Akili hii ni ndogo kabisa!
Unaweza kutuambia udikiteta wa Hitila hapa na mapana yake, halafu ukatwambia udikiteta wa Magufuli unahistoria na kukubalika hivi katika nchi ngapi duniani?
Inapotajwa orodha ya madikiteta Duniani, Magufuli yupo au chuki za kijinga tu?
Udikiteta unaozuia maliasili za nchi kuibiwa, huo ni udikiteta mzuri na unafaa sana
Udikiteta unaowaondoa kazini wajinga na waliokuwa wakifanya operations za kichwa badala ya mguu huo ni udikitea bora sana
Hata haiitaji akili nyingi sana kulitambua hili.
Ukiskiliza sababu za wengi wa hao wanaomchukia hayati Magufuli kupitiliza wanakwambia alikuwa muuaji,mporaji,mtekaji mara sijui udikteta n.k.
Lakini kiukweli ndani ya mioyo yao hayo si mambo yanayofanya wamchukie Magufuli isipokuwa tu hizo ndio sababu wanazoona zina maana wakizitaja mbele za watu kujustify chuki zao kwa yule mtu...
Si kweli kwamba eti wanaumizwa sana na utekaji wa Mo, si kwamba eti wanaumizwa sana na matukio ya kinyama waliofanyiwa akina Aliphoso Mawazo,saanane na wengineo awamu ile.....nasema hivi si kwa lengo la kubaliki vile vitendo vya kiovu hapana, maana vingeweza kunitokea hata mimi.
Wengi wanaomchukia bwana yule ni kwa sababu zao binafsi tu ambazo ni kuharibiwa mifumo ya kuendesha maisha yao binafsi kwa njia za shortcuts na ujanja ujanja ambazo walikuwa wamezizoea kwa miaka mingi kabla ya awamu yake.
Nakumbuka baada ya jamaa kufariki kuna mzee mmoja pale Mwanza ni mfanya kazi mkongwe wa NIMR alionesha kufurahi mno akisema kabisa kwa watu, kwamba tangu aanze kufanya kazi kwenye hiyo taasisi hakuna kipindi ambacho aliishi kwa shida sana kama kipindi cha Magufuli, sababu pesa zilikuwa hamna yaani ilikuwa kila wakiandika Proposal kwenda wizarani kwa ajili ya kujiingizia pesa zilikuwa zinapigwa chini au kama sio kupigwa chini basi wanawekewa mlolongo mrefu sana wa kuzipata hizo hela za Proposal, mpaka ikafika kipindi wakaacha hata kuandika Proposal wakawa wanasubiri zile za kutumwa na serikali. Kwa hiyo kifo cha Magufuli alitegemea kitampa haueni kubwa sana kwa maana ya kurudi kwenye yale maisha ya miaka ile ya kujichotea tu pesa za serikali...... na hata huyu mzee naye leo hii ukipiga nae stori kwa mtu ambaye hamfahamiani sababu za kumchukia Magu atakazozitaja ndio hizi hizi kama wanazosema hawa jamaa muuaji,dikteta, n.k
Ukitaka kuamini hawa haters wa marehemu Magu hizo wanazotaja sio sababu halisi zinazowafanya wamchukie angalia sasa hivi kuna matukio mengi sana ya kinyama yanaendelea hapa nchini kama ulawiti kwa watoto wadogo,upotevu wa mabinti wadogo kupitia biashara ya kusafirisha watu(humantraficking), mapadre kuuwawa(kumbuka tukio la kule mbeya),utekaji wa nyara na mauaji ya kiholela( kule kawe beach mwaka jana ilikuwa kila ifikapo weekend lazima watu waokote maiti) bado kuna ujambazi uliokithiri raia wanaonewa na kuporwa mali zao.... yote haya yanaendelea lakini huwezi kuwaskia hawa wapenda amani wakiongelea au kukemea sana sana utawakuta kwenye mada kama hizi wakijifanya wanauchungu sijui magufuli alikuwa ni mtekaji,dikteta n.k
Binafsi mimi Nikimskia mtu kama Tundu Lisu au mzazi wa Ben saanane analezea chuki zake kwa magufuli nitamuelewa sababu hawa wachache niliowataja walikuw ni wahanga kweli kweli wa awamu ya tano.... lakini hawa wengine machawa wa mafisadi na watumbuliwaji wa vyeti feki huwa nawadharau sana na ndio wengi.