Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Asalam-aleikoum Wana-JF,
Nimeona nitoe hoja yangu kuhusu maamuzi ya wanasiasa ya kuanzisha tozo kubwa za miamala ya mitandao kwa kisingizio cha kujenga uchumi. Lakini matokeo yake tunayaona, watu wanalia kila kona ni maumivu.
Hoja yangu ni kwamba badala ya tozo hizi mpya ambazo ni kuongeza makodi juu ya makodi, na ni jambo ambalo linadhoofisha shughuli za uchumi kupitia mitandao ya simu, serikali ingeshusha bei za vifaa vya ujenzi kama cement, mbao, mabati, misumari, nondo nk ili kuchochea shughuli za ujenzi nchi nzima.
Siku serikali ikifanya uamuzi huo nchi nzima itarindima kwa ujenzi kila kona! Na hivyo wananchi wengi watapata ajira, watalipa kodi zaidi ili serikali nayo iendelee na ujenzi wa hayo ma-SGR, madaraja nk. Lakini uamuzi huo utawawezesha wananchi wengi kujenga nyumba bora za kuishi, kuliko hivi mlivyopandisha bei za vifaa vya ujenzi marudufu hadi watu wamekata tamaa, hakuna ujenzi hakuna ajira.