Kama kweli Sabaya ana hii hatia leo aburutwe Mahakamani

Kama kweli Sabaya ana hii hatia leo aburutwe Mahakamani

Kama kweli alimteka na kumtesa kwa kipigo kikali Diwani wa Kata ya Sombetini, Bakari Msangi huko jijini Arusha basi alifanya kosa kubwa sana.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sauti Kubwa ni kuwa Bakari Msangi alienda kutoa msaada kwa vijana waliokuwa wamewekwa chini ya ulinzi na Sabaya na timu yake kwa tuhuma ya kufanya biashara ya fedha za kigeni bila kibari. Diwani Msangi alipigiwa simu na ndugu Ally Saady ili akatoea msaada.

Inasadikiwa vijana waliowekwa chini ya ulinzi na Sabaya na timu yake walipigwa kipigo kikali na baadhi yao kujisadia haja kubwa na ndogo na kujeruhiwa vibaya. Diwani Msangi alipofika kutoa msaada nae alipata kichapo.

My take; kama hizi tuhuma ni kweli leo hii Sabaya akamatwe na jumatatu afikishwe mahakamani. Asipofikishwa mahakamani basi tunajua ni unafiki wa kisiasa unaendelea.
Kwa hiyo unampangia Raisi nini cha kufanya
 
Nauliza tuu

Hivi Kinana na Mwigulu wana jisikiaje kwa aliyo yafanya Sabaya.??

Kuna taarifa kwamba wakati Sabaya akiwa na kesi ya kugushi kitambulisho alie muokoa kwanye hili janga ni alie kuwa Katibu mkuu wa Ccm wakati huo bwana mkubwa Kinana baada ya kuombwa na bwana mwingine alie kuwa mwenezi wa chama hicho rqfiki yetu Mwigulu.

Na kweli kesi ilifutwa japo hukumu ilisha andaliwa ya kumpeleka Sabaya akarushe ndege Kisongo. Wenye kumbukumbu mta kumbuka Sabaya alivyo kwenda na wahuni wengi mahakamani kumshangilia maana alisha jua matokeo.

Ukuu wa Wilaya aliupata kwa chapuo za hao hao wawili kama fadhila ya kutekeleza jambo moja baya sana Arusha dhidi ya Chadema.

Nitaliweka siku nyingine.
Leo kaondoshwa kwa aibu. Je? Mwigulu na Kinana mna la kusema?
 
Mkuu huwezi kumkamata suspect(s)bila ya kumfungulia mashitaka na polisi kufanya uchunguzi ili kuthibitisha tuhuma na mwishowe DPP to apply mind kuona kama kuna winnable case,sio vema kukamata watuhumiwa na kuwaweka mahabusu wakati upelelezi bado haujafanyika,kama una uchungu na hizi tuhuma mshauri huyu Diwani akafungue kesi polisi.
hivi ndivyo inavyopaswa kuwa ,ndo maana hatuelewi masheikh wa uamsho wanafanya nn
 
Kama hizi ni tuhuma za kweli basi Sabaya ni JAMBAZI lililokuwa ndani ya Serikali.
 
Huu ukweli mbona wahusika walikuwa hawaujali? Mkuu wa Mkoa alimkemea hadharani kuwa asiwasweke watu ndani bila kufuata utaratibu lakini alimpuuza. Akae ndani kama ilivyo ada kwa wengine wakati uchunguzi unaendelea.

Tena kwenye hili lenye mashahidi kibao wala hafurukuti. Na hao vijana aliokuwa anawatumia hawatakawia kumuachia mzigo.
Alionywa sana lakini hakutaka kusikia. Sasa ni wakati wa kuvuna alichopanda.

Amandla...
Ukiwa CCM unaua hadharani, unasishwa kupisha uchunguzi. Kisha unaachiwa huru.
Je unakumbuka ya Ditopile, Akwilina, yule mwandishi aliyeuwawa Nyololo (Iringa), .....?
Ukiwa ni mungu mtu
 
Kosa la jinai alafu Diwani afungue kesi? Anyway naanza kupata picha huenda Sabaya anasingiziwa.
Mkuu tuishi kisheria how polisi wafanye upelelezi bila ya docket?Diwani ndio anayeona amefanyiwa ukatili huu na suspect,ni wajibu wake kwenda police post na kufungua mashitaka.
 
Huu ukweli mbona wahusika walikuwa hawaujali? Mkuu wa Mkoa alimkemea hadharani kuwa asiwasweke watu ndani bila kufuata utaratibu lakini alimpuuza. Akae ndani kama ilivyo ada kwa wengine wakati uchunguzi unaendelea.

Tena kwenye hili lenye mashahidi kibao wala hafurukuti. Na hao vijana aliokuwa anawatumia hawatakawia kumuachia mzigo.
Alionywa sana lakini hakutaka kusikia. Sasa ni wakati wa kuvuna alichopanda.

Amandla...
Visasi sio vema unanikumbusha era ya mwendazake,tuishi kwa kuheshimu wajibu wa kisheria,our President Samia ameshaonyesha nia ya kuifanya nchi yetu iwe ina heshimu sheria zake.
 
Vigilantes kesho tunaanza kazi, lbda afichwe tusimbambe, tukimbamba ama zetu ama zake, mama kaanzisha tu, sisi tunamalizia
 
"sio vema kukamata watuhumiwa na kuwaweka mahabusu wakati upelelezi bado haujafanyika"

Mkuu mbona watu tumekaa sana mahabusu kwa kunyimwa dhamana na upepelezi haujakamilika ?? Mkuu hizi sheria labda huwa wanafanyiana favour kutegemeana na mtu.

Mpaka sasa kuna watu wanateseka mahabusu na uchunguzi bado haujakamilika. Na baada ya uchunguzi akikutwa hana hatia hana lolote la kudai na muda wake aliopotezewa.

Hii nchi ukitaka kuishi vema nimegundua tafuta pesa na power. Masuala ya sheria ni upuuzi. Hatuna wafanyakazi wazalendo wengi wapo kimaslahi. Nimeyaona mengi polisi, rushwa ipo na kamwe hakuna kiongozi wa kuja kukomesha rushwa hii nchi.
I understood you ila hatuwezi kufanya uhalifu huu kuwa ni sehemu ya maisha yetu,hatuwezi kuhalalisha haya mkuu wangu na sio mabaya mawili yanatengeneza jambo moja jema!
 
Hivi nani aliruhusu mtu kama Sabaya akawa ndani ya ofisi za umma? Mbona anaonekana hayuko sawa kiakili na ni mtu mkatili sana? Tena mwenye tamaa kubwa ya mali
 
Mkuu huwezi kumkamata suspect(s)bila ya kumfungulia mashitaka na polisi kufanya uchunguzi ili kuthibitisha tuhuma na mwishowe DPP to apply mind kuona kama kuna winnable case,sio vema kukamata watuhumiwa na kuwaweka mahabusu wakati upelelezi bado haujafanyika,kama una uchungu na hizi tuhuma mshauri huyu Diwani akafungue kesi polisi.
KWA iyo wale waliomahabusu miaka minne ,8 ni sio binadam ,nae akae KWA taratibu zilezile wakati uchungunzi unaendelea, lahana Sana huyu jamaa
 
Sabaya akae ndani miaka 8 kwanza kama wazee wa uhamsho kusubiria ushahidi kukamilika
 
Kama kweli alimteka na kumtesa kwa kipigo kikali Diwani wa Kata ya Sombetini, Bakari Msangi huko jijini Arusha basi alifanya kosa kubwa sana.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sauti Kubwa ni kuwa Bakari Msangi alienda kutoa msaada kwa vijana waliokuwa wamewekwa chini ya ulinzi na Sabaya na timu yake kwa tuhuma ya kufanya biashara ya fedha za kigeni bila kibari. Diwani Msangi alipigiwa simu na ndugu Ally Saady ili akatoea msaada.

Inasadikiwa vijana waliowekwa chini ya ulinzi na Sabaya na timu yake walipigwa kipigo kikali na baadhi yao kujisadia haja kubwa na ndogo na kujeruhiwa vibaya. Diwani Msangi alipofika kutoa msaada nae alipata kichapo.

My take; kama hizi tuhuma ni kweli leo hii Sabaya akamatwe na jumatatu afikishwe mahakamani. Asipofikishwa mahakamani basi tunajua ni unafiki wa kisiasa unaendelea.
Ameshafikishwa vipi kuna jingine Tena unataka ndugu yangu?
 
Uzuri wake nishakureport subiri ban yako upumzike ujifunze nidhamu
 
Back
Top Bottom