Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"

Very interesting
 
Naunga mkono hili bandiko.

Inashangaza ana kuona eti kuna muungano lakini Zanzibar kuna ZSSF,ZRA,Bodi yake ya mikopo nknk ambavyo ni kwa ajili ya wazanzibar tu Mtanganyika huruhusiwi kusogeza pua halafu kuna NSSF,HELSB nknk ambavyo ni kwa ajili ya Mtanganyika na Mzanzibari

Hiyo Tanzania iko wapi?
 
Serikali moja ndio wazo la wasio na uchu na tamaa za madaraka Serikali 3 ni mzigo wananchi masikini kuzilisha zote
 
Leo tunapo adhimisha miaka 60 ya huu muungano wetu adhimu, nafanya tafakuri, niliwahi kuandika nini humu kuhusu muungano wetu.
Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya muungano wetu adhimu.
Ujumbe wangu ni muungano wetu adhimu udumu milele, na sasa ni muda muafaka tuachane na huu muungano wa kimaghumashi, wa union na federation, sasa twende kwenye muungano wa kweli wa union wa nchi moja, serikali moja, na rais mmoja!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Tusaidie
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…