Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Very interestingMkuu Tujitegemee, safari ya kuelekea kwenye serikali moja ndio njia pekee ya kuuimarisha muungano kwa dhati, kwa sababu nauhesabu muungano wetu kama ndoa, "mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataandamana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja!". This is a very big sacrifice!.
Ili kuimarisha kuiimarisha hiyo ndoa lazima hizi big sacrifices za kuachana na baba yake na mama yake zifanyike, na kuandamana na mkewe!. Wale wanandoa wanaendelea kukaa kwa wazazi, ndoa zao hukumbwa na matatizo!
Tanganyika na Zanzibar zilipoungani, ni Tanganyika pekee, ilitoa the biggest sacrifice, ya kuupoteza utaifa wake, ikauua kabisa for the sake of union na kuwa Tanzania!. What sacrifice did Zanzibar did?!. You can't eat your cake and have it! Kama mmemsikia vizuri Jaji Warioba, wazo la muleta serikali tatu, ili ili kuibembeleza Zanzibar ibakie kwenye muungano kufuatia katiba ya Zanzibar kuuvunja muungano kimya kimya huku bara ikinyamaza, ikimchelea mwana kulia!
Kwenye thima ya Muungano, Tanganyika iliishakufa zamani, hivyo nchi inayoitwa Tanganyika, haiwezi tena kukufufuka!, this is a very big sacrifice!, dhima hiyo ikaitambulisha Zanzibar kuwa "sii nchi" bali "ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" yenye mamlaka yake ya ndani!. Katiba ya Zanzibar ya 1984 (Toleo la 2010), linaitambulisha Zanzibar kama nchi, ndani ya JMT, ina weka mipaka yake!, bendera yake!, wimbo wake wa taifa!, na kumtambulisha rais wa Zanzibar kama Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la JKU na Vikosi vya SMZ!, uliwahi kuona wapi nchi ndani ya nchi?!.
Inaonekana kana kwamba Zanzibar inabembelezwa ibaki ndani ya muungano kwa kuiacha ifanye kila inanachotanga!, kama ni sacrifices, only Bara!, kila kitu ni Bara!, wajumbe wa tume ya kukusanya maoni 50/50!, kugharimia gharama za tume, ni bara asilimia 100!. Sasa bunge la Katiba, nalo linagharimiwa 100% na bara!.
Sasa kama nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, its about time, Zanzibar nayo, itoe sacrifice, ipoteze utaifa wake!, tende kwenye nchi moja, serikali moja na rais mmoja, tena ili kuwapunguzia machungu, wenzetu, katiba itamke rais wa kwanza, atatoka Zanzibar (awe Dr. Shein).
Nimeitaja CCM kwa sababu tukubali, tukatae, CCM ni chama dola!, kama kiliweza kuamua yale mengine!, na kama nia ya dhati ni kuimarisha muungano, sio serikali tatu!, sio serikali mbili!, ni serikali moja!
Pasco.