Kama leo ungekuwa ndio unatimiza miaka 26 ungefanya nini?

Kama leo ungekuwa ndio unatimiza miaka 26 ungefanya nini?

Burn the bridge _Tz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2021
Posts
2,319
Reaction score
6,878
Mfano una miaka 27
Hujaoa wala huna mtoto
Una shahada
Huna kitanda wala asset yoyote
Huna fani yoyote

Je ungetafuta fani gani, ingeishia wapi?? Vipi kuhusu mahusiano.

Naandika hivi kwa sababu vijana wengi wanapoteza dira kwa kukosa maelekezo kutoka kwa kaka zao

Ahsante
 
Yani una shahada halafu huna fani yoyote?

Acha kujicompare na wengine.
Kutokana na tatizo la ajira, kwa sasa inatakiwa kijana hata kama una academic qualifications inatakiwa utafute fani nyingine ili uweze kusurvive unless otherwise itateseka sawa na wale ambao hawajasa

Hapa nina maana kwa fani kama
Maendeleo ya jamii
Ustawi wa jamii
Usimamizi wa rasilimali watu
Usimamizi wa biashara
Afisa utamaduni
Uhusiano wa kimataifa
Uchumi nk
 
Mfano una miaka 27
Hujaoa wala huna mtoto
Una shahada
Huna kitanda wala asset yoyote
Huna fani yoyote

Je ungetafuta fani gani, ingeishia wapi?? Vipi kuhusu mahusiano.

Naandika hivi kwa sababu vijana wengi wanapoteza dira kwa kukosa maelekezo kutoka kwa kaka zao

Ahsante
fani ya nn wakati nina degree aisee hapo ni kuwa WINGA TU
 
Hapo umemaanisha nini?
Utateseka sawa na wale ambao hawana fani.
Kaka nina maana kwamba asaivi kuna tatizo sana la ajira

So kama mtu una taaalmu kama ualimu nk ambazo ni academic qualifications inatakiwa kuwa na fani ingine ya mikono ili uweze kusurvive kwenye maisha ya kila siku

Hiyo ndio maana yangu
 
Utateseka sawa na wale ambao hawana fani.
Kaka nina maana kwamba asaivi kuna tatizo sana la ajira

So kama mtu una taaalmu kama ualimu nk ambazo ni academic qualifications inatakiwa kuwa na fani ingine ya mikono ili uweze kusurvive kwenye maisha ya kila siku

Hiyo ndio maana yangu
Tatizo lako unajicompare na watu wengine right?

kuna watu hawana shahada, diploma,cheti wala skills ya aina yoyote ile lakini life lao linasonga.
 
At 18 hadi 26 ni muda wa kujaribu na kujifunza mambo mengi, at 27 ni muda ambao inabidi uwe umeshajua cha kufanya kwenye maisha yako uanze hata kwa kiasi kidogo ila uwe umeshajua cha kufanya, ni jambo la hatari kama bado huna hata cha kukuingizia kipato

Wahi haraka kutafuta cha kukufanya ujitegemee lakini nakushauri kwanza tafuta uzoefu.

Kajifunze skill chini ya wazoefu, unaweza kwenda moja kwa moja au nenda veta miezi michache then nenda sehemu wanazofanya hizo shughuli, kama umejifunza kuchomelea mageti tafuta workshop, kama umejifunza biashara tafuta duka uwe unauza kuwajua wateja kabla hujatia mtaji kwenye duka lako, kama umejifunza kunyoa tafuta ofisi yenye mzoefu aku guide, kama umesomea mambo ya tour guide tafuta watu wanaoenda huko mbugani, tena sikuhizi hakunaga bure bure ikikubidi toa hela kabisa, unapatiwa ujuzi ambao hautaktoka.

Ikipendeza zaidi focuss na biashara ambazo sio rahisi kuathirika kama Chakula, Usafiri, Afya, Elimu, Kilimo,

Epuka sana Kupoteza muda na pesa kwajili ya wanawake na sex, pombe, betting, social media, marafiki wasio na msaada kimaendeleo, n.k. ni vitu ambavyo vimewafanya vijana wengi wanajikuta wamefika 35 hakuna walichofanya.


Umri uliopo unaweza kujiona bado mdogo lakini ni kufumba na kufumbua tu ushafika 35 hata sura ishaanza kukaza, ukisahafika umri huo hata kupata ajira au kupata sehemu ya kujitolea kupata uzoefu ni ngumu sana, kila unakoenda wanakwepa watu wazima wanataka vijana wadogo
 
Back
Top Bottom