Kama labda unajiuliza kwanini Kipa Peter Manyika Jr leo anadaka sana jibu ni hili...

Tatizo huyo dogo maji kupwa maji kujaa,,,


Akija mjini mademu wengi sana,,,Bora tu abaki Singida,,, Tumuone katika kiwango hicho hicho,,,


Yasije yakatokea ya Karius!!!
 
Pigo la mwisho alishakubali akaokolewa na post mbona husemi?
Sasa ukikubali mpira ukupite lakini usiingie wavuni, yaani utoke nje au ugonge post, kuna tatizo gani? Maana yake ni kwamba alijinyoosha hadi mahali salama kulinda lango, na huo mpira haukuwa na madhara. Au ulitaka makipa wawe wanairukia mipira yote hata inayoenda kutoka nje?
 
Ila sipendezewi baadhi ya mashabiki wa Simba kumtukana kocha mkuu.

Sijaona kosa hadi kushushiwa lawama na matusi yule mzee, tubadilike tusijifanye makocha
 
siku moja matola akipewa simba, vikombe kedekede[emoji16]

Matola namuheshimu na Rafiki yangu wa siku nyingi sana na ni Kocha mzuri mno ila ana tatizo moja la Kuwagawa Wachezaji, Kupenda 10% kwa wale anaowapanga Kucheza tabia mbaya aliyoirithi kutoka kwa Kaka zake akina Abdallah King Kibaden na Jamhuri Kihwelo Julio na anapenda mno ' Ukubwa ' tabia ambayo Watani zangu ' Waha ' wanayo sana tu kama una uzoefu nao.
 
Tatizo huyo dogo maji kupwa maji kujaa,,,


Akija mjini mademu wengi sana,,,Bora tu abaki Singida,,, Tumuone katika kiwango hicho hicho,,,


Yasije yakatokea ya Karius!!!
Mkuu hivi karius ameitwa national team?
 
Ila sipendezewi baadhi ya mashabiki wa Simba kumtukana kocha mkuu.

Sijaona kosa hadi kushushiwa lawama na matusi yule mzee, tubadilike tusijifanye makocha
Aaah hhha simba noma,kwa hiyo sasa hivi wanatamka Masoud
 
Tatizo huyo dogo maji kupwa maji kujaa,,,


Akija mjini mademu wengi sana,,,Bora tu abaki Singida,,, Tumuone katika kiwango hicho hicho,,,


Yasije yakatokea ya Karius!!!

Uko sahihi 100% Mkuu Kipa Manyika Peter Jr kilichomgharimu alipokuwa Simba SC ni kupenda sana ' Starehe ' na hasa Mwanamke aliyemmaliza alikua ni Yule Binti kutoka Familia ya Kitajiri na Mbunge wa Bunge la JMT aitwae Najma kwa kila mara kumfuatafuata Manyika Jr Kambini, kumpa Gari yake, Kumpa Pesa na kutaka waende Kula Bata. Akina Hanspoppe walimsema sana huyu Dogo lakini siku zote Sikio la Kufa huwa halina dawa. Hata hivyo natumai ' msoto ' alioupata huko Singida United akirejea hapa mjini Msimbazi atakuwa tayari ameshakuwa ' matured ' hivyo atabadilika na kutusaidia mno. Ni Kipa mzuri sana ila ' Starehe ' na ' Utoto ' ndiyo vilimmaliza na labda Wanasimba wote tumshukuru sana Baba yake ambaye alitumia muda mwingi sana ' Kumpika ' upya Mwanae Manyika mara kwa mara pale Uwanja wa Karume na si ajabu vitu ' adimu ' alivyovifanya leo yawezekana ndiyo yale ' Mafunzo ' maalum aliyokuwa akipewa na Baba yake. Simba SC kama tutamrudisha Kikosini na akisaidiana na Aishi Manula kisha tukambakiza yule Kipa ambaye tulimtoa Toto Afrika na tumwache Said Nduda tutakuwa imara sana golini.
 
Ila sipendezewi baadhi ya mashabiki wa Simba kumtukana kocha mkuu.

Sijaona kosa hadi kushushiwa lawama na matusi yule mzee, tubadilike tusijifanye makocha

Watu wote wanaomchukia na kumsema vibaya Kocha wa Simba SC Mfaransa Pierre Lechantre hawajui mpira halafu ni ' Wapuuzi ' hakuna mfano. Ndiyo maana kuna muda mwingine huwa naamua tu kunyamaza na kuwaangalia tu Watu ambao hata a,b,c's za mpira hawana na hawajui.

Leo hii kila ' Mpuuzi ' anasema Timu apewe Masoud Irambona Djuma huku wakimsifu kuwa ndiyo anaiwezea Simba na anajua kufundisha. Ili uone kuwa Wapenzi wa mpira wa Simba SC kama si Tanzania kwa ujumla baadhi yao ni ' Wapuuzi ' hawa hawa ambao leo hii wanampigia ' Chapuo ' Djuma apewe Timu ndiyo hawa hawa wakati Simba SC imefanya vibaya katika Kombe la Mapinduzi kule Zanzibar ndiyo walikuwa mitandaoni wakimtaka aondolewe au awe chini ya Kocha Mkuu.

Hivi kwa Mtu anayeujua kweli mpira ' Kindakindaki ' anaweza kuthubutu kumfananisha Lechantre na Djuma? Hivi Djuma ana CV ya hata kuifikia robo ya CV ya Lechantre? Kuna kuna Mwafrika yoyote mfuatiliaji wa Mpira ambaye leo hii hajui uwezo mkubwa alionao Lechantre? Kuna vitu vingine huwa vinatia hasira hadi Mtu unakosa hata uvumilivu.

Wanaojua mpira huangalia Kwanza matokeo ya Uwanjana na aina ya Uchezaji wa Timu huja baadae na wala siyo Kipaumbele sana kwani Timu haiwi Bingwa kwa kucheza ' Sexy Football ' badala yake Watu hutaka matokeo na Vikombe pekee kitu ambacho Simba SC imefanya safari hii.

Upuuzi huu wa kutaka Simba SC icheze mpira wa Kitabuni pekee ndiyo umeigharimu hata Klabu ya Arsenal ambayo kwa mpira wake huo wa ' Kuburudisha ' Watazamaji sasa ina miaka ya Umri aliona mdogo wangu wa Kike wa miaka 22 kama sijakosea bila kuchukua Kombe ya EPL huko Uingereza.

Sioni sababu yoyote ya Kocha Pierre Lechantre ' Kufukuzwa ' Simba SC na badala yake nadhani sasa huyu Kocha apewe Mkataba mrefu ili aitengeneze Simba yetu Kimataifa zaidi. Halafu Kocha Djuma ' aonywe ' haraka aache tabia yake ya kupika ' majungu ' kwa baadhi ya Wachezaji ' Waandamizi ' wa Simba SC ili ' wachomeshe ' akishirikiana na baadhi ya Wanachama wa Simba SC ambao wanampenda Kinafiki ili Timu iharibu halafu Lechantre afukuzwe na akabidhiwe Timu yeye.

Ni hayo tu Mkuu na tupo pamoja.
 
Mkuu, umeongea ukweli mtupu na kitaalamu bila ya kuacha kitu na Pierre aongezewe mkataba tu.Naunga mkono hoja mkuu

Pamoja sana mkuu.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Uandishi wako mwanzoni ni mzuri ila mwishoni umeonyesha yote ukiyoandika ni hisia zako tu
 
Mpira umempita kati ya kwapa na kiuno.
 
Hajatosha wa kurudi SIMBA.. IKIBIDI apigwe bei jumla ili siku akikaa kwenye kiwango cha ubora anunuliwe.
Sio mechi 1 au 2 pale simba ataozea bench tu.. Manyika onyesha uwezo wako zaid ya hapo season mpya yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…