kama illustration tu, msinielewe vibaya!
Katika Ibara ya 8 ya Rasimu ya Katiba Jaji Warioba ameweka usawa huo huku akiamini kuwa eti ni "kudumisha Muungano!" Kaingizwa mjini mzee huyu bila kujijua!
 
Tanzania si huru bali imefanywa kwa muungano huru wa nchi huru yaani tanganyika 9.dec.1961 na zanzibar 05.01.1963.Kwa kuwa kila mwaka tuna adhimisha uhuru wa tanganyika,basi tanyika ipo ila dormant state'imevaa koti la Muungano'.JE KWA NINI TANGANYIKA ISIVUE KOTI HILO?
 
Serikali 1 inamanisha nchi moja. Kati ya hizi nchi 2 ni ipi itakayokubali kujiondolea mamlaka yake kama nchi na kuyaweka kama sehemu yake kwenye Muungano? Hapa ni wazi znz ndo wahanga kwa nchi yao kumezwa, ni wazi hawako tayari. Lakini pia watz bado nao hawaoni uhalisia na umuhimu wa muungano huo, ivo kusema tu solidify kupata ser 1 kwa wananchi halina mashiko yeyote. Zaidi sana tukumbuke hata mume na mke wanaofunga ndoa, wasipokuwa na mtazamo mmoja na malengo ya pamoja wanayotaka kuyafanikisha, huku kila upande ukionyesha na kutoa mchango wake kikamilifu, ni dhahiri kuwa muungano wao utavunjika ama kuingia ktk mgogoro
 
Nawatakia mapumziko mema ya leo siku ya Muungano.

Pasco
 
Kila mtu ana interest duniani ni rahisi sana kuzibadilisha interest za mwenye uwezo mdogo uitaji ushawishi mkubwa.

Kwa levels zako Pasco sio mtu mdogo; ifike wakati sasa tukisoma thread za Pasco tunajua kama ni swala la dini mlengo wa Pasco akidadavua unapata perspective fulani, kama ni siasa sio lazima uwe na chama lakini tutegemee principal za Pasco zitaenda na ideology, Muungano na chochote kwenye matukio ya siasa tuangalie mtazamo wa Pasco kwa principles zake; ni sawa na kumsoma Mag 3, Mzee tupatupa wa lumumba, au committed party members unajua mtazamo gani kabla ujasoma.

Kwa nyie wadadavuajia sio lazima muwe na mitazamo ya wanachama au unazi wake, lakini ideology ya mtazamo; sasa Pasco leo kasema hivi kesho atasema vile kwenye hoja hiyo ile ile kama unamfuatilia kwa miaka mitano mazingira hayo hayo anaweza yapa perspective kama tano. Matokeo yake Pasco as a brand aeleweki what drives pasco kimsimamo ata kama hoja zake zina mashiko.
 
Nadhani now its the most opportune time, twende kwenye serikali moja kuimarisha muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , kwanza naunga mkono hoja ya nchi moja, serikali moja chini ya rais mmoja.


Pili, kwa vile maoni haya uliyatoa a way back kabla ya mchakato wa Katiba, and now it's very unfortunately tumeingia kwenye mchakato wa katiba bila kufanya a national convention ya kupata a consensus ya Tanzania tunataka kutengeneza taifa la aina gani, muungano wa aina gani, union or federation, kwa sasa muungano wetu ni both union kwa upande mmoja, na federation kwa upande mwingine which is very unique na ndipo kwenye mzizi wa fitna.

Sasa kwa vile mchakato ulikamilika, na tunachosubiri sasa ni kukamilisha tuu mchakato kwa referendum ya kuikubali au kuikataa, nilitegemea utupe update ya maoni yako kwa hapa tulipo and a way forward

P
 
Mkuu DASM , siku zote humu jf, mimi ni mkweli Daima kwa kuusema ukweli uliopo no matter what. Nimeandika mengi kuhusu muungano. Hili ni moja ya mabandiko hayo.
P
 
Mkuu Pascal unamaanisha unachoongea, au unaongea ili watu fulani waone msimamo wako?
Mkuu Lycaon pictus, angalia tarehe ya bandiko hili.
P
 
Hakuna kisichowezekana chini ya jua! kama mwanzo tuliweza kwa nini sasa tushindwe?
Pasco
Naunga mkono hoja. Mfano kipi rahisi Zanzibar kuwa na mwana chama FIFA au kuungana na Tanzania Kama Timu moja,
Tuanze kuongeza mambo ya muungano na kupunguza mambo yasiyo ya muungano kamakweli ipo dhamira ya kudumisha muungano wetu
 
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Naunga mkono hoja japo wanasema serikali moja nchi moja itamezwa ... !

Ila hata huu wa serikali mbili bado kuna nchi moja ya huku mainland imemezwa...
 
eo ni Sikukuu ya Muungano, nachukua fursa hii kuutafakari Muungano wetu adhimu, kupitia hoja mbalimbali za kimuungano.

Nawatakia maadhimisho mema ya muungano na mapumziko mema.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…