Kwenye familia nyingi kuna watu hasa vijana wanaopitia majaribu mengi ya kimaisha wakati wakijaribu kujua na kujiuliza kwanini wapo hapa Duniani. Kwenye kipindi hiki hawa ndugu wengi wakiwa vijana ni wakati mgumu sana kwenye maisha yao.
Haya matukio yamekuwa yakitokea kila siku lakini wengi wetu hatuyapi uzito mfano kijana akiamka na kusema kuanzia leo mimi ni tofauti nimeokoka na sitaki kula hiki au kile ni huyu pia ni Hamza, wengine wanasema sitanyoa nyewe nitakuwa Ja kama Bob Marley na kukuza marasta huu pia ni U hamza, wengine wanakuwa kama vichaa kwa usongo wa mawazo huu pia ni uhamza.
Lakini vilevile kuna watu wanatumia wakati huu wa hawa vijana kuwafundisha vitu vibaya kama kuchukia serikali, jeshi, kubagua watu kwa rangi zao, ubaguzi wa dini, matabaka na kuchukia matajiri. Na wengine kwa kushawishiwa wanaweza hata kuuwa watu hao.
Hakuna mtu mwenye akili zake sawa anaweza kwenye kuuwa mtu. Matatizo ya akili sio kuwa kichaa pekee mabadiliko yeyote hata kama ni mawazo yakabadilisha tabia ni tatizo la akili. Tunasikia watu kila siku wanasema nilipata depression hili ni tatizo la akili!, hazira zilizo pindukia hili ni tatizo la akili, wakati mwingine ukiona watu wanabadilika kila siku ni tatizo la akili.
Tatizo kwenye familia zetu unamsikia kijana anasema mimi nitaua mtu lakini tunapuuza, tunasikia vijana wanaongelea wamechoka kuishi tunaona ni ujana tu lakini wakati mwingine ni ishara kwamba kuna tatizo. Tukiona ndugu au jamaa ameweka hasira na kundi fulani kiasi cha kufikiri kuchukua maisha yao tujue kwamba kuna tatizo.
Ukimwona mtu amepania sana kulipiza kisasi vilevile ni tatizo na ni tatizo la akili. Mfano mzuri wa tatizo la akili ni hasira ukikasirika hauna tofauti na mtu mwenye matatizo ya akili tofauti ni kwamba hasira ni ya muda lakini chukulia kwamba hiyo hasira haiishi ungekuwa mtu wa aina gani?
Hivyo tukiona mtu hayuko sawa tutafute njia za kumsaidia mapema hata kama ni kwa kwenda polisi.